Maamuzi ya kuchagua viongozi ikiwamo mabalozi Tanzania yamekuwa ya ajabu ajabu kuanzia enzi za Nyerere. Nadhani haya ndiyo madhara makubwa sana yatokanayo na siasa za chama kimoja na demokrasia iliyo hasiwa.
Viongozi walipotokea kutofautiana kimawazo, au kugombana kwa sababu moja ama nyingine, ili kupooza mambo Mkuu alikuwa anawapeleka nje kuwa mabalozi ili wapishe wenzao na wale anaoelewana nao zaidi wafanye kazi kwa amani. Uteuzi mwingi wa mabalozi nchini Tanzania ulikuwa na vijisababu visivyo na tija kwa Taifa. Nakumbuka uteuzi wa M.Generali Sarakikya kipindi kile kuwa Balozi Nigeria ulikuwa na sababu kubwa, hata uteuzi wa Mwakawago kwenda UN ulikuwa na nia ya kurekebisha matatizo katika chama. Huu utaratibu wameeendelea kuufuata mpaka leo.
Sasa siasa za namna hii huwa haziendelezi nchi hata kidogo kinyume chake ni kuwa zinabomoa. Watanzania tuna bahati mbaya sana na tuna kazi kubwa mpaka tuje kupata katiba mpya isiyotokana na mabavu ya CCM na ujanja ujanja wake ndipo tutaanza kupiga hatua sahihi kuelekea maendeleo ya kweli kwa ajili ya Taifa zima.