Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Siko huko uliko wewe.Kuwa mtulivu utanielewa.Hata nilipo tunapata tabu sana na Rais ameshapita mara nyingi tu sijawahi ona mbadiliko yoyote yale.
Nakupa tu taarifa fupi..Nipo sehemu umeme kwa week una katika zaidi ya mara 200.
Hakuna sababu na huu ni mwaka wa tano.
Nani anajali unafikiri?
Umewahi kufiwa?Na mtu yoyote wa karibu?
0
 
Aliposema ndani ya siku saba choo kijengwe hujapaona?
Ndani ya miaka 5 ya uongozi wake hili halikufanyika wateuliwa wake wakiwepo wanafanya kazi zake, je atasimamia mwenyewe kazi ikamilike ndani ya wiki moja? Tatizo kubwa hapa ni yeye mwenyewe na liko nchi nzimà linatokana na uteuzi kwa kuwaangalia usoni wateule kujua ni nani, wanatoka wapi na wanamuweka mbele Mungu yupi badala ya kuangalia uwezo na uzoefu wao. Nyumba ya DC ni Ikulu ya kufikia Rais Wilaya yoyote isiyo na State Lodge rasmi. Wafanya biashara watashangaa siku moja kumkuta Rais wao mpendwa chooni wakienda kujisaidia nyumbani kwa DC. Afadhari watumie nyumba ya DED.
 
Matatizo Kama haya Ni matokeo ya wateuliwa KUWA na kiburi Cha dharau,

Huwezi kukusanya ushuru Halafu soko halina choo.

Ikiwa mwenye hoteli TU analazimishwa awe na choo sembuse soko?

Bwana au Bibi Afya sijui anakaguaga Nini kwa Wafanyabiashara akashindwa kukagua choo Cha soko?
 
Hah Hah siasa haihitaji hasira, ndiyo tatizo la kukosa mfumo kila kitu wateuliwa kama ma-RC, DC, DED hawajiamini kutoa maamuzi wanasubiri Mh. Rais atatue. Hili pia lipo ktk mhimili wa Bunge ambapo wabunge wa CCM wanashindwa kuiwajibisha serikali wanawaachia mawaziri watoe maswali na majibu kwa niaba ya wabunge wa CCM.

Uchaguzi wa Oktoba 28 , 2020 wagombea wa CCM watakuwa wapweke hakuna wa kuwabeba kutoka mhimili wa serikali kuu (dola) wala spika kuwalinda dhidi ya maamuzi magumu ya wananchi kuchagua wabunge kutoka upinzani wenye uwezo wa kusema kwa niaba ya wananchi na kuibana serikali ili iweze kuamka toka usingizini ipate kuwajibika.
Mkuu mbona unatetea viti vya ajabu? Hivi swala la kujenga choo cha uma tena kwenye mkusanyiko wa watu ni mpaka wasubiri maamuzi kutoka juu eti kisa mfumo mbovu?. Ki ukweli wateule wengi wanamungausha sana muheshimiwa mtu unakuta hawezi kabisa kuongoza lakini ndio hivyo kapata bahati ya kuteuliwa. Hivi kweli ujenzi wa choo ni wakusubiri hadi raisi aseme. Kwanza Mh. Raisi kawahurumia sana hawa walistahili adhabu nyingine maana wanacheza na maisha ya watu.
 
Nafikiri kipindi hiki kuna shida kwa local governments kujiendesha, ni kama zimenyanga'anywa mamlaka yake. Makusanyo mengi ya halmashauri kwa sasa yatakuwa yanakwenda hazina, hivyo hata ukihitaji kutumia pesa lazima uombe kutoka huko serikali kuu jambo ambalo linazifanya halmashauri kushindwa kutekeleza mipango yake kwa uhuru kama ilivyokuwa huko nyuma.
Afu Wajinga wanashangili utumbuaji....
 
Nafikiri kipindi hiki kuna shida kwa local governments kujiendesha, ni kama zimenyanga'anywa mamlaka yake. Makusanyo mengi ya halmashauri kwa sasa yatakuwa yanakwenda hazina, hivyo hata ukihitaji kutumia pesa lazima uombe kutoka huko serikali kuu jambo ambalo linazifanya halmashauri kushindwa kutekeleza mipango yake kwa uhuru kama ilivyokuwa huko nyuma.
Wewe umenena hali halisi mkuu na ubarikiwe sana. Hili hata Raisi analifahamu sana, yaani hata ushuru wa machinjio na minada yote inakusanywa kwa mashine za EFD. Kimbembe ni pale mnapozihitaji kwa shughuli mbalimbali za halmashauri kuzipata inakuwa mbinde sana. Ukiwa mkurugenzi kuhamisha fedha za fungu fulani kwenda shughuli zingine zilizoibuka ni kosa la kuweza kukufanya utumbuliwe na hili limeshawatokea bahadhi ya maDED. yaani mpaka zile mia 5 au elfu moja za ushuru wa machinjio huko vijijini na hata ushuru wa minada zinaenda hazina!!!! yaani minada na masoko mengi huko vijijini hayana vyoo na maisha yanakwenda.
 
Tuna rais mbovu na mwenye mambo yasiyofaa. Najua ccm walilazimika kumchagua mwaka 2015 kuokoa jahazi tu kutokana na wingi wa kura kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ila hafai kabisa na akina Mwinyi na Kikwete wanafahamu na kukerwa sana na hili.

Rais Magufuli leo akiwa njiani kutoka msibani, amesimama mara kadhaa kuwasalimu wananchi na kuwasikiliza. Ameshangazwa na watu walio chini yake kushindwa kujenga choo cha soko ilihali mapato ya halmashauri yao ni zaidi ya bilioni 1.8

Rais Magufuli ametoa agizo la choo husika kukamilika ndani ya siku saba la sivyo mkurugenzi aandike barua ya kuacha kazi. Pia ameagiza siku saba wakati choo kinajengwa wananchi waende kujisaidia nyumbani kwa DC pamoja na mkurugenzi ambae nyumba yake iko mtaa wa pili kutoka soko lilipo kwani nchi haiwezi kukosa choo wakati wanakusanya bilioni 1.8.

Amesema yuko 'very serious' na suala hilo hivyo mwananchi akibanwa afungunguliwe. Amewaamirisha wawatayarishie maji ya kutosha lakini kama wana akili watajenga usiku na mchana.

Rais Magufuli amesema haiwezekani wakusanye bilioni moja kutoka kwa wananchi alafu washindwe kuwajengea choo hivyo amewataka wafanyibiashara sokoni hapo kutolipa ushuru sokoni hapo kuanzia leo mpaka siku kitapojengwa choo.

Yaani ningekuwa Kibiti leo ningekula makande ya njugu harafu kesho uharo wake angeushudia huyo DC si kwa uzembe huo.
Yanalipana posho tu kapumbavu sana
Hah Hah siasa haihitaji hasira, ndiyo tatizo la kukosa mfumo kila kitu wateuliwa kama ma-RC, DC, DED hawajiamini kutoa maamuzi wanasubiri Mh. Rais atatue. Hili pia lipo ktk mhimili wa Bunge ambapo wabunge wa CCM wanashindwa kuiwajibisha serikali wanawaachia mawaziri watoe maswali na majibu kwa niaba ya wabunge wa CCM.

Uchaguzi wa Oktoba 28 , 2020 wagombea wa CCM watakuwa wapweke hakuna wa kuwabeba kutoka mhimili wa serikali kuu (dola) wala spika kuwalinda dhidi ya maamuzi magumu ya wananchi kuchagua wabunge kutoka upinzani wenye uwezo wa kusema kwa niaba ya wananchi na kuibana serikali ili iweze kuamka toka usingizini ipate kuwajibika.
Mbona kama maamuzi ya hasira sana?Mara gari ya DED igeuzwe ambulance,huku tena watu wakajisaidie kwa DC, aisee
Magufuli hana viongozi,ajipange upya labda awapeleke crush program ya miezi mitatu mitatu ndio wapewe majukumu.
Nakiri kuwa Rais na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Dkt. Magufuli ni Mtu wa Jazba ila tukiacha Unafiki kwa 99% anaangushwa tu na Watendaji wake.
Tatizo ni yeye,tunaenda kumpumzisha October
What kind of leadership is this? Badala ya kutatua tatizo anaongeza tatizo
Ccm aspirants always claim to build the nation but they end up building their stomachs.
 
Kama nyumba ya mkurugenzi haina choo cha nje si ndio itakuwa balaa?!!!!
 
Back
Top Bottom