Tuendelee kuchukua tahadhari, nashukuru sana uongozi wa nchi hii, tunapewa taarifa kama zilivyo, hamna kuficha au mikwara, au mikanganyiko ya amri za viongozi, kwamba kila huyu na lake.
Rais Uhuru ameongoza kwenye mstari wa mbele huku akitumia ushauri wa kisayansi, japo amehamasisha maombi ila amekua akiwekeza kwenye kuskliza ushauri wa kitaalam maana kwa sisi waumini tunajua hekima zote na busara na maarifa yote yanatoka kwa Mungu.
Hauwezi ukamshika simba mwenye njaa kidevu huku ukiomba Mungu amzuie asikutafune, itabidi utumie maarifa aliyokupea Mungu uchomoke nduki huku ukiomba asikufikie na kukukamata. Kwa hivyo kuomba Mungu azuie corona huku umekaa kwenye klabu unapiga beer na machangudoa pembeni, hamna utofauti na hilo la kumshika simba kidevu huku ukiomba Mungu....utaliwa tu.