Rais Kikwete amemteua Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Rais Kikwete amemteua Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi

Marata

Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
44
Reaction score
8
Rais JMK amemteua Spika Mstaafu Mh. Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Msekwa mwenye umri wa unaokadiriwa 80+ atashikilia cheo hicho kwa miaka 5 kuanzia 2nd, May 2015.

===============

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Rais pia amemteua ndugu Daudi Rukiko Mayeji kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga. Kabla ya uteuzi huu, ndugu Mayeji alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi , Mkoani Tanga.

Uteuzi wa Ndugu Msekwa na wa Ndugu Mayeji umeanza tarehe 2 Mei, 2015

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu, Dar es Salaam.
4 Mei, 2015
 
Rais JMK amemteua Spika Mstaafu Mh. Pius Msekwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. Msekwa mwenye umri wa unaokadiriwa 80+ atashikilia cheo hicho kwa miaka 5 kuanzia 2nd, May 2015. Chanzo cha Habari Gazetti la Mwananchi.

Ndugu Siyo miaka mitano Counselor Mpaka afe ndo anabadilishwa! mkuu
 
Ndugu Siyo miaka mitano Counselor Mpaka afe ndo anabadilishwa! mkuu

Hapana ni miaka mitano as per Mwananchi ya leo pg 5. Ila tangazo linaonesha uteuzi ni kuanzia 2nd May mpaka baada ya miaka mitano.
 
Si dio hapo akatae kuonesha yeye madaraka basi,ila atakuambia nimeteuliwa...
 
Ndugu Siyo miaka mitano Counselor Mpaka afe ndo anabadilishwa! mkuu
Pius Msekwa alishawahi kuwa Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi miaka ya 1984 na kamaliza muda wake naona wamerudia tena
Hapana ni miaka mitano as per Mwananchi ya leo pg 5. Ila tangazo linaonesha uteuzi ni kuanzia 2nd May mpaka baada ya miaka mitano.
upo sahihi kabisa Mkuu
 
Bado hajachoka kuteua? Shemeji kaondoka na lichama lake hilo. Asante kwa mtaji ulotupa
 
Nasubiria asseme amechoka anataka kupumzika awaachie wajuukuu zake sasa.Vinginevyo hana tofauti na yule aliyemnanga kuwa anapenda UKUBWA NA MADARAKA.
 
Back
Top Bottom