Rais Kenyatta afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kenyatta.jpg

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri. Katika hotuba yake ya kwanza katika mwaka wa 2020 aliyoitoa kwenye Ikulu ya Rais Mombasa amemteua Monica Juma kama Waziri wa Ulinzi huku Raychelle Omamo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Ukur Yatani ameteuliwa kama Waziri wa Fedha, Mutahi Kagwe Waziri wa Afya huku Betty Maina akichukua Wizara ya Viwanda na Sicily Kariuki akiwa Waziri wa Maji.

Pia ameweka kipaumbele katika biashara na kusema kuwa juhudi zinafanywa kusaidia biashara ndogo ndogo. Pia ametaka nchi kutoa umuhimu kwa uchumi badala ya siasa.

Aidha, Rais amesema kwamba anaamini hakuna utawala ambao umekabiliana na ufisadi kama alivyofanyika kwenye utawala wake. ''Kuanzia mawaziri mpaka magavana, maafisa wa kiserikali, maafisa wa ununuzi, nimekuwa mstari wa mbele. Rais Uhuru ameonyesha imani kuwa ufisadi umeogopesha wezi wa mali ya umma na kuacha mpira kwa mfumo wa mahakama akiitaka iwajibike kuhakikisha kuwa nchi inashinda vita dhidi ya ufisadi.

Miongoni mwa aliyoyazungumzia ni utoaji wa fedha za ujenzi wa viwanda viwili vya maziwa.

Esther Koimett Waziri wa Habari na Mawasiliano. Simon Chelugui ni Waziri wa Leba. Peter Munya ndio Waziri wa kilimo huku Mwangi Kiunjuri akipigwa kalamu na wengineo.

Wakati wa hotuba yake Rais amesema kwamba wanaweka mipango ya kukwamua uchumi na kuweka wazi kuwa asilimia 70 ya madeni yamelipwa.

Source: BBC Swahili
 
Anafuata nyayo za mzee baba. Ngoja tuone kama na yeye atahamisha wanyama kuelekea maeneo ya home kwake
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri. Katika hotuba yake ya kwanza katika mwaka wa 2020 aliyoitoa kwenye Ikulu ya Rais Mombasa amemteua Monica Juma kama Waziri wa Ulinzi huku Raychelle Omamo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Ukur Yatani ameteuliwa kama Waziri wa Fedha, Mutahi Kagwe Waziri wa Afya huku Betty Maina akichukua Wizara ya Viwanda na Sicily Kariuki akiwa Waziri wa Maji.

Pia ameweka kipaumbele katika biashara na kusema kuwa juhudi zinafanywa kusaidia biashara ndogo ndogo. Pia ametaka nchi kutoa umuhimu kwa uchumi badala ya siasa.

Aidha, Rais amesema kwamba anaamini hakuna utawala ambao umekabiliana na ufisadi kama alivyofanyika kwenye utawala wake. ''Kuanzia mawaziri mpaka magavana, maafisa wa kiserikali, maafisa wa ununuzi, nimekuwa mstari wa mbele. Rais Uhuru ameonyesha imani kuwa ufisadi umeogopesha wezi wa mali ya umma na kuacha mpira kwa mfumo wa mahakama akiitaka iwajibike kuhakikisha kuwa nchi inashinda vita dhidi ya ufisadi.

Miongoni mwa aliyoyazungumzia ni utoaji wa fedha za ujenzi wa viwanda viwili vya maziwa.

Esther Koimett Waziri wa Habari na Mawasiliano. Simon Chelugui ni Waziri wa Leba. Peter Munya ndio Waziri wa kilimo huku Mwangi Kiunjuri akipigwa kalamu na wengineo.

Wakati wa hotuba yake Rais amesema kwamba wanaweka mipango ya kukwamua uchumi na kuweka wazi kuwa asilimia 70 ya madeni yamelipwa.

Sababu ya kuondolewa Waziri wa Kilimo Bw. Mwangi Kiunjuri ni kusema "Ruto hawezi kuwa 2022 " wakati Mh. Ruto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya.

"Ruto hawezi kuwa 2022"

Back
Top Bottom