Rais Kenyatta apitisha Muswada wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni; faini hadi Kshs. milioni 5 kwa habari ya uongo

Nenda kasome na kaitafute hakika utaamini kuwa tanzania sheria yetu ya mitandao ni nzuri sana na hakika wakenye wanayo kazi.....mfano kusambaza za utupu ni kifungo cha miaka 10
Hapa makamanda watakaa kimya na kujifanya hawakuona kwa sababu tu Kenyatta wao kasaini (tena kwa mkono wa kushoto).
 
Jamhuri ya Kenya imepitisha sheria kandamizi ya masuala ya mitandao. Pamoja na mambo mengine sheria hiyo itapunguza sana Uhuru wa Kujieleza na kuminya investigative journalism.
Source; BBC Swahili 16/5/2018
Hehe, nimeisoma yote yani ya Tanzania ina unafuu Mara 1000...

Faini million mia ukiandika habari ya uongo[emoji23][emoji23]
 
Katika hali ya kawaida Uhuru bila mipaka ni uchizi! Kuna watu wanadhani Uhuru wa kujieleza hauna mipaka,tukiacha iwe hivyo hatutakuwa na jamii,tutakuwa na genge
Ni kweli mkuu, Uhuru ni lazima uwe na mipaka maana ukizidi pia ni KERO kwa wengine..
 
Hapa [HASHTAG]#jiwe[/HASHTAG] lazima liseme bora ya kwetu inatoa adhabu ndogo kuliko ya jirani zetu Kenya ili kujustify dhulma waliyowafanyia Tz.
 
Katika hali ya kawaida Uhuru bila mipaka ni uchizi! Kuna watu wanadhani Uhuru wa kujieleza hauna mipaka,tukiacha iwe hivyo hatutakuwa na jamii,tutakuwa na genge
Ni uzuzu tu wa miafrika na ngozi zao nyeusi kama roho zao, huo uhuru unamipaka afrika tu, afrika yuna muda wa kushughulikia mambo ya kijinga tu mambo ya maana hatuyawezi.wenzetu ujinga kama huu waliasha achana nao.

Uhuru wa kuongea unazuiaje maendeleo?
 
Kenyatta ameona jinsi kondoo wanavyosagwa kirahisi hapa TZ ikabidi na wao wa-adopt sheria hiyo kandamizi.
 
Hapa wakenya kimya, kumbe zile mbwembwe tu sasa mnavyochukiana hiyo sheria lazma mtanyooshana sana
 
Kwa utaratibu huo, wakenya wameanza kufuata mfumo wa rule of law.
 
Sirudi Afrika. Yaani maskini wana tabu sana, upumbavu umewajaa kichwani, kila wanachofanya ovyo, ushamba mzigo. Huyu kama kaanza kumuiga Pombe akichanganya na madawa yake ya kulevya kwisha habari yake. Ovyo kabisa, yaani Afrika hakuna penye uafadhali. Wote makalio tu
 
Tulilalamikia sana sheria za mtandao na kuwasifia majirani zetu, sijui kuna unafuu gani katika hili make na wao sasa zamu yao imefika, na yafuatayo ndi yaliyomo kwenye sheria zao kandamizi,

BEWARE!

President Uhuru Kenyatta assents to Cybercrimes Bill;

1. It criminalizes abuse of persons on social media removing legal lacuna or publishing of speech that is deemed harmful to someone's Reputation.

2. It criminalizes publishing/posting of false news or stories.
Clause 12 of the law, publishing of a false or fictitious information will attract a Sh.5 million fine or a two-year jail term, the jail term to extends to 10 years if the false information is calculated to cause panic chaos or violence.

3. It Criminalizes sharing of Pornographic materials on Social media(Images, videos). This will attract a fine of upto Sh.10M or Jail term of upto 30 years.

4. The Law outlaws unauthorised access and sharing of government data or confidential information, these provisions are likely to deal a blow to the public-interest defence that protects whistle-blowers.

The new law imposes hefty fines and long prison terms for cyber bullies and fake news dealers. It also targets journalists, media houses, social media users, bloggers and other internet users.

Tujadili na kuangalia kati yao na sisi wapi kuna unafuu? Je, na wao wana cha kutucheka sasa kuhusu sheria za mtandao? Kuna wengine walisaini vijalida vya kuilaumu Tz kutoka huko Kenya...wanasemaje sasa?
 
Katika hali ya kawaida Uhuru bila mipaka ni uchizi! Kuna watu wanadhani Uhuru wa kujieleza hauna mipaka,tukiacha iwe hivyo hatutakuwa na jamii,tutakuwa na genge
Hii sentensi,"Uhuru wa kujieleza" unafahamu maana yake!?
 
TUNAANIKA NA KUWEKA HADHARANI MTANDAO NA SAFU YA WAHUSIKA WA UTAPELI, UNYAG’ANYI NA UPOKONYAJI DHALIMU (VITENDO VYA UHALIFU/JINAI) WA NYUMBA YA MJANE PRUKERIA PONCIAN BALILEMWA, MALI YA MUMEWE MAREHEMU PONCIAN P. BALILEMWA KIWANJA NA. 95 KITALU G, CT. NO. 1151 KATA YA NYAMANORO JIJINI MWANZA KWA UMMA NA MBELE YA MAHAKAMA KUU YA RUFAA KAMA IFUATAVYO:-


SEHEMU YA KWANZA


1. Benki – “NATIONAL BANK OF COMMERCE LIMITED (THE DEFUNCT)

Wamegundulika kuhusika na mchezo mchafu wa utapeli wa kudai mkopo usiojulikana juu ya nyumba tajwa wakitumia mawakili wa kampuni ya IMMMA – hasa waheshimiwa mawakili Bw. Zephrine Galleba, Sadock D. Magai, Lau K. Masha na Faustine Anton Malongo – kuanzia mwaka 2000/2001 – 2003, 2003 – 2006, 2009 – hadi sasa. Katika miaka yote hii benki ya NBC LTD ilikuwa haipo (ilifanyiwa marekebisho na kuzaa NMB, NBC – 1997 LTD na CHC – Mkusanyaji madeni ya benki ya zamani ya NBC LTD), 1997.

- Wahusika wa benki ya NBC LTD waliojitokeza na kuteua kampuni ya IMMMA na kuwaidhinisha kuwa ni kabidhi/mfilisi wa kuuza nyumba isio na mkopo wowote ni :- GERALD JORDAAN (Mkurugenzi), A.M. MINJA, DEREK DE VILLIERS (Makao makuu DSM) – Manager Collections na Meneja wa Tawi la NBC LTD – MWANZA (Demand notices of 2000 & 2001).

- Kesi Na. 117/2001 MAHAKAMA YA WILAYA YA MWANZA PRUKERIA PONCIAN BALILEMWA DHIDI YA NATIONAL BANK OF COMMERCE. Mshitakiwa NBC LTD aliweka pingamizi dhidi ya kushitakiwa kwake akidai si mhusika wa mkopo daiwa wala hahusiki kukusanya madeni ya benki mfu ya NBC LTD bali mhusika ni shirika la CHC (CONSOLIDATED HOLDING CORPORATION). Uamuzi ulitolewa tarehe 14/01/2003 kwa pingamizi kukubaliwa na kuondokana na kesi dhidi yao kuwa sio wahusika. Mahakama hii ilitenda haki vyema - tunaipongeza.


2. Tarehe 13/07/2001, kupitia TANGAZO katika gazeti la NIPASHE uk. 13 KAMPUNI YA MADALALI YA COMRADE AUCTION MART & COURT BROKERS wa S.L.P 61503 DSM: 0744-262461 wakatangaza wakidai kupewa idhini na SADOCK D. MAGAI na LAU K. MASHA wa kampuni ya IMMMA (ISHENGOMA, MASHA, MUJULIZI NA MAGAI) kuuza nyumba lalamikiwa miongoni mwa nyumba zingine katika mikoa ya: MWANZA, BUKOBA, SHINYANGA, TABORA na KIGOMA.


3. Tarehe 28/11/2003 NBC LTD waliojitoa katika kesi Na. 117/2001, wakala njama na utapeli wa hali ya juu sana pasipo kufahamika wala kutoa taarifa kwa mama mjane (mdhulumiwa) Prukeria kuwa hati ya nyumba yake/ya mumewe ilifanyiwa uhawilishaji (TRANSFER) kwa na kuwa ni mali ya RIZIKI MBISE (Maarufu kama MAMBO YA CHINGA), na kwamba uhawilishaji huo umefanywa na benki mfu ya NBC LTD tarehe 28 Novemba 2003 na HATI YA UHAWILISHAJI WA KITAPELI ulifanywa na KAMPUNI YA IMMMA Plot No. 357 UNITED NATIONS ROAD, UPANGA, P.O.BOX 72484 DSM naye Bw. RIZIKI MBISE hati yake hiyo feki kuthibitishwa mbele ya Mh. MILLINGA, W.J – Wakili wa serikali P.o. Box 331 MWANZA tarehe 18 Desemba 2003 akitambulishwa na Bi. SOPHIA M’KITOSI. Hati ya TRANSFER inaonesha benki kuiuza kwa RIZIKI MBISE Tshs. 4,600,000.00 chini ya thamani ya majengo-nyumba ya mbele na nyuma yenye thamani ya zaidi ya tshs. 250,000,000.00


Tarehe 25/09/2000 mjane Prukeria P. Balilemwa baada ya kupokea Demand notices kadhaa kutoka NBC LTD ambayo alifahamu na kujua wazi kuwa haipo na kutilia mashaka taarifa zake za mkopo na dhamana ya nyumba visivyojulikana wala kufahamika aliamua kuiandikia benki ya NBC (1997) LTD – The Director Collections kutaka kujua kama wao ndio wadai/wakopeshaji watoe ushirikiano kwake kwa kumpa taarifa kamilifu na za uhakika kama kuna mkopo-daiwa kwa marehemu mumewe asioujua ambao haujui ili ashirikishe wanafamilia kutatua tatizo na adha ya kusumbuliwa-sumbuliwa na taarifa nyingi za kampuni ya IMMMA. Barua hiyo iliyonakiliwa kwa Branch Manager, Nyerere Road-Mwanza ilitumwa Posta kwa njia ya rejesta tarehe 27/09/2000. Tangia kutumwa kwa barua hiyo hadi leo haijawahi kujibiwa wala benki kujitokeza kujibu lolote licha ya jitihada nyingi za mlalamikaji-mdhulumiwa kufika mala kadhaa NBC (1997) LTD kupewa taarifa pasipo mafanikio yoyote.


4. Mamlaka za ardhi ambazo zinatuhumiwa kuhusika na mchezo huo mchafu wa hadaa, utapeli na utwaaji wa kidhalimu wa nyumba – lalamikiwa ni Ofisi/idara ya usajiri wa Hati-Mwanza Bi. Mziray kwa tarehe tofauti tofauti katika mwaka wa 2005 kwa kuhusika na usajili wa uhawilishaji umiliki (transfer) na kubadili jina la mmiliki halisi na halali kwenda kwa mmiliki wa kitapeli Bw. Riziki Mbise. Mamlaka nyingine ni HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA. Halmashauri hii ikijua wazi kuwa mmiliki wa ardhi/nyumba bishaniwa kuwa ni Poncian Petro Balilemwa kwa uchunguzi rasmi uliofanyika (official search) miaka ya 2006 na 2009 ilibainisha kuwa ni miliki ya Bw. Balilemwa. Lakini ilipofika tarehe 12/10/2009 wakatoa taalifa watendaji watatu (3) tofauti kwa tarehe hiyo hiyo na wenye majina yaliyofichika, saini zisizojulikana na vyeo (designations) visivyotambulika kuwa mmiliki ni RIZIKI KALEBI MBISE.


NB: (i) PONGEZI KWA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA PALIPO NYUMBA YENYE MGOGORO KWA UMAKINI NA KUMTAMBUA MMILIKI HALALI WA NYUMBA HUSIKA KUWA NI PONCIAN PETRO BALILEMWA TANGIA MWANZO 1980s – 2015/2018 NA KUWA NDIYE MWENYE JUKUMU, PIA, LA KULIPA KODI ZA ARDHI NA PANGO.

(ii) Baada ya taarifa hii tutaendelea kuwasilisha taarifa juu ya mamlaka za: WIZARA YA ARDHI NA NYUMBA, TAASISI ZA UCHUNGUZI kuhusiana na uhalifu, rushwa, usimamizi na utoaji wa haki kwa namna walivyoshiriki na kendelea kushiriki kuipotosha sheria na kuipokonya haki bila huruma, maadili na kanuni za utendaji na bila kuzingatia utawala wa sheria.


TUNA USHAHIDI WA KUTOSHA NA USIOTILIWA MASHAKA NA KAMWE HATUMWONEI MTU NA HATUTARAJII MTU KUONEWA, BALI NAOMBA MKUU WA NCHI, RAIS WETU MR. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFURI AIAGIZE MAMLAKA HUSIKA ZIWAJIBIKE KWA HAKI.



Chanzo: 1. Wanafamilia (mama mjane) 12/05/2018

2. TBC1 Habari - 11/05/2018
 
Mambo yote yanatoka magharibi,its not our world.
 
Lakini haijataka watu wanaotumia social media kutambulika, pia haijataka usajili wa blogs, haijataka usajili wa online TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…