Rais Kikwete: Nabii asiyekubalika nyumbani kwake?

Amemweka Babu Seya na wanae nyuma ya pazia kwa miaka yao yote duniani so kawafanya wafunge ndoa na Gereza

Kuna watu wengine JF wanakuwaga ni pointless kabisa hebu tupe link ya Babu seya na JK. Babu seya amekuwa akiharibu watoto wa watu wewe unaliona hilo sawa??? na JK yuko kwake kule Ferry alitokaje kuja kuhukumu kesi ya babu seya. Jamani tuwe home of great thinkers and not otherwise.
 

Inaonekana wewe ni mgeni kwenye mambo haya ya forums. Wakati wa mkapa kulikuwa na kitu inaitwa Bsctimes (kama sikosei) ambako watu walikuwa wakitoa nondo kama hawana akili nzuri. Walimkoma nyani giladi na wala hawakuwahi kwenda keko wala kokote kule.


Swala la kupitisha mswada ni tofauti na utendaji. Utekelezaji wa hili swala bado uko mbali sana na hali halisi.


Yaani kwa vile hakuna mwingine unayemwona wewe kuwa anafaa basi Kikwete aendelee kuwa kiongozi. Wana ccm wote Tanzania hakuna yeyote mwingine zaidi ya Kikwete anayefaaa?


So far alichofanya Kikwete ni kipi?


Kikwete ana madudu yake mengi tu (soma post ya Kibanga hapo juu) na wala sio kwamba kakuta madudu yaliyofanywa na wengine


Hizo sifa zote ulizotaja hapo, Kikwete hana. What about makamo wa raisi Sheini?
 

Mazuri yenyewe bado hayajatajwa ... yanasubiriwa
 

Kaka mie ndio nilikuwa mgeni wa Jamiiforum but kama umesahau wakati mkapa jamiiforum (ambayo wakati huo ikiitwa jamboforum) iliiandamwa ikawa shut down ndio transparency hiyo!!!!

Mie nasema ndani ya CCM hakuna mwenye sifa nilizozitaja hapo juu. Shein ni simba aliyekaa kimya kama angelikuwa mwadilifu angelijuuzulu wakati wa mkapa ambapo madudu yalikuwa yakiendelea. Kaja wakati wa Kikwete salamu ndio hizo hizo je ndio kiongozi mwadilifu huyo au mwoga!!!! asiharibu kitumbua chake. Hakuna mwenyesifa mkubwa kwangu mie kama independent voter
 
Kaka mie ndio nilikuwa mgeni wa Jamiiforum but kama umesahau wakati mkapa jamiiforum (ambayo wakati huo ikiitwa jamboforum) iliiandamwa ikawa shut down ndio transparency hiyo!!!!

Unazidi kuchemsha bado ... jamii forums iliandamwa na kufungwa (shut down) wakati wa Kikwete na sio wakati wa Mkapa.


Kwa hiyo uko wazi kusema kuwa hautapigia kura ccm kwa vile hakuna msafi na mwenye sifa ulizozitaja hapo juu?
 
Unazidi kuchemsha bado ... jamii forums iliandamwa na kufungwa (shut down) wakati wa Kikwete na sio wakati wa Mkapa.



Kwa hiyo uko wazi kusema kuwa hautapigia kura ccm kwa vile hakuna msafi na mwenye sifa ulizozitaja hapo juu?

Hebu tuambie jambo forum ilienda wapi???? na nadhani nilishasema tangu thread ya mwanzo kuwa hakuna msafi CCM labda apewe tu huyo JK which mie sitapiga kura kwake bora iwe kura mfu pengine atajirekebisha
 
Hebu tuambie jambo forum ilienda wapi????

Jamboforums ilibadilishwa jina kuwa jamii forums sometimes kati ya 2007 na 2008 (sina hakika zaidi katika hili) baada ya kutokea mgongano kati ya waanzilishi wa forums kuhusu umiliki wa jina jamboforums.

Mgogoro unaouongelea kati ya jamboforums (jamiiforums) na serikali, umetokea wakati wa serikali ya Kikwete na sio Mkapa. Mimi nimeijua hii forum mwaka 2006. Sina hakika kama ilikuwepo mwaka 2005 au kabla ya hapo. Kina Julius (au wale members tuliokuwa nao toka enzi za Bsctimes) wanaweza kudhibitisha hili.

nadhani nilishasema tangu thread ya mwanzo kuwa hakuna msafi CCM labda apewe tu huyo JK which mie sitapiga kura kwake bora iwe kura mfu pengine atajirekebisha

Kama Kikwete sio msafi kama walivyo wengine uliowataja hapo juu, kwanini waona kuwa bora Kikwete na sio wao?

Ufisadi wa Kikwete una tofauti gani na ufisadi wa Lowasa au Sitta?
 

Kikwete naweza kukuhakishia si fisadi hao wengine ni mafisadi haswa haswa. Ila tatizo la kikwete ni mtu ambaye si mfatiliaji wa jambo na anapenda sana sifa kitu kinachomponza. Hawa wengine wanajifanya wafatiliaji kumbe wanafatilia kwa maslahi yao binafsi nadhani tofauti umeziona hapo ndio maana nasema afadhali Kikwete
 

Mhh,

Yaani unaweza kunihakikishia kabisa kuwa Kikwete si fisadi. Kwanza unaanza kwa kusema kuwa ccm wote mafisadi na kisha unabadilika njiani na kusema kuwa Kikwete ni msafi na sio fisadi.

Hebu jibu haya yaliyoandikwa na Kibanga ampiga mkoloni


 
Steve dii nimekuona hapo juu, tafadhali sana nisaidie kumkumbusha ndugu mdondoaji kuwa waendeshaji wa jamiiforums (jamboforums) walitupwa ndani wakati wa uongozi wa Kikwete na sio Mkapa
 
Kwani Mwanahalisi lilifungiwa katika utawala upi?Kulikoni je?Na Kubenea alimwagiwa tindikali wakati wa utawala wa Nyerere?Na hao majasusi wanaokesha JF kila kukicha ni waajiriwa wa Kamuzu Banda?Ni uhayawani kufikiria kwamba JK ametupa uhuru wa kuongea wakati haki hiyo iko wazi na bayana kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano.Yani haki yako ya Katiba unaihusisha na matakwa ya mtu?Kweli safari ya kumkomboa Mtanzania bado ni ndefu sana kwa mawazo kama haya!
Na hatma ya Meremeta ni ipi hadi leo?Pinda (mteuliwa wa Kikwete) alisemaje Bungeni alipoulizwa kuhusu Meremeta?

Halafu napokuona wa ajabu ni namna unavyoweza kuonyesha bayana kuwa JK ana uwezo wa kufanya mazuri lakini unajikanganya kwa kushindwa kutueleza nini kinamkwaza kufanya mazuri kama kuwachukulia hatua mafisadi wa Kagoda,Richmond,Kiwira,IPTL,rada,nk.

Tumia busara usiendeshwe na simulizi kwani simulizi zimekuwepo tangia enzi hizo.Kwanza,nimeshakujibu kuwa huo muswada wa kutenganisha biashara na siasa ni kiini macho kwa vile CCM yenyewe inaendeshwa na wafanyabiashara wa fedha chafu.Unatarajia nini kama mwenyekiti wa kamati yake ya maadili ni jambazi wa rada Chenge?

Kwa upande wa kisheria,uamuzi huo unaweza kupingwa mahakamani kuwa unawanyima wafanyabiashara waadilifu fursa ya kushiriki katika demokrasia.Kwa taarifa yako,tatizo sio wafanyabishara kujihusisha na siasa hususan katika mfumo wa uchumi wa soko.Tatizo ni wafanyabisahara wa aina ya Rostam Aziz,Lowassa,Karamagi na mafisadi kama hao.Kwani kama Rostam anaweza kuandikisha utitiri wa makampuni kwa kutumia majina mbalimbali,atashindwaje kusema anaacha biashara na kubaki mwanasiasa asilimia 100% huku makampuni anayomiliki kwa majina mbalimbali yakiendeleza ufisadi?

Pia uanapswa kuelewa kuwa tatizo sio sera,miswada au sheria bali usimamizi na utekelezaji wake.Kwani wakati tunaingizwa mkenge wa Richmond kulikuwa hakuna sheria inayosimamia manunuzi?Je wakati tunaingia mkenge wa IPTL hakukuwa na sheria za kuhakikisha kuwa mkataba huo haugeuki kuwa loba ya mbao?

Ni kipi kinakupa matumaini kuwa sheria ya kutenganisha siasa na biashara itatekelezeka ilhali hseria nyingine zinazoweza kuzuia ufisadi zimeendelea kubaki vitabuni tu?

Na muulize huyo rafiki yako JK kwanini yeye mwenyewe hafuati sheria kwa kututangazia mali zake ili tujue kama naye si mfanyabisahara?Kwanini asimuige Pinda?


Kwahiyo kwa vile ndani ya CCM hakuna aliye bora basi tuendelee na Kikwete?Hivi unafahamu kuwa membership ya CCM ni takriban asilimia 10 tu ya population ya Tanzania?Yani unachosema ni kwamba laiti ungekuwa na mke malaya ungeendelea nae hivyohivyo kwa vile tu kwa mtizamo wako huko nje hakuna wanawake walio bora zaidi?Haya ndio yanayowaua watu kwa ukimwi.

Kumbuka kuwa uongozi wa TAIFA LETU sio divine right ya CCM pekee.Kumsifia Kikwete kuwa ni bora kwa vile tu wenzake huko CCM ni wachafu,au hakuna aliye bora zaidi yake,ni ufinyu wa mawazo.

I would say kuna watu kama Dr Slaa ambao at least wametuonyesha nini maana ya kiongozi kuwa na uchungu na nchi.


Na kwa akili yako iliyo timamu ukishakuwa na barabara nzuri hapo Dar wakati wakulima huko mahenge wanasumbuana na kivuko feki unatarajia hayo mazao yanafikaje bandarini Dar?Eti infrastructural economics!Yaani barabara za lami mijini zimekusahaulisha kabisa adha ya watanzania wenzako wanayipata huko reli ya kati na Tazara?Vipi kuhusu ATC?

Ni ulevi wa kifikra kuangalia upande mmoja wa "maendeleo" na kupuuza upande mwingine.Tegemeo la uchumi wa Tanzania ni katika kilimo,na kama unafuatilia mijadala ya bunge vizuri utakumbuka kwanini bajeti ya WIzara ya Miundombinu iliwekewa ngumu katika kikao cha bajeti kilichopita.Fuatilia hilo kisha ufanye review ya hoja yako dhaifu.

Of course,kutawala nchi sio sawa na kuongoza nyumba ndio maana hatutaki kiongozi dhaifu ang'anganie kuongoza wakati ameshindwa hata kumudu nidhamu ya baraza lake "dogo" la mawaziri waziofika 60.Kama hawezi kuwamudu hao "wachache" alowateua ataweza kumudu kuwatumikia watanzania zaidi ya milioni 40?


Unavyoongea kuwa ameingia na kukuta madudu inasomeka kana kwamba ALILAZIMISHWA KUINGIA MADARAKANI.Dont tell me kuwa hakujua madudu yalokuwepo before hajaingia madarakani because HE WAS PART YA MADUDU ALIYOYAKUTA ALIPOINGIA MADARAKANI.Kwa kumbukumbu zako,JK alianza kushika madaraka ya kitaifa lini?Mwaka 2006?Alikuwa anafahamu fika uzito wa jukumu analolipokea na akatuahidi kutupatia ufumbuzi.

Halafu baadhi ya kauli zako ni kama za KUJIPENDEKEZA.Mbona sijamsikia JK mwenyewe akisema kuwa CHANZO CHA MATATIZO YALIYOPO NI WATANGULIZI WAKE?
 
Mazuri yenyewe bado hayajatajwa ... yanasubiriwa

Hana Mazuri kama yapo waseme na si kusema tu waje na ushahidi!

Mwenye mada hii alikuwa anazungumzia kuwa Raisi anakubalika nje kuliko ndani, na yote inatokana na kusifiwa na wazungu.

Hivi tumesahau ya Mkapa walivyokuwa wana msifia? Kikowapi sasa hivi aibuuu anatamani ata kuhama nchi!

Mfano waingereza wealikuwa wanamsifia kumbe watu wana mradi wao wa Radar wanataka kutuhumiza wamechukua hela ambazo zilibidi ziende kwenye elimu ya msingi wao wakaenda kununua Radar (HakiElimu waliongea sana haya mambo kuwa 10,000 kwa kila mwanafunzi wa msingi azijafika kumbe wajanja wameenda kununulia Radar)
 

Kaka sio uvivu wa kufuatilia ni magusudi jamaa anapewa 10% unafikiri Lowasa alikuwa anakula peke yake? au hujuhi habari ya Chenge, Idriss, na mwingine wanasema awamtaji(SFO) walivyogawana za rada?

Hivi kweli Balali alikula peke yake bila Mkapa?

sasa kaa ukijua sio uzembe ni makusudi kwa sababu jioni hesabu inaingia au jamaa wanamdai za uchaguzi kwahiyo anawachunia warudishe chao( Rostam & Lowasa)
 
Commoro wapi best, kumkimbiza mgambo ndo unamsifia? Kwanza wale jamaa walikuwa kama sungusungu wa Mh. Mrema! Mwabie aende Somalia au Afghanistan akapambane na wanaume wa kazi!
 
Amewatunuku vyeo ndugu na marafiki zake hata pale ambapo hawakuwa na uwezo na matokeo yake wamevurunda na kumuaibisha ; mifano michache ni pale Board of External Trade na ATCL kwa wale wanaotaka kuthibibitishiwa!!
 
Amewatunuku vyeo ndugu na marafiki zake hata pale ambapo hawakuwa na uwezo na matokeo yake wamevurunda na kumuaibisha ; mifano michache ni pale Board of External Trade na ATCL kwa wale wanaotaka kuthibibitishiwa!!

Kaka aihitaji ushahidi kwani Shukuru Kawambwa amjuhi? mtu anahama wizara kama watu wanavyopanda vidato leo form one, mwaka form two,....
 
Rafiki yangu, hayo niliyowekea red yana ukweli. Unajua ni lini mpanga wa MMEM na MMES zilianza? Yeye amefanya lipi zaidi ya kutimiza tu aliyofanya mwenzake? Kwenye hili la shule naliogopa, kwa sababu mwenzake Mkapa aliongeza shule nyingi za msingi pasipo kuathiri ubora. Yeye ameachiwa kusimamia tu hizi shule za secondary ambazo mwenzake alishakuwa na mpango kabambe ndo katutokea na ziro zaidi ya 60000. Aibu kuwapotezea muda watoto zaidi ya 60000 kwa zaidi ya miaka minne. Umeongelea kuhusu barabara, maji and the like. barabara zipi, maji yapi, hizo project zote sializianzisha Mkapa? Hili suala la kusimamia hata wewe tu unaweza kusimamia. Tunachotaka ni innovation and creativity ambazo zimeibuka wakati wake ambazo yumkini zinaviashiria vizuri kwa uchumi na ustawi wa jumla wa nchi yetu.
Napenda nimpongeze sana kuhusu chuo kikuu cha Dodoma. Katika hicho sina upinzani naye, kafanya kazi nzuri yenye maslahi makubwa kwa taifa.
 

I like this dialogue. Mlalahoi, nadhani sasa unakea kuwa mlalahai. keep it up
 
Mlalahoi nimekupa thanks watu wanakuja na cheap politics eti JK ameleta freedom of speech eti utawala bora sijui upi wa kutowapeleka wezi wa EPA mahakamani utawala bora wa kuingia mikataba mibovu utawala bora wakuuza Migodi yetu kwa bei chee wa kuuza fukwe zetu wa kuuza Kigamboni

mmekazania freedom of speech mnasahau nchi ina uzwa jamani acheni utani wakati mwingine tuwe serious wakati wa Mkapa tulikuwa wa tano kwa umasikini duniani sasa ni wa pili toka mwisho bado tunang'ang'ania eti freedom of speech imekua wakati tunalipa mamilion kila siku kwa mikataba fake kama ya IPTL big up Mlalahoi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…