Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Huko Tz, kuna kitu ka hicho wakenya wamepata? Na bado utakuta wabongo wengine wakilalamika!
 
Bora tutalalamike lakini tutajifunza kitu mkuu
 
ni kweli mkuu..
lengo lake ni tanzania iseme the same, ili pia waje wafanye biashr upande wa pili bila permit..

na sisi tukifuata hilo, wakenya watakuwa wame win
Hapo umemaanisha nini? So nyie wa Tz kutolewa vikwazo hivyo na rais Uhuru, nikufeli mmefeli au wasemaje?
 
Na ujinga.yaani tuna ujinga mwingi hadi inasikitisha.
 
Na hii kitu ya kodi inafaa kuzungumziwa. Wafanya biashara wa Sector mbalimbali KE wamelalamika ju ya kutozwa kodi ya juu sana wakileta bidhaa Tz au wakitaka kuanzisha biashara flani huko, wakati huku KE hakuna udhalilishaji ka huo kwa wafanyabiashara wa Tz.
 
Shida yetu iko hapo..tunamuogopa kila mtu..hv why lakini?sijui niNyerere au nani alitujaza ujinga wa kuogopa ogopa kila kitu! Tujaribu tukiona wanatuzid akili mamlaka zipo!khaa
Sisi ni makondoo.hatuko aggressive kwenye mambo ya msingi.Tunataka tu kupiga porojo za mdomoni,majungu na umbea.
 
Hivi kenya kuna ajira gani kwa watanzania,hili chaka la working permit tusijaribu kuliingia kwenye biashara hapo sawa,kwenye ajira watuache kwanza kidogo
Kama huna sifa unataka uajiriwe vip.Dunia ya sasa ni mapambano na kama huwezi kupambana kaa tulia wenye uwezo watapambana.Hakuna nchi ambayo haina fursa mambo mengine yatategemea uwezo wako wa akili na kutenda.
 
sema hawa jamaa sjawahi kua na imani nao, uwekezaji ni muhimu sawa ila sheria ziwekwe nzuri haya mambo ya kubrand mlima kilimanjaro kenya iwe mwisho
Huo mlima Kilimanjaro haujabrandiwa kuwa wa Tz, hata kwenye issue za guide books wanaonesha kabisa mlima uko Tz ila ukiwa Amboseli Game Park unaweza pata view yake pia. Ukiwa msafiri nafkiri utaelewa nacho zungumzia hapa!
Na hapo kumbuka faida kwenyu pia, watalii wakitaka kuuona full, si tunawaleta Tz au wao wenyewe wanaweza kuja next trip huko?
 
Wakenya wajanja, hata kama huna work permit, wala business visa, kazi hupati Kenya.. Mtanzania hawezi pewa nafasi na wakenya kufanya kazi.. Sisi tusiruhusu hilo, eti wakenya waje free huku, hilo litakuwa kosa kubwa sana kutokea
Kasome kwanza upate shahada, na uwe na washkaji huku, alafu njoo KE. Hakuna mteremko kwenye maisha ya hustling, labda uwe mtoto wa Sheikh Khalifa! 🤣
 
Sisi ni makondoo.hatuko aggressive kwenye mambo ya msingi.Tunataka tu kupiga porojo za mdomoni,majungu na umbea.
Hivi kwanini tuko hivyo sasa? Kuna mdada nilikutana naye 3yrs ago anatoka kenya anakusanya🌻🌻🌻🌻🌻 mikoa yenye alizeti ana kampuni so anaprocess mafuta ya alizeti sana anaenda uza huko!
Yule bidada hana maongezi kama ya kitz...yaan hata ukimpgia simu inabidi umchallenge vitu vya msingi..sasa sisi si wanawake si wanaume tunapenda petty issues balaa..hivi ni LAANA au kuna kiongoz huko nyuma alishaharibu kuturithisha?
Haiwezekani ukamuogopa binadamu mwenzako eti kisa anaakili kukuzidi wewe...kwanini usiombe huo weledi ukawa nao wewe! Mie bongo jamani sina hata la kusema! Nasema sina
 
Unataka tuendelee kua makondoo mpaka lini.Unaposhindwa kua na uwezo wakupambana maana yake wewe ni dhaifu sasa namna yakuondoa huo udhaifu sio kujifungia ndani bali kutoka nakujifunza kwa yule aliyekuzidi.Tukumbuke miaka inaenda tusiporekebisha mapungufu yetu sasa iko miaka kitakuja kizazi kitakachokua hakiwezi chochote wakati huo wenzetu watakua wameshafika mbali kwenye kila nyanja.Na athari za huu ukondoo zinagusa jamii nzima kuanzia uchumi,elimu,burudani na mengine yakijamii.Kwahiyo tutafute ufumbuzi wa matatizo yetu badala ya kujificha.
 
Mkuu unachekelea na yeye mama atafanya the some....uone ajira zote zitachukuliwa na wakenya Hadi uwalimu.....kwasababu wako smart na agressive....time will tell utakujaa kulala Mika hapa tenaa
Kinachotushinda sisi kua kama wao au zaidi yao ni nini,au sisi ni matahira?,au vilema,hebu tujiulize maswali ya msingi ili tutafute ufumbuzi wakudumu.tuache kulia lia.
 
Oya una undugu na hii id ya makaveli10
 
Muda wakufanya hayo ulishapita.tuko nyuma ya muda kwahiyo ni vyema tukaamsha vichwa tukiwa ndani ya mpambano.Kama tu kwa huu utulivu tulionao tumeshindwa kuboresha elimu yetu iwe na viwango vyakueleweka unadhani itatuchukua karne ngapi kubadilisha jamii nzima mentallity ya kinyonge tuliyonayo.
 
tutaenzi kufundisha watu wetu kufanya kazi kwa bidii, tuanze kufundisha skills kwa watu wetu, tuanze kuwapa watu wetu elimu bora halafu ndio tuingie kwenye mashindano ya namna hii otherwise watu wetu watakauwa wanafanya kazi za chini sana....
Haya mawazo ilitakiwa yafanyike miaka ya uhuru sio sasa.Ata uko kwenye soka si unaona baada yakugundua viwango vya wachezaji wetu viko chini na ili wapate exposure dawa ni kuwachanganya na wachezaji kadhaa wa kigeni.Kwa kufanya hivyo naamini yako mabadiliko mengi kwa wachezaji wetu hasa kwa wale wenye nia ya kujifunza.Tukiendelea hivyo tutatengeneza wachezaji wengi wenye moyo wakujituma na kua serious na kazi kuliko tungesema wafundishwe kwanza nadharia yakujiamini na kujituma alafu badae ndo waingie kwenye ushindani.
 
Hapo matatizo ni yetu sio wao.Tatizo letu tumeridhika sana na maisha ndo maana tunajua vizuri matatizo yetu lakini hatutaki kuyapatia ufumbuzi zaidi yakupiga tu porojo za maneno.
 
Naungana nawe kwa kila kitu kwwnye uzi huu...tuache hofu zisizo na maana jamani
 
Wakati wa mgomo wa madoctor wa Kenya waliomba madoctor wa huku ilikuaje waliambiwa Kama hawajitaki waende Nini kilifuatiaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…