Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika)

Watupatie chetu kwa asilimia miamoja. Sijawa mzalendo kiasi hicho pesa yangu ikajenge reli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasioelewa wanachoomba husema hivyo. Lakini ungejaliwa kufikia umri wa kustaafu haungesema hivyo. Ukitaka kuelewa ukweli watazame wale wastaafu wa Afrika Mashariki wanavyohangaika kila mwaka kuiomba serikali iwaingize kwenye daftari la wastaafu ili wao nao wapate pensheni kila mwezi kama wenzao waliokuwa kwenye mifuko. Kawaulize wastaafu wa PPF waliolipwa 100% kila siku nasikia wapo ofisini wakiomba na wao warudishwe kwenye daftari la wastaafu ili wawe wanalipwa kila mwezi. Kuchukua chako chote kwa sasa hivi ni kutoona mbali. Ni kujifanya wewe ni mjanja wa kupanga matumizi na kwamba unayaweza. Ni kusahau kwamba binadam huwa anabadilika akiwa na pesa mkononi na anaweza kutumia pesa vibaya akabaki hana mbele wa nyuma. Hiyo ndiyo sifa ya binadamu duniani kote. Ndiyo maana ukiajiriwa kwa mkataba wa Mwaka au miaka 5 hawakulipi mishahara yako yote ya miaka 5 ili ukajijue mwenyewe. Utazimaliza pesa zote kabla ya hiyo miaka 5 na utaanza kusumbua mwajiri wako.
 

Mimi nadhani ni mapema sana. Ukweli ukiujua hali ilivyo kwenye Mifuko hiyo utawaza upya. Kwa kikokotoo hicho alichopendekeza kitumike kuwalipa mafao wastaafu, napenda kukueleza kwamba Mfuko mpya wa PSSSF hautaweza kuwalipa wastaafu wake hata kwa miaka 3 tu. Fomula hiyo inafyooooonza sana fedha za Mfuko. Fomula hiyo haina tofauti na DECI system au UPATU au PONZI Scheme. Hiyo fomula iliyopendekezwa inatumiwa na makundi ya UPATU duniani kulipana pesa kuuubwa kutoka kwenye kuchangiana wao kwa wao na hatimaye wanakuwepo watu wengine chini wanaokosa malipo au mafao wakija kudai kwa sababu ya kanuni au fomula inayotumika kulipana.

Ni vyema kushauriana na kuambiana ukweli. Hiyo fomula haipo duniani kote. Ipo tu kwenye vyama vya UPATU. Kama hukubaliani nami nenda kote duniani ukaulize fomula inayotumika kulipa mfao kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii duniani.
 
Kwanza nimpongeza Mhesh.Raisi kwa maamuzi ya kizalendo na busara ya kusimamisha kikokotozi kipya cha ssra.
Ili kuondoa dhana ya ubaguzi wakati mifuko yote ni kwaajili ya watanzania,, tunapoenda kama taifa kutengeneza kikokotozi kimpya ni vema na haki mifuko yote miwili,NSSF na PSSSF ikawa na kikokotozi KIMOJA TUU kinachofanana kwa mifuko yote.
Hii itaondoa unyonyaji wa mfuko wa NSSF ambao mkupuo ni 25% tu.

Hii siyo HAKI na haikubaliki hata kidogo. Na ni kinyume cha matakwa ya katiba ya nchi inayozuia kutunga sheria za jamuhuri zenye ubaguzi wa aina yoyote ile.
SSRA ilishindwa kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha mifuko inawanufaisha wenye mifuko, SIYO uwekezaji wa hovyo.
 
sie wengine tulishamuelewa mapema! Wali wa kushiba unaonekana siniani! Mungu azidi kumuongoza rais wetu mpendwa Magu na serikali yetu kwa ujumla! Mungu azidi ibariki Tz!
 

hicho kikokoto wali nunua duka gani.maana kilipata mpaka mzabuni itakuwa na fisim wakipitisha na dk asiye kuwa hospital
 
mpaka sasa bado wastaafu hawajalipwa mafao yao na shule zimefunguliwa sasa hapo sijui hawakumuelewa Raisi au amedanganya mbele ya vyama vya wafanyakazi,ukienda kwenye mifuko ya jamii wanakuambia wanasubiri kanuni zipitiwe na bunge huku Raisi alisema watumi kanuni zao za zamani. Tanzania matatizo makubwa
 
Shida kubwa ni je_hayo mafao yatalipwa kwa wakati ama usumbufu wa nssf wa njoo kesho njoo week ijayo utaendelea...hata hizo 33.3 % zilizopokelewa tangu November 2018 bado hawajawalipa
...nenda nssf hapo Ilala/Temeke utawaonea watu huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hatari Sana... Yupo mwanasiasa anasema hiyo mifuko imefilisika... Pesa nyingi imeliwa ktk miradi na mikopo kwa watu maalum...
 
Hivi mbona mambo mengine yanashughulikiwa kwa haraka hivyo, iweje mafao ya uzeeni na mafao mengine yanasuasua utafikiri tunazikopa, kuna ndugu zangu wengi tu wanasubiria pension yao mpaka leo mwaka umepita sasa, hela ni zetu nyambafu sio za mkopo,
 
Inasemekana mwaka huu watachukua pesa zikafanyie kampeni, wanyonge watalia sana
 
Maamuzi ya Rais hayakuwasaidia watumishi Wa umma waliokuwa wanachangia NSSF na PPF. Wameendelea kulipwa Kwa kikokotoo chao cha asilimia 25 hata kama wote walihamishiwaPSSSF! Ukistaafu kikokotoo cha asilimia 25 kinakuhusu!! Ni maumivu mpaka basi!
 
Chonde chonde wafanyakakazi , muda wenu ndio huu
Hahahaha
Mtafukua makaburi ambayo tayari wafu walishafufuka kitambo.

Rais alishatoa maelekezo ya kusimamisha hicho kikokotoo.

Hii hoja ya 2018 unaiibua leo ili kuitumia kwenye kampeni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…