RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba kama nchi ikiendelea kuzalisha wanasiasa kwa wingi itaishia kwenye malumbano na migogoro isiyo na tija, badala yake amewataka Watanzania kuijenga katika misingi ya sayansi na teknolojia.
Akizungumza kwenye mkutano wa sita wa Siku ya Wahandisi nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema njia pekee ya kuiletea nchi maandeleo ni kuzingatia sayansi na teknoliji badala ya siasa ambayo huishia kwenye porojo na malumbano.
Alisema umefika wakati kwa kutumia wataalam hasa wanasayansi kufanisha utendaji badala ya wanasiasa katika mambo yanatakiwa watu waliobobea kwenye fani hizo.
"Tukijaza wataalamu wa siasa tutaendele kubishana tu na tukiwajaza wanasheria tutaishia kufungana, kinachotakiwa sasa ni wataalamu wa sayansi na teknolojia, ili nchi yetu iweze kusonga mbele kimaendeleo," alisisitiza Rais.
Rais alisema pamoja na kazi nzuri ya kufundisha wahandisi inayofanywa na UDSM, bado kuna changamoto nyingi za kuboresha fani hiyo, kama vile ubora wa ufundishaji unaoweza kukidhi mahitaji ya sokoni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vyote muhimu.
Alisema kazi ya uhandisi inahitaji kujiendeleza kimasomo, hivyo aliwataka wahandisi na makandarasi nchini kutotosheka na kiwango cha elimu walicho nacho badala yake watafute nafasi za kujiendeleza kimasomo.
"Heshima ya uhandisi inategemea ubora wa kazi mnayofanya, acheni mambo ya ujanja ujanja," alisonya Rais Kikwete.
Rais Kikwete alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa umoja ili kuondoa tofauti dhana iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwamba wazawa hawawezi kufanya vizuri isipokuwa wanaotoka nje ya nchi.
Alisema kama wahandisi na makandarasi wakifuata maadili ya kazi, shughuli nyingi zinazohusiana na fani hiyo zitafanyika kwa ubora unaotakiwa na kuipunguzia hasara taifa kutokana majengo kuporomoka. .
NIliposoma hii habari, nilijibu kwa kebehi Bwa ha ha ha ha. Lakini katika kujibu hoja ya mtu siku kadhaa baadaye, nikasema kuwa miaka 30 tangu kauli hii ya kuendesha nchi kisayansi itoke, tutaitafakari na kusema kuwa Kikwete alikuwa sahihi.
Naomba nijirudi kwa kuondoa kebehi hii na kuona kauli ya Kikwete kama changamoto. Ikiwezekana, MODS naomba muirudishe hii hoja kule Jukwaa la Siasa!
Mwalimu Nyerere alisema tulipopata uhuru, "wenzetu wanapaa, sisi tunatambaa, inabidi tukimbie tuwafikie" (sina nukuu kamili, lakini huu ni uelewa wangu wa alichokisema Nyerere).
Rais Kennedy wa Marekani aliposema kuwa ni muhimu kwa Marekani kufikisha mtu mwezini, alitoa changamoto ambayo katika miaka kumi, ikawa kweli. Alitoa changamoto kwa wananchi wake na wakaitikia wito
Special Message to the Congress on Urgent National Needs Page 4 - John F. Kennedy Presidential Library & Museum
NImetafakari sana hii changamoto pamoja na kuwa Mkwere huwa anaweka maneno mengi na kuchanganya vitu kama upishi wa mseto, nimeamua nichambue yaliyo ya maana na niyajengee hoja.
Ni kweli hakuna ambalo Kikwete atalisema ambalo tutaliona la maana au umuhimu kwa kuwa tumejipofusha kuona lolote bora kutoka kwake kutokana na udhaifu wa Uongozi wake kuwa makini, fanisi na hasa kushughulikia Uhujumu, Uzembe na Ufisadi.
Nitapokea makonzi yenu kwa unyenyekevu kwa kutamka kuwa Kikwete ni Rais mzuri, katika nyakati mbovu na hata nchi isiyomfaa. Right President at rong country and time!
Nimesema hivi na nitaomba nitumie kilugha cha Pundit kujieleza.
Think of a CEO or Manager who has Macro Management style, always delegating and looks at reports. Most of times, this kind of Manager has a strong competent team and does not require to Micro Manage everyproject and every penny, as long as this Manager and Leader trusts the people supporting him.
Sasa hapa kuna mawili, Management na Leadership.
Kwenye Management, yeye ni Macro Manager, yule ambaye anafaa kuongoza shirika au mradi ambao tayari una ufanisi wa hali ya juu na hahitaji kuchafuka sana au kutoka jasho. Kama Leader, anaruhusu walioko chini yake kujitutumua na kuonyesha ujuzi na utaalamu wao, hivyo ni kuwa-empower wafuasi wake kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha kazi zao na kujieleza.
Lakini pamoja na sifa hizi, Kikwete alichoshindwa kubaini ni kuwa Tanzania inahitaji Micro Manager na Close directive ya Leadership!
Hao anaowaamini kuwa watafanya kazi vizuri, kawapa madaraka makubwa sana na wanajifanyia kazi hovyo hovyo, na yeye Kikwete anafeli kuwa Kiongozi na Mtawala mzuri kwa kuendelea kung'ang'ania kuwa yeye ni Macro Manager, hivyo aachie Uhuru wa watu kujifanyia mambo.
Sasa tukiangalia kufanya kazi kwa kutumia Sayansi na Teknolojia, suala la Macro au Micro Management si la kisiasa tuu, bali ni la kutumia sayansi na teknolojia.
Naipokea changamoto ya Kikwete kwa mtazamo wa kusema ili Tanzania tuendelee, tunabidi turudia kauli ya Nyerere na Kennedy kuwa sasa hivi, siasa basi, tuendeshe nchi kwa kutumia Sayansi na Teknolojia.
Hii si kwa masuala ya Utawala na Uongozi pekee, bali ni kila kitu tunachokifanya. Iwe ni Kilimo, Ufugaji, Biashara, Viwanda, Uvuvi, Michezo, Sanaa na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Alichokosea Kikwete ni kuchanganya mambo ya kutaka wahitimu wengi wa Uhandisi na hata kutoa uwiano dhaifu wa wahandisi na kuachana na siasa kukimbilia Teknolojia na Sayansi.
Kauli ya kutaka nchi iendeshwe Kisayansi na Kiteknolojia ingetolewa katika mandhari tofauti na hii aliyokuwapo. Ni kweli inabidi tuachane na kuendesha nchi kwa kutumia siasa pekee na tuoanishe itikadi na sera ambazo ni siasa na matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuendesha nchi, ikiwa ni pamoja na Utawala, Uongozi, Uzalishaji mali na Huduma za jamii.
Laiti kama angeanzia kujitathmini kwa kuangalia anachofanya yeye kama Kiongozi na Mtawala kwa darubini ya Sayansi na Teknolojia, angegundua kuwa Tanzania inahitaji Micro Manager na si Macro Manager!
Tanzania bado inatumia zana na hata mawazo na fikra za kiutendaji za kijima.
Leo hii wenzetu wanakaribia kuachana na Nano Technology na kwenda kwenye technology mpya,sisi bado hata Computer inatushinda.
TUnashindwa kuwa na central database ya Serikali kuweka Nyaraka au kumbukumbu. Hatuna hata vitambulisho vinavyoaminika, hatuna anuani au makazi ambayo yanaweza aminika na benki hata kupata mkopo, kila kitu ni kutafuta faili au yale ma-black book, kupata kumbukumbu. Tunatumia muda mwingi kufanya vitu kutumia analog methods huku tungeweza kuwa kwenye digital age.
Mfano, unakwenda Uhamiaji au Leseni ya Gari kubadilisha picha au kupata leseni na paspoti mpya, kama huna nakala ya pasipoti na leseni yako, ni vigumu kwa wanaotoa huduma kukusaidia. Si hivyo tu, kila kumbukumbu iko kwenye karatasi, moto ukikamata ni kilio na kusaga meno.
Sasa tafakari muda utakotumika kwenda litafuta hili faili la Rev. Kishoka pale Uhamiaji. Kama wangekuwa na Database, na kutumia Computer ningeweza wasilisha ombi la kupatiwa pasi mpya kwa kutumia internet, au kutuma fax fomu zangu na siku ya kwenda ichukua, nitokee nakitambulisho changu na fedha kulipia kama sijalipia nimalizane nao. Zaidi kama tungekuwa na mfumo wa anuanizakuaminika na hata posta kufanya kazi vizuri, wala nisingepoteza muda kwenda uhamiaji kupigishwa gumba na picha upya au kutoa chai nipate pasipoti yangu wiki nne baada ya kuwasilisha maombi. Uhamiaji wangenitumia kwa posta Pasipoti yangu na mchezo ungekweisha.
Mfano mwingine, Wastaafu wengi walioko mikoani, hawawezi kupata penshieni zao bila kufunga safari kwenda Dar kupata mafao yao. Kama NSSF, PPF au wengine wangekuwa na mfumo mzuri wa computer na Mstaafu huyu ana kitambulisho chaTaifa,angebakia kwao Malampaka pesa aendezichukua benki au atumiwe cheki yake kila mwezi!
Tuje kwenye uzalishaji mali kama kilimo, uvuvi, ufugaji na hata uchimbaji madini. Ukiondoa wazawa wachache wenye uwezo, asilimia kubwa ya Watanzainia wanatumia zana za kijima kuzalisha mali katika nyanja hizi. Ndio tunaelewa ni umasikini, lakini ni mpaka lini tuendelee kusubiri kutumia Trekta au mbegu bora kuweza kuzalisha kwakutumia Sayansi na Teknolojia hivyo tuweze jitosheleza?
Tanzania imezungukwa na maziwa makubwa matatu na mito mingi ndani ya nchi, lakini tunakabiliwa na njaa kila baada ya miaka miwili kisa hakuna mvua, je umwagiliaji uko wapi?
Hata kama leo tutasema kuwa mkulima wa Tanzania anaweza kupata mavuno mengi, je ni mbegu bora, kilimo cha kisasa au kitu gani kinatumika kumzindua Mtanzania?
Je tunashindwa nini kutumia Sayansi na Teknolojia vizuri kuhakikisha kuwa tuna umeme na nishati za kutosha? Mabwawa ya Umeme yanajaa tope, tunashindwa nini kuyasafisha na hata kutoa kinga yasipate tope? kwa nini hakuna mkazo kutoka taasisi za Sayansi au mamlaka husika kulisukuma Taifa kwenda kwenye matumizi ya Umeme wa Upepo na Jua?
Sasa pamoja na kuwa kauli ya Kikwete inaelekea kumsuta nikitumia vigezo nilivyoweka hapo juu, lakini si dhani ni haki tukimbebesha mzigo huu yeye pekee bila sisi wote kuubeba mzigo huo.
Nakubaliana naye kuwa tatizo la Tanzania kuendelea ni siasa nyingi. Wanasema Wamarekani "too many chiefs and not enough Indians"! Ndilo tatizo la Tanzania, kila kitu ni siasa nyingi ambazu huua ufanisi na tija kwa kuwa kila mtu mtazamo wake ni wa kisiasa na si kisayansi au teknolojia.
Mitazamo ya kisiasa na hata kufanya mambo kwa kuegemea siasa kumetufanya tupoteze muda mwingi katika safari yetu ya kusukuma gurudumu la maendeleo na ujenzi wa Taifa.
Mfano mwingine mzuri wa porojo za siasa ni ile website ya Ikulu. badala ya kufanya mambo kwa kutumia Sayansi ambayo anaihubiri, wasaidizi wake wamekaa wakivutana kisiasa na kubishana ni nini kitokee, ni rangi gani itumike!
Nakubali kuna mengi ambayo yangefanikiwa kama tungekuwa na Uongozi mahiri na makini na hilo Kikwete ni wa kulaumiwa, lakini tusipuuzie changamoto hii.
Tutumie fursa hii kuleta maendeleo kwa kumtaka Kikwete afanye kweli kama Kennedy alivyofanya kuwa kusema tunahitaji kujifunga mikanda na kuingia gharama kama tunataka kwenda mwezini (soma hiyo link hapo juu).
Tunachotakiwa kumuasa na kumuomba Kikwete ni kuwa inabidi awe Micro Manager na awe mkali sana na si mkali kidogo kama Mwinyi alivyoombwa na Nyerere!