CHIBA One
JF-Expert Member
- Nov 16, 2018
- 558
- 2,093
Mhe Rais,
Kwanza nikupongeze kwa nia yako ya dhati ya kupambania maslahi ya nchi na watu wake. Umeonyesha utu, ari, na malengo ya dhati ya kuhakikisha mambo yanaenda na kutekelezeka kwa wakati, ninakupongeza.
Mhe Rais,
Katika mikutano yako kadhaa na waandishi wa habari, umekuwa ukionyesha kusikitishwa na kukasirishwa na tabia za wasaidizi wako kukuangusha na wengine kutumia mianya ya nafasi yao kukwapua mali za umma.
Naomba utambue hili limekuwa linatuuma maradufu sisi wananchi hasa tunapoona kuna wasaidizi wako ambao wao hata uongee vipi, watakutana kwa faragha kwa vicheko na kukusengenya as if wewe sio Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hii.
Hawaogopi maneno wala makaripio yako ya busara unayoyatoa, Unapowaambia "Hili kaliangalieni" "Mkajirekebishe" "Mpunguze" "Mjitafakari" hawa watu hawana dalili za kufanyia kazi maneno yako Mhe. Rais.
Kwao matumbo yao ni kipaumbele cha kwanza kuliko hizi mali za umma Mhe. Rais.
Una watu ambao wako radhi kuitafuna hii keki kwa gharama ya tone la mwisho la damu yao. Watu hawa Mama hawarekebishwi kwa "Kulitazama hilo" wanatakiwa watoke damu puani kama kenge ili wajue kweli kumbe unamaanisha.
Mhe. Rais, tunaumia sana kama wananchi kuona mpaka leo hakuna mtu ana kesi Mahakamani kwa ubadhirifu huu wa mali za umma. Wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu kwa nini unaona huna nguvu ya kuwaadhibu haraka?
Kwa nini umekuwa na utaratibu wa kuhamisha watu vitengo badala ya kusimamisha, kufukuza na kufungua mashtaka dhidi yao?
Hao TAKUKURU baada ya kuona yote hayo Mama, wanasubiri nini kufungulia watu Mashtaka ya Uhujumu Uchumi?
Mhe. Rais, tunaomba ututendee haki maana tunaloa jasho na damu kukamuliwa haya mapato yanayoliwa na watu wachache, linda imani tuliyokupa.
Muuza Mchele,
Mbalali.