Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Rais Kenyatta aruhusu Watanzania kuanza kufanya kazi na biashara Kenya bila kuwa na Work Permit wala Business visa

Kigelegele kwa Kenyatta aruhusu watanzania kuanzia sasa ruksa kufanya kazi na biashara kenya bila kuwa na work permit wala Business visa

Kasema mida hii mkutano wa wafanya biashara
hapana watakuja uza hadi nyanya hawa wakenya wabaki tu kwao
 
Wawekezaji wa Kitanzania waliopo Kenya ni wachache sana ilana wakenya makampuni Tanzania ni wengi tukiruhusu waajiri ndugu zao tumekwisha
 
Kigelegele kwa Kenyatta aruhusu watanzania kuanzia sasa ruksa kufanya kazi na biashara kenya bila kuwa na work permit wala Business visa

Kasema mida hii mkutano wa wafanya biashara
Mwendazake aliziba fursa nyingi sana!! Ni mwanzo mzuri kwa ujirani mwema
 
embu tufikirie nje ya box, balozi zetu zimetupa information gani za opportunities zilizopo kenya kwa watanzania, na how easy kuzi access hizo infor kwa raia wa kawaida.
Kwa hiyo unataka balozi zikuletee taarifa nyumbani kwako za ukafanye nini kenya? utasubiri sanaaaaaaaaaaaa
 
Makampuni mangapi ukilinganisha na makampuni ya Kenya hukuTanzania, imagine waamue kuajiri wakenya kwenye makampuni yao hali itakuwaje?
 
labda sijaelewa unasikitika nn, lakn embu take moment mtu na hela zake mtanzania wa namanyele, ana details gani za aina ya biashra ya kufanya nchini kenya? hajui mtu kenya, na wala asitegemee support ya ubalozi wetu kule...

wao makejipanga. wao tayr wana information za kutosha kwa kila raia wao anayetaka kwnda kuwekeza au kufanya biashr tanzania. possibly atapewa mkopo wenye riba ndogo, atasemehewa kodi kwa upande wa kenya kwa kila bidhaa atakoyo itoa kenya kupeleka tanzania, kwa miaka fulani..

pengine, kwa mkenya atakaye kuja kuwekeza huku, moja ya mashrt ya kupata mkopo kwao, lazma aajir wakenya kiasi kadhaa katika top management, na mshahar usiwe less tha amount fulani..
sisi tumejipanga kwa hili ili tuseme ok njooni?
wao wana hakika hakuna mtanzania atakaye weza kushindana nao katika ardhi yao kibiashar labda mtanznia mwenye asili ya asia.

embu tufikirie nje ya box, balaz zetu zimetupa information gani za opportunities zilizopo kenya kwa watanzania, na how easy kuzi access hizo infor kwa raia wa kawaida.
Nasikitika srikali yetu ilivyotutekeleza....
 
Kigelegele kwa Kenyatta aruhusu watanzania kuanzia sasa ruksa kufanya kazi na biashara kenya bila kuwa na work permit wala Business visa

Kasema mida hii mkutano wa wafanya biashara
Kwa jinsi wakenya walivyo wabaguzi,waTz wataweza kupenya kweli huko Kenya?Au Kenyatta analijua hilo ndio maana amecheza karata yake,ili na Mama Samiah aingie kichwakichwa kuruhusu wakenya huku?!!!
 
ulishawahi kufanya biashara na mkenya? ulishawahi kuishi hata Nairobi tu? ulishawahi kufanya kazi hata za kuajiriwa na mkenya? wabongo tupo polepole sana, visingizio kibao,upeo wa kimataifa mdogo etc, hapo tunatakiwa kurekebika. ukifika Nairobi tu watu unaokutana nao barabarani wako busy wanakimbia kwenda wanakoenda, bongo unakuta mtu anaenda kazini kwake au kwenye kibarua anatembea kama muda ni shemeji yake. huu ndio ukweli. tunatakiwa kubadilika. ndio maana investors wanaependa kuajiri wakenya kuliko sisi kwasababu hizi. bora tena hata bara, ukienda zenji ndio muda utafikiri nini sijui, wako poelpole mamwinyiiiii. unyonge sio wanyonge ila wazembe.
Mkuu hakuna kitu unaweza kunifundisha kuhusu kenya. Nimeishi Eldoret, nimesoma na kuishi nairobi. Nimefanya biashara embu. Ninaifahamu kenya vizuri. na ninajua tukifungulia mipaka...tanzania tutapigika kidogo kwa awali..lakini itatulazimu tujifunze kuchangamka na hiyo itatusaidia kukuza viwango vya watu wetu.

Hii ya kujifungia mipaka ili kulinda watu wetu haitusaidii
 
mimi sioni tatizo waje tu

Ajira sasa hivi hazipo nyingi wataziongeza na hata wakiajiriana wenyewe hakuna shida tutapata kodi zao na mishahara yao watatumia humu humu nchini kununua bidhaa ,vyakula nk
kwa kauli yako ni dhahir umekir kuwa ningumu sisi kwenda kufanya biashara kule, wala kuwekeza kule.

hivyo kauli ya kenyetta kuwa tunatoa permit free kwa watanzania, ni kauli yenye maana ya kuwaomba watanzania wawape wakenya permit free, ila kaigeuza.

kunazo benefit kwa upande fulani, kama ulizosema lakn kuna hasar kubwa sana pia. mfano, mtoto wa mkurigenz wa kcb tanxania ambaye ni mkenya, ata kwalifai kuomba kazi crdb au any foreign company liopo Tanzania, sawa na mtanzania wa kawaida..

ndio tujipange kuwalinda raia wetu pindipo makampuni yao yanakuja, kwamba nafasi fulani kwny management lazima watanznia wawepo. na kulimit namb za raia wao kulingana na kampuni yenye mtaji fulani kutoka kwao.
 
ni kweli mkuu..
lengo lake ni tanzania iseme the same, ili pia waje wafanye biashr upande wa pili bila permit..

na sisi tukifuata hilo, wakenya watakuwa wame win
Mkuu kwanza sidhani kama kuna mkenya anaweza kuja kufanya biashara Tanzania , KRA ipo smooth sana kwa wafanyabiasha wao kuliko sisi, ulishawahi sikia habari ya Efd kenya? au uliwahi kusikia habari ya kufungiana akaunti kwa kesi zisizo kichwa wala miguu?
Sana sana kwa kauli hiyo ya Uhuru ni kwamba anataka kuvuna Watanzania potential ambao mfumo wetu wa kodi umeshawaumiza vibaya , na kuwapa greener pastures huko kenya
 
No..tanzania na burundi ndio hazina political will. Tangia enzi za kikwete kenya, uganda na rwanda wamekua wako tayari kufungua mipaka yao na kuruhusu raia waingie na national ID tu bila passport..tanzania na burundi tumekua tukijivuta vuta. Mpaka wao wakaamua kuanza kwa nchi zao. Mambo ya kufuta work permits wamekua tayari kwa miaka 10 sasa...TZ na Burundi ndio tumekua tunakataa

Uko sahihi, Rwanda walikua wa mwanzo kabisa kwenye hizi jitihada.
 
Huu uwoga na tumeaminishwa na wana siasa kuwaogopa wa Kenya na unyonge ndio shida kubwa, tunawaogopa nini hasa mbona tumejaza wahindi makampuni yote na kila siku wanaingia tu. Ajira ni ushindani na ufanisi ndio inabidi tujiongeze tuwe waadilifu ili sisi ndio tuwe na thamani kwao siku waombe wa Tanzania katika makampuni yao. Tabia ya kuaminishwa kuwaogopa wa Kenya hata sijui nani aliyeileta, Mimi simuogopi mkenya kwa lipi zaidi? tuache unyonge
+1
fear of uknown , wakenya ni wakawaida sana , tunejazwa hofu hadi hatuelewi tufanye nn
 
Safi Sana Maana Waitress wa Ki Kenya walipungua.sana kwenye.Pub na Ma Cassino
 
Wakenya wajanja, hata kama huna work permit, wala business visa, kazi hupati Kenya.. Mtanzania hawezi pewa nafasi na wakenya kufanya kazi.. Sisi tusiruhusu hilo, eti wakenya waje free huku, hilo litakuwa kosa kubwa sana kutokea
Nina imani walioko kwenye system hawawezi kuruhusu hili.
 
Back
Top Bottom