Twende mbele turudi nyuma, wengi wetu humu JF tujitokeze tukagombee, Akina Slaa wametimiza wajibu wao, tuwaunge mkono, record ya kura inaonesha kuwa sehemu ambazo chadema iliweka mgombea mwenye nguvu, elimu na uwezo wa kujenga hoja wa udiwani na ubunge Slaa amepata kura za kutosha lakini ameangushwa na wagombea wabovu.
vijana tujitokeze tukafanye kampeni na kuomba kuchaguliwa ili tusaidie harakati, ndiyo maana mimi nimeamua kujitokeza kugombea Isimani Iringa uchaguzi ujao na naanza maandalizi mara moja
Mfano halisi ni Tundu Lisu ambaye ameshinda singida kwa mara ya kwanza upinzani kupata jimbo kule, wakati tundu kashinda singida kusini singida kaskazini mgombea wa sisiem kapata 90% maana yeke ni kwamba wananchi wanaelewa na wanajua kuchambua pumba na mchele
lazima tuanzisha movement sasa ya kupata wagombea sahihi kila jimbo nchi nzima 2015