Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Si kawaida yangu kupongeza pasipostahili kupongeza au kukosoa pasipostahili kukosoa, ila leo kwa dhati ya moyo wangu, nakupongeza Rais wangu John Pombe Magufuli au JPM kwa hili la Kikokotoo, kwa kurejesha 50% kwa mifuko iliyokuwa ikitoa 50 na ile ya iliyokuwa ikitoa 25% ibaki hivyo hivyo na 25% katika kipindi cha mpito hadi mwaka 2023.
Nimekusikiliza hatua kwa hatua, na kusoma lugha ya mwili wako, hakika umejiweka kwenye nafasi ya mfanyakazi, na kuyabeba machungu na maumivu ya kiakili na kisaikolojia waliyopitia tangu kutangazwa kwa kanuni mpya ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Nasema asante Rais wangi. Nimefurahi zaidi ulipowaeleza wabunge wetu ukweli mchungu kuwa kama sheria hii ya 25% ingepelekwa Bungeni kuwahusu wao, hakika wasingeipitisha. Rais umesimama katikati ya wafanyakazi wa taifa hili. Umezungumza kama Baba. Ni jambo ambalo lilikuwa haliingii akilini, na wewe umesema halileti logic, kwamba nimetumikia nchi kwa uaminifu mkubwa, ninapostaafu unanipa 25% halafu unaniambia hizo zingine nitakupa kidogo kidogo hadi ufe.
Sielewi wasomi wetu wanafikiri kwa ubongo gani. Ninapostaafu, na pengine kwa uaminifu wangu sijaweza kujenga hata kakibanda, natakiwa nikalipe kodi, nisomeshe watoto, niachane na gari ya umma nipande daladala, sasa nilitaraji hiko nilichojikusanyia kingenisaidia kuweka hata kakibanda au kabiashara, unaniwekea masharti magumu, ambayo wakati najiunga na mifuko hukuniambia. Ndio maana nasema asante sana Rais wangu JPM.

Sasa tutakula mwaka mpya kwa raha mustarehe hadi lile jino la Krismas litaonekana. Asante Rais wangu, ile stress ya miezi kadhaa waliotupa hawa watu wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa inaondoka. Lakini baba, usimame hivyo hivyo ili kipindi cha mpito kikimalizika 2023 wasije tena na hadithi za ujanja ujanja au za Alinacha au Abunuasi ambazo hazina maslahi kwa mfanyakazi anapostaafu. Wewe ni Rais wetu, kwa hili nasema asante sana ila mishahara sekta binafsi kwa baadhi ya sekta ni hairidhishi na ndio msingi wa mahesabu. Wakija hiyo 2023, waje pia na fomula ya mishahara na kikokotoa.

Mungu akubariki
 
Waziri Mhagana na Mkurugenzi SSRA wang'atuke
 
Kweli nchi hii INA vichaa wa kutosha, Mh.Rais ndiye aliyeandaa kikokotoo cha mafao?, uliza uambiwe kama ni mbumbumbu wa sheria, kanuni na taratibu za mifuko. Hapa tunapaswa tumpongeze Mh. Rais kwa kuwajali wastaafu, anayepinga ni Mchawi
 
Nchi imepata rais sahihi asiyeangalia chama chake kina msimamo gani, yeye ni problem solver wa wananchi bila kujali vyama wala dini
Ila kumbuka yeye ndiye injinia wa kutengeneza hayo matatizo ili apate credit za kisiasa
 
Embu peleka hizo pumba Lumumba!
 
unajisahaulisha kuwa wapinzani ndio waliopiga kelele hadi huyo kichaa wenu akaamua kuwasaliti wasaidizi wake. Unadhani mswada hadi unaenda bungeni na kupitishwa na wabunge wa chama chake yeye alikuwa hajui
 
Tatizo LA wapinzani ni kupinga hadi mafanikio, ama kweli kwa JPM, wapinzani wataisoma namba, Jamaaa anakandamiza vibayaaa. Big up JPM. Tupo nawe bega kwa bega
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…