mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza Wizara ya Elimu na ile ya Usalama wa Ndani kuharakisha mwongozo na mikakati ya kufungua shule na maeneo ya ibada itakayohakikisha usalama wa wanafunzi walimu na waumini.
Alisema haya huku idadi ya walioambukizwa iliyotolewa jana ikiwa 59 huku watano wakifariki, Nairobi na Mombasa. Jumla ya maambukizi sasa yamefika 2021 na waliokufa ni 69.
Rais alisema kwamba wazazi hasa walio na wanafunzi wanaofanya mitihani mwaka huu wana wasiwasi kuhusu hatima ya watoto wao na mikakati inafaa kufanywa ili kufungua shule kwa utaratibu.
“Ninaagiza wizara ya Elimu kuharakisha na kukamilisha mashauriano yanayoendelea na washikadau yatakayofanikisha shule nchini kuanza kufunguliwa,” alisema.
Rais alisema mwongozo wa kufungua shule unafaa kushirikisha kanuni ambazo shule na taasisi za elimu zitazingatia ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi.