Ni mtazamo wangu na wewe unaruhusiwa kuwa na mtazamo wako. Anyway tuje katika hoja zako, hoja ya kwanza ulisema kuwa freedom of speech is a natural right yangu mie na wewe sasa nikuulize swali mlalahoi ni rais gani aliyekuwa anaruhusu mie na wewe tukawa tunaisulubu na kuisimanga serikali kwa uhuru. Mkapa alikuwa akitumia majasusi, Mwinyi makomredi, Nyerere system sasa je hiyo freedom ilikuwapo mbona unazungumzia vitu ambavyo ni non-sense kabisa. Ni nani hapa jamvini aseme alidiriki kuitamkia wazi serikali imeoza wakati wa mwinyi, nyerere na mkapa let alone kumkosoa rais kama hujaenda kujisaidia ndoo keko!!!!.
Kwani Mwanahalisi lilifungiwa katika utawala upi?Kulikoni je?Na Kubenea alimwagiwa tindikali wakati wa utawala wa Nyerere?Na hao majasusi wanaokesha JF kila kukicha ni waajiriwa wa Kamuzu Banda?Ni uhayawani kufikiria kwamba JK ametupa uhuru wa kuongea wakati haki hiyo iko wazi na bayana kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Yani haki yako ya Katiba unaihusisha na matakwa ya mtu?Kweli safari ya kumkomboa Mtanzania bado ni ndefu sana kwa mawazo kama haya!
Tuje katika swala muswada bunge limepitisha muswada wa utawala bora ambao unatenganisha biashara na utawala. Lakini muswada huo ni serikali ndio iliyoundaaa na kurasijisha bungeni sasa nikuulize kuna miswada mingapi serikali imeikalia kujifanya bado inaishughulikia kwanini wauruhusu kama sio mtazamo wa rais kupendelea uongozi utenganishwe na shughuli za mtu binafsi. To me I think that is irrelevant unaposema hauna faida. Mkapa aliruhusu ndio matokeo yake Kiwira Coal mine, Meremeta Gold Mine etc. Sasa huoni kama hili jambo lina manufaa kwa jamii.
Na hatma ya Meremeta ni ipi hadi leo?Pinda (mteuliwa wa Kikwete) alisemaje Bungeni alipoulizwa kuhusu Meremeta?
Halafu napokuona wa ajabu ni namna unavyoweza kuonyesha bayana kuwa JK ana uwezo wa kufanya mazuri lakini unajikanganya kwa kushindwa kutueleza nini kinamkwaza kufanya mazuri kama kuwachukulia hatua mafisadi wa Kagoda,Richmond,Kiwira,IPTL,rada,nk.
Tumia busara usiendeshwe na simulizi kwani simulizi zimekuwepo tangia enzi hizo.Kwanza,nimeshakujibu kuwa huo muswada wa kutenganisha biashara na siasa ni kiini macho kwa vile CCM yenyewe inaendeshwa na wafanyabiashara wa fedha chafu.Unatarajia nini kama mwenyekiti wa kamati yake ya maadili ni jambazi wa rada Chenge?
Kwa upande wa kisheria,uamuzi huo unaweza kupingwa mahakamani kuwa unawanyima wafanyabiashara waadilifu fursa ya kushiriki katika demokrasia.Kwa taarifa yako,tatizo sio wafanyabishara kujihusisha na siasa hususan katika mfumo wa uchumi wa soko.Tatizo ni wafanyabisahara wa aina ya Rostam Aziz,Lowassa,Karamagi na mafisadi kama hao.Kwani kama Rostam anaweza kuandikisha utitiri wa makampuni kwa kutumia majina mbalimbali,atashindwaje kusema anaacha biashara na kubaki mwanasiasa asilimia 100% huku makampuni anayomiliki kwa majina mbalimbali yakiendeleza ufisadi?
Pia uanapswa kuelewa kuwa tatizo sio sera,miswada au sheria bali usimamizi na utekelezaji wake.Kwani wakati tunaingizwa mkenge wa Richmond kulikuwa hakuna sheria inayosimamia manunuzi?Je wakati tunaingia mkenge wa IPTL hakukuwa na sheria za kuhakikisha kuwa mkataba huo haugeuki kuwa loba ya mbao?
Ni kipi kinakupa matumaini kuwa sheria ya kutenganisha siasa na biashara itatekelezeka ilhali hseria nyingine zinazoweza kuzuia ufisadi zimeendelea kubaki vitabuni tu?
Na muulize huyo rafiki yako JK kwanini yeye mwenyewe hafuati sheria kwa kututangazia mali zake ili tujue kama naye si mfanyabisahara?Kwanini asimuige Pinda?
Kuhusu CCM mie siwafagilii na nakubaliana na mtazamo wako kwani hata mie sikubaliani nao kabisa but ngoja nikuulize ndani ya CCM nani anafaa kuwa kiongozi wa nchi sasa hivi tukimtoa JK nani Lowassa?, Abdallah Kigoda, hakuna hata mmoja msafi humo ndani hadi Sitta mwenyewe anayejiita kiongozi wa kupambana na ufisadi tukitaka tutamfunulia madudu yake aliyoyafanya wakati akiwa Tanzania Investment Centre na pia wakati akiwa NDC sasa kwakweli sijaona kiongozi msafi CCM hata kidogo.
Kwahiyo kwa vile ndani ya CCM hakuna aliye bora basi tuendelee na Kikwete?Hivi unafahamu kuwa membership ya CCM ni takriban asilimia 10 tu ya population ya Tanzania?Yani unachosema ni kwamba laiti ungekuwa na mke malaya ungeendelea nae hivyohivyo kwa vile tu kwa mtizamo wako huko nje hakuna wanawake walio bora zaidi?Haya ndio yanayowaua watu kwa ukimwi.
Kumbuka kuwa uongozi wa TAIFA LETU sio divine right ya CCM pekee.Kumsifia Kikwete kuwa ni bora kwa vile tu wenzake huko CCM ni wachafu,au hakuna aliye bora zaidi yake,ni ufinyu wa mawazo.
I would say kuna watu kama Dr Slaa ambao at least wametuonyesha nini maana ya kiongozi kuwa na uchungu na nchi.
Kuhusu infrastructure economics sidhani hata katika nchi zilizoendelea projects zote zinaenda kwa wakati mmoja. Bali zinaenda kwa awamu kutegemeana na umuhimu wake. Unadhani soko la wakulima wa tanzania liko wapi mzee? Wakulima wako wakijengewa barabara halafu jijini dar, arusha barabara zikawa mbovu haya mazao yatafika???? Zungumza jambo ukiwa na akili timamu na sio umelewa kuendelezwa kwa miji ya kibiashara na muhimu kwani ndio soko kuu la mazao na hasa kwa tanzania ukichukulia wakulima wetu kuuza mazao nje ni ndoto. Usidhani kutawala nchi ni kama kuongoza kajumba kako!!!!
Na kwa akili yako iliyo timamu ukishakuwa na barabara nzuri hapo Dar wakati wakulima huko mahenge wanasumbuana na kivuko feki unatarajia hayo mazao yanafikaje bandarini Dar?Eti infrastructural economics!Yaani barabara za lami mijini zimekusahaulisha kabisa adha ya watanzania wenzako wanayipata huko reli ya kati na Tazara?Vipi kuhusu ATC?
Ni ulevi wa kifikra kuangalia upande mmoja wa "maendeleo" na kupuuza upande mwingine.Tegemeo la uchumi wa Tanzania ni katika kilimo,na kama unafuatilia mijadala ya bunge vizuri utakumbuka kwanini bajeti ya WIzara ya Miundombinu iliwekewa ngumu katika kikao cha bajeti kilichopita.Fuatilia hilo kisha ufanye review ya hoja yako dhaifu.
Of course,kutawala nchi sio sawa na kuongoza nyumba ndio maana hatutaki kiongozi dhaifu ang'anganie kuongoza wakati ameshindwa hata kumudu nidhamu ya baraza lake "dogo" la mawaziri waziofika 60.Kama hawezi kuwamudu hao "wachache" alowateua ataweza kumudu kuwatumikia watanzania zaidi ya milioni 40?
Kikwete hajashindwa miaka mitano bali ameiingia na kukuta madudu yaliyofanywa na mwenzie aliyemtangulia ambayo yakamuharibia muelekeo wa utekelezaji wa sera zake. Likewise kaa mkijua kuwa hali ya uchumi wa kidunia pia imeterereka kutokana na kuanguka kwa sekta ya fedha. Zote hizi ukizichanganya unakuta ni bahati mbaya uongozi wake umekutana na masaibu hayo na sio majaribio kama unavyotaka kuileta kwani hali hiyo tuliipata wakati wa 1979-1982 tukilishwa unga wa njano na sukari guru.
Unavyoongea kuwa ameingia na kukuta madudu inasomeka kana kwamba ALILAZIMISHWA KUINGIA MADARAKANI.Dont tell me kuwa hakujua madudu yalokuwepo before hajaingia madarakani because HE WAS PART YA MADUDU ALIYOYAKUTA ALIPOINGIA MADARAKANI.Kwa kumbukumbu zako,JK alianza kushika madaraka ya kitaifa lini?Mwaka 2006?Alikuwa anafahamu fika uzito wa jukumu analolipokea na akatuahidi kutupatia ufumbuzi.
Halafu baadhi ya kauli zako ni kama za KUJIPENDEKEZA.Mbona sijamsikia JK mwenyewe akisema kuwa CHANZO CHA MATATIZO YALIYOPO NI WATANGULIZI WAKE?