Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Rais Kikwete ateua mabalozi wapya. Marmo, Batilda na wengine ndani!

Wanaenda kumwakilisha jk siyo wananchi. Wananchi waliwatupa kwenye dust bin, Jk kaenda kuwaokota kwenye dampo.

Nani asiyejua kwamba uchaguzi uliopita ulitawaliwa na rushes na hill za kukomoana? Mbona Hillary Clinton alishindwa kura za maoni akateuliwa kuwa waziri? Kaka kazi ya siasa kuna kubadilishwa majukumu na kushindwa uchaguzi silo kigezo cha ubovu wa Kiongozi. Kwani hao walioshinda wana ubora upi?
 
Rais amefanya uteuzi wa Mabolozi wapya miongoni mwao ni:
1)Dr.Deodoros Kamala- UBELGIJI
2) Dr Batilda burian-Kenya
3) Filip Marmo-Uchina
4)Ali Saleh-Oman
Na wengineo
Source TBC Habari

Mbona Membe aliwahi kusema wakati anafunga semina ya maofisa ubalozi iliyofanyika Dar miezi miwili iliyopita kuwa mabalozi watakao teuliwa kuanzia sasa watakuwa vijana! Je na Philip Malmo naye ni kijana? Kitu kingine hao watatu wa mwanzo kwenye hii list walikataliwa na wananchi wa Tanzania inakuwaje wawe wawakilishi wa nchi yetu nje? Haya ndio mambo ya hovyo kabisa ya Jakaya Mrisho Kikwete
 
Mods haya si matusi kwa mkuu wa nchi?

Ni kweli JK ndio AMIRI JESHI MKUU hatakiwi ku~tusiwa haaaata kidoooogo! Ashindwe na ajaribu kulegea... ZIDUMU FIKRA ZA RAIS WETU... Najua kina FF,RITZ1 na wengineo mtaitikia ZIDUUUUUUUUUUMUUUUUUUU...
 
"Jah Hero" hayupo kstiks hiyo List??
 
Watanzania kweli kazi yetu ni kukosoa tu kila jambo, sasa mnataka rais hawachague kina nani ndiyo mfurahi?
 
Batilda kapelekwa Kenya ili iwe rahisi kwake kuhudhuria kesi ya uchaguzi maana inategemewa kwisha 2014.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Mabalozi:-
(i) Mhe. Phillip MARMO, ameteuliwa kuwa Balozi nchini CHINA. Kabla ya hapo Mhe. Marmo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
(ii) Dkt. Deodorus B. KAMALA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini BELGIUM. Kabla ya hapo Mhe. Kamala alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
(iii) Dkt. Batilda S. BURIAN, ameteuliwa kuwa Balozi nchini KENYA. Kabla ya hapo Mhe. Dkt. Burian alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
(iv) Dkt. Ladislaus C. KOMBA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini UGANDA. Kabla ya hapo Dkt. Komba alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
(v) Bibi Shamim NYANDUGA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MSUMBIJI. Kabla ya hapo Bibi Nyanduga alikuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
(vi) Bibi Grace J.E. MUJUMA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini ZAMBIA. Kabla ya hapo Bibi Mujuma alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Ushirikiano wa Kikanda (Regional Co-operation), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
(vii) Bwana Mohamed H. HAMZA, ameteuliwa kuwa Balozi nchini MISRI. Kabla ya hapo Bwana Hamza alikuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, ZANZIBAR, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
(viii) Ndugu Ali A. SALEH, ameteuliwa kuwa Balozi nchini OMAN. Kabla ya hapo Bwana Saleh alikuwa Balozi Mdogo (Consul General) nchini Dubai.
2. Uteuzi huu unaanzia tarehe 12 Oktoba, 2011. Wataapishwa tarehe 19 Desemba, 2011 saa 03.00 Asubuhi.
 
Nani asiyejua kwamba uchaguzi uliopita ulitawaliwa na rushes na hill za kukomoana? Mbona Hillary Clinton alishindwa kura za maoni akateuliwa kuwa waziri? Kaka kazi ya siasa kuna kubadilishwa majukumu na kushindwa uchaguzi silo kigezo cha ubovu wa Kiongozi. Kwani hao walioshinda wana ubora upi?

Nakubaliana na wewe.
 
Nani asiyejua kwamba uchaguzi uliopita ulitawaliwa na rushes na hill za kukomoana? Mbona Hillary Clinton alishindwa kura za maoni akateuliwa kuwa waziri? Kaka kazi ya siasa kuna kubadilishwa majukumu na kushindwa uchaguzi silo kigezo cha ubovu wa Kiongozi. Kwani hao walioshinda wana ubora upi?

Ingelikuwa ushindani wa ndani ya chama kimoja kinachomtafuta nominee for general election huo ubongo wako ningesema uko sahihi kaka, but for Batilda and others is another issue! Wananchi waliwahukumu kwa aibu huwezi kumlinganisha na Hillary aliyepigwa chini kwenye presidential nomination, not in general election! Pia jiulize kwanini Batilda hakupangiwa mbali? Kapelekwa Kenya ili awe karibu na Muungwana!
 
Sijui katiba inasemaje, lakini ni lazima mabalozi wa kuwakilisha watanzania watoke CCM tu, kuna cream nzuri tu upande mwingine!
 
Duu haya fadhila hizo kama kawa ingawa kidogo amezingatia taaluma!!pia nawashauri....awarudishe wazee wote huko wamejibinafsishia balozi kama zao...kina Mtiro warudi wajiandae kustaafu!
 
hongera mh, rais fanya kazi yako katiba inakuruhusu na wanaobeza wanyamazie kama huwaoni, ipo cku watakukumbuka maana rais ajaye hatatoa ruhusa hy tena.
 
Back
Top Bottom