kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Naomba kumshauri Rais kwamba kwa mtazamo wangu Ni vigumu kupata wawekezaji walio serious kuja kuwekeza nchini kwa sababu nchi yetu haina mfumo mzuri wa kisheria na kikatiba. Haki Tanzania inapatikana kwa utashi wa Rais na si kwa kuzingatia misingi ya kisheria.
Ni kweli anaweza anaweza kuvutia wawekezaji lakini naomba nimtabirie kwamba wawekezaji wengi watakaokuja na waliopo ni wale wanaowekeza kwa lengo lakuchuma na kuhifadhi walichochuma nje ya mipaka yetu.
Tutegemee wawekezaji ambao mitaji yao mikubwa itawekezwa nchi jirani au kwenye mataifa yao na hapa watapafanya sehemu yakuchuma.
Ili tuwe na wawekezaji wenye confidence na Tanzania lazima tufanye mabadiliko ya sheria ikiwemo katiba. Maamuzi ya haki yaachwe kwenye muhimili na Mahakama na Rais aache kuwa chanzo Cha haki.