Rais Kikwete unalo suluhisho la Matokeo mabaya ya Kidato cha Nne 2012

Rais Kikwete unalo suluhisho la Matokeo mabaya ya Kidato cha Nne 2012

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
6,710
Reaction score
9,063
Mimi kama mdau wa Elimu na Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii nimesikitishwa sana na matokeo ya mitihani ya Kidato cha nne(F4)mwaka 2012 yaliyotangazwa mwaka huu na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Shukru Kwambawa! Kwamba zaidi ya nusu ya Vijana wetu wamepata daraja 0(DIV-0). Hii ni jumla ya watoto 240,903 sawa na asilimia 60.6(60.6%)! Hii ni aibu na fedheha kwa nchi yetu.

Sina uhakika kama Mhe.Kikwete utapita kwenye ukumbi huu na kuweza kusoma ushauri huu. Hata hivyo nina hakika wapo watu wako wa Ikulu bila shaka watapitia humu na kuona ushauri huu wa Bure na watakuambia.

Mpaka sasa kwa habari za kuaminika kuna vijana 4 tayari wameshaondoa uhai wao kutokana na matokeo haya yenye kukarihisha. Umma wa Watanzania umejaribu kushauri viongozi wa Wizara husika kuwajibika kwa kujiuzulu lakini wamekataa katakata kana kwamba jambo lililotokea haliwahusu! Je, Mheshimiwa Rais unataka Vijana wangapi wa Kitanzania wafe kwa kujinyonga kupinga matokeo haya mabaya ndipo uchukue hatua????

Tumesikia mengi tangu matokeo haya yatangazwe huku viongozi wa Wizara husika wakitupa lawama kwa Wanafunzi,Wazazi na Waalimu. Hakuna hata kiongozi mmoja aliyekiri au kukubali udhaifu uliopo kwenye sekta ya Elimu! Hivi ni nani hajui kwamba shule za kata zilizojengwa kama uyoga nchi nzima hazina waalimu,hazina madarasa ya kutosha,hazina vitabu vya kiada na ziada,hazina maabara ya sayansi,hazina madawati na hazina tuseme kila kitu!!!
Haya mapungufu yako wazi na kila kiongozi wa serikali anajua na Watanzania wote wanajua hivo.

Hivi ni kwanini shule zilizoongoza kwenye matokeo haya mabaya ni za BINAFSI na siyo za KATA au za SERIKALI???Jibu liko wazi. Ndiyo maana hakuna mtoto wa Mbunge,Waziri,DC au RC anayesoma kwenye shule za kata au serikali kwa vile wanajua udhaifu ulioko kwenye shule hizo na hivyo basi viongozi wengi hawaoni uchungu wa watoto kupata 0 au IV!

Sasa mimi kama Mtanzania na mdau wa Elimu napenda kutoa ushauri kwako Mheshimiwa ambao unaweza ukakubali kuufanyia kazi au ukautupa kapuni. Mara nyingi CCM na wewe mwenyewe Mhe. Rais mmekuwa mkijitanabaisha kuwa wewe na Serikali yako ni sikivu! Sasa basi Tumesikia hanbari ya Waziri Mkuu kuunda Tume kuchunguza kisa cha Vijana wetu kushindwa. Watanzania tunajiuliza hii Tume inataka kuchunguza nini ilhali matatizo na sababu za kushindwa watoto zinafahamika???Je, hii si namna ileile ya siku zote ya kujaribu kutuliza upepo na hasira za Watanzania kwa kuunda Tume ambazo aghalabu huwa hazina suluhisho lolote la tatizo husika???

Ushauri wangu ni kama ifuatavyo: Kwa vile matokeo haya yamekuwa ya kiwango cha chini sana kuliko kawaida naomba uagize yafanyika haya yafuatayo:

  1. Kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu uagize Serikali kupitia Baraza la Mitihani-NECTA waitishe kikao cha dharura na wawaite wote waliosahihisha Mitihani wakae na kusahihisha Mitihani yote upya kwa kuzingatia kigezo kinachoitwa STANDARDISATION. Huu ni utaratibu ambao hutumika kwenye Mitihani iwapo kunakuwa na mass failure au mass pass aidha kutokana na ugumu wa Mtihani kwa kutungiwa Mtihani nje ya Syllabus au Mitihani rahisi kuliko kawaida! Kitakachofanyika hapa ni kuangalia swali/maswali ambayo watoto wengi hawakuweza kuyajibu na hivyo NECTA kufanya uwiano wa alama kwa kuwapa watoto ALAMA(Marks) ZA ZIADA kufidia swali au maswali magumu yaliyowashinda.Huu ni utaratibu wa Kimataifa. Kutoka na hivo basi watoto wengi ambao naamini wanauwezo watapata alama na kuweza kuwaongezea grades(daraja) pengine toka 0 kwenda IV, kutoka IV kwenda III, kutoka III kwenda II katika yake makundi ya waliofanya vibaya tu! Nini maana ya Standardisation: Standardisation is a process which takes care of a situation where the distribution of examination marks is not as required. Standardisation takes account of differences in the difficulty of examinations from year to year and ensures that students are not disadvantaged if an examination is harder than usual in a particular year.
  2. Vijana wote waliopata Daraja la 3 mpaka 0(DIV-III mpaka 0) waruhusiwe kurudia mitihani kwa gharama za serikali na mitihani itakayotungwa iwe ni kulingana na kiwango kile ambacho shule zimefundisha. Tumesikia juu ya watoto kufanya mitihani migumu zaidi ya uwezo wao(siyo walichofundishwa).
  3. Kama la 1 na 2 hayawezekani basi Serikali ifute matokeo yote ya Kidato cha 4 mwaka jana na itangaze kurudia Mitihani kwa Wanafunzi wote nchi nzima ambayo ni gharama kubwa zaidi na na itaathiri hata wale ambao walifaulu kwa DIV I na DIV II na itakuwa sawa na kuwaonea. Hii inaweza kutumika tu kama kuna udanganyifu mkubwa katika matokeo ya nchi nzima kama wizi wa Mitihani n.k.
  4. Jambo la nne na la mwisho ni Rais lazima uchukue maamuzi magumu ya kuwawajibisha Viongozi Waandamizi wa Wizara husika kwa kuwapumzisha kazi ambao ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr. Shukuru Kawambwa, Naibu wake Bwana Phillip Mulugo, Katibu wao wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mkurugenza wa NECTA Dr. Ndalichako.

Mhe. Rais kama ambavyo huwa unajinadi kuwa you have a smiling face but very tough on issues nakuomba katika hili uvae uso wa ukali badala ya tabasamu kuwasaidia hawa watoto wa Watanzania maskini. Vinginevo hawa Vijana wetu ambao ni wahanga wataendelea kuumia na hatujui ni wangapi wataoondoa uhai kutokana na madhila haya ya kushindwa Mitihani. Bado tunaweza kunusuru uhai wa Vijana na wakaweza kuendelea na maisha ya shule kwa amani kabisa.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom