Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameituhumu nchi ya Urusi kutumia mitandao ya kijamii kuchafua jina la Ufaransa barani Afrika.
Rais Macron alisema maneno hayo tarehe 6 Januari 2025 wakati akiwahutubia wanadiplomasia wa Ufaransa wanaohudumu nje ya nchi hiyo.
Akiongelea swala la kupungua ushawishi wa Ufaransa barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni, Rais Macron alisema propaganda zinazoenezwa na Urusi kuhusu nchi yake kwenye mitandao ya kijamii ndio chanzo cha kupungua kwa ushawishi wa Ufaransa.
Vile vile, alisema wanaharakati wa Afrika wanaofahamika kama Pan Africanists ambao wana ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii,hutumia kete ya kupinga ukoloni kuchafua taswira ya Ufaransa.
Miongoni mwa Pan Africanists hao ni Bibi Nathalie Yamb kutoka nchini Niger na Bwana Kemi Seba kutoka nchini Benin ambao mwaka 2023 Rais Macron aliwaita " waajiriwa wa Putin"
Source: FRANCE 24