Ufaransa ilipataje hayo " maendeleo yake"? Jiulize.Nitakutolea mfano. Kabla ya mapinduzi ya Niger yaliyotokea 2023, Ufaransa ilikuwa inaingiza mabilioni ya Dollar kwa kuuza umeme kwenye nchi nyingine za Ulaya. Lakini Ili kupata huo umeme walikuwa wanabeba Uranium ya bure pale Niger wanapeleka kwao kwenye vinu vya Nyuklia wanatumia kuzalisha umeme wa uhakika kutumia kwenye nchi yao mwingine wanauza. Tangu mapinduzi ya Niger yatokee, hakuna Uranium imepelekwa Ufaransa. Matokeo yake, shirika la Ufaransa la Orano linalohusika na hayo masuala ya umeme limepata hasara balaa hadi serikali ikawapa ruzuku. Bei ya umeme imepanda na kodi inayotozwa kwenye gesi ya kupasha moto majumbani imeongezeka ( Takwimu Na taarifa zipo Google ukizitaka kuthibitisha )Sasa hapo unasema Ufaransa imeendelea au ni mwizi mzoefu ambae hawezi kuishi bila kuiba ? Swala sio maendeleo suala ni bila wizi angeendelea ? Au hukumuona Macron alivyokuwa anaongea kama mwehu baada ya kusikia kibaraka wake katolewa pale Niger. Alikuwa kabisa ugali wa bure unaondoka. Ndio maana hata ECOWAS walikuwa kimbelembele kwenda kuivamia Niger kisa mapinduzi wakati kwenye nchi za Afrika Magharibi mapinduzi ni kitu cha kawaida. ECOWAS walikuwa wanatetea ugali wa Ufaransa pale.
Je unajua hizo nchi za Afrika Magharibi zilizotawaliwa na Ufaransa zinatumia pesa zinazochapishwa Ufaransa na zinalazimishwa kutunza pesa kwenye Benki kuu ya Ufaransa na wakizitaka wanapewa kama mikopo na riba juu? Unajua ni kiasi gani cha pesa Ufaransa wanaingiza kwa kulazimisha hayo makoloni kutumia hiyo sarafu ya CFA Francs? Mifano ni mingi inahitaji uzi mwingine kuelezea Ufaransa anavyoyanyonya makoloni yake ya zamani hadi leo.Ufaransa kaendelea kwa sababu kawaibia halafu wao wameshindwa kumuibia. Upo?