Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Kwa nini vikwazo vilikuwepo in the first place?
 
Huo ni mtego, Watanzania tujihadhari kesho tutageuziwa kibao, ndio maana nchi kama Marekani, inajaribu kupunguza biashara na China ila kulinda soko la ajira na biashara kwa Wamarekani.
Fanyeni kazi wacheni ndoto za kuogopa ushindani mliojengewa vichwani mwenu na jiwe.

Hakuna maisha yasiyo na changamoto za kiushindani.
 
Achana nao hao wengine kazi kulalamika tu

Kenya wamejivua lawama kuwa nsiseme ohh permit ngumu kupata ohh visa ngumu kupata .Haya njooni mfanye kazi au biashara zenu free bila kisingizio .

KENYATTA KAFANYA JAMBO KUBWA
 
Wewe nani hadi ushindane na maamuzi ya rais ambayo kimsingi ni ya kimaendeleo.

Huoni kuwa ametufungulia milango ya kufanya biashara ?

Njoo hapa Arusha uangalie leo watu tunavyo furahia hiyo fursa .

Tutapeleka mahindi kenya, vitunguu, maharage, mbaazi hayo mazao kenya yana soko kubwa tu.
 
Hakika mkuu hapo tuna peta kabisa maana hali ilikuwa siyo yenyewe
 
Huo ni mtego, Watanzania tujihadhari kesho tutageuziwa kibao, ndio maana nchi kama Marekani, inajaribu kupunguza biashara na China ila kulinda soko la ajira na biashara kwa Wamarekani.
Kwa kufanya hivyo Trump aliua biashara za wamarekani ku compete globally na kuharibu soko lao marekani sababu manifacturing facilities zao ziko China ndio maana walimpiga chini uraisi

China cheap manufacturing costs makampuni kibao ya kimarekani yakakimbilia kule
 
Wanao lalamika ni wale waliozoea kudekezwa tu .
Sisi wauza mahindi na vitunguu huu ndiyo muda wetu sasa kufanya kazi na wakenya.
 
Wakenya hawafai, narudia tena Wakenya hawafai.Cheza mbali na Wakenya ni watu na nusu wale
Mtajijua sasa wakati wenzenu ndiyo kwaanza kumekucha na tunamshukuru sana mama Samia .
 
Mimi nakuelewa sasa kauli yetu kila siku tuna imba tunataka wawekezaji waje ina maana gani wakitokea watu wanataka kuwekeza tunaanza kushtuka hawa wanataka kutuibia. weka sheria za kulinda haki ya nchi, mwekezaji akija kitu kikubwa atataka ardhi ya kuwekeza na ni kazi ya serikali kuwapa ardhi. Mama kasema sisi tuna ardhi kubwa nyinyi mna mtaji tufanye biashara. Mimi sisemi kuwamilikisha ardhi ila kuwapa ardhi ya kufanya uwekezaji. USA wakati wanakuja kigamboni watu wakaanza tunauza ardhi haiwezekani hao wakaondoka kila kitu kikadoda. Hii tabia tunataka hatutaki ndio shida. Hawa Dubai hawana chochote zaidi ya kuithamisha ardhi yao na leo ni moja ya ardhi bei kubwa na uwekezaji mkubwa.
 
Hii kwa sie watu wa zamani kidogo tunakumbuka kisa cha Ubasha cha zamani saana, jamaa aliingia town akaambiwa huku ukilemaa watu wanakupelekea moto. Akaanza kuuza embe na kumenyea watu huku mkali kama simba, sasa wakaja watu kumbahashia akahamaki na kwa bahati mbaya akajikata kidoleni sasa wajuba wakamwambia dawa ipo ila anatakiwa kuzamisha iko kidole katika tigo ya mjuba na mjuba alikubari na akaona sio kesi ili upone we weka tu.

Zikapita siku 3 -4 hivi kaja mjuba na kidole chake kimeumia kafata dawa kwa muuza embe, ebana heee .....................................japo ashakum si matusi.

Wenzetu wa Kenya hili watupe muda kidogo manake kuliwa hatutaki.
 
Wanao lalamika ni wale waliozoea kudekezwa tu .
Sisi wauza mahindi na vitunguu huu ndiyo muda wetu sasa kufanya kazi na wakenya.
kabisa unajibebea mwenyewe unaenda nayo moja kwa moja sokoni kenya bila mtu wa kati au unenda fungua kabisa godown la kuuza mazao yako kule

Wafanyabiashara wa mazao fursa hiyo
 
Omba omba kutoka 🇰🇪 Waje 🇹🇿 Wafanye nini? Na hizo pesa zenu zisizo na thamani?

Make it make sense
Thamani ya pesa au utoaji?

Maana Kenya tofauti na hapa Tanzania mtu anaweza kukuelezea shida na ukimuelewa unaweza kumpa hata elfu 5 na sio kule kila mtu ana pilika zake.

Tanzania ni nchi na wananchi wake wenye UTU na roho nzuri. Binafsi Kenya naijua sana,Wakenya ni wabinafsi, hawana UTU na wana roho mbaya sana.

Mfano Jaribu kupanga halafu useme umepata tatizo la ki fedha hauna kodi,tofauti na Tanzania unaweza kueleweka na mwenye nyumba akakupa muda.

Unafikiri mama ndio kaenda na muarobaini wa kumaliza tatizo la misuguano ya mara kwa mara Tanzania na Kenya?
 
Hii fursa Kenyata aliyotupa itakuwa haina maana kama kitengo cha kutoa passport kitakuwa kizito kuzitoa na urasimu wao wa kutaka sijui barua za mwaliko sijui nini.Watoe watu wakatafute fursa kenya
 

I have lived in Nairobi , what you are saying is very true, wakenya wako sharp sana and proficient , huyu mama kwa kweli anakoenda hapana. Huyu mama anataka kujifanya anafuraisha watu itakula kwake
 
kabisa unajibebea mwenyewe unaenda nayo moja kwa moja sokoni kenya bila mtu wa kati au unenda fungua kabisa godown la kuuza mazao yako kule

Wafanyabiashara wa mazao fursa hiyo
Shauri zenu kaeni na majungu yenu mtakuja kuletewa ridhiki zenu na jiwe
 
Hii fursa Kenyata aliyotupa itakuwa haina maana kama kitengo cha kutoa passport kitakuwa kizito kuzitoa na urasimu wao wa kutaka sijui barua za mwaliko sijui nini.Watoe watu wakatafute fursa kenya
Wacha kudanganya watu wewe.
Lini umeenda uhamiaji kutaka pasipoti ya kwenda east Afrika ukaambiwa lete barua ya mwaliko?
 

Watz wengi hawajawahi kufika hata hapo kenya, hawajui the impact itakayotokea once wakifanya wanachotaka kufanya. Wakenya wenzetu Sijui walimpa nini Mungu , wako very sharp kichwani, wana akili za kutisha na ni quick learner , mkenya unaweza kumuweka kwenye kazi ambayo hajasomea ukamtrain within a short period of time akawa maste kuliko hat waliosomea. Huyu Mama Sijui anatupeleka wapi , tufanye tu uchaguzi kwa kqeli tunahitaji kiongozi makini sana
 
Fanyeni kazi wacheni ndoto za kuogopa ushindani mliojengewa vichwani mwenu na jiwe.

Hakuna maisha yasiyo na changamoto za kiushindani.
Hili ni somo gumu sana watanzania kuelewa. Wanajua dawa ni kujifungia tu humu na ufukara wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…