Rais Magufuli achochea kuimarika kwa sekta ya biashara

Brilliant, Magufuli 5 again
Vote for Magufuli
 
Sisi sote tutamchagu magufuli kwa moyo mmoja bila wasiwasi
 
Ukiona ipo hoi ujue alikuwa halipi kodi, alikuwa anaiibia serikali.

Kusema ni kitu rahisi sana. Wengi wanaosema either wanalipwa kwa kodi ambazo hata hawajui zinakusanywa vip au ndio wale wako wako tu kwenye makampuni ya watu. Hawajui nini kinachoendelea.

Napata tabu sana napoona maswali magumu yanatolewa majibu rahisi kweli kweli. Elimu yetu inakwama wapi?
 
Mleta post,
Umeshawahi kufanya biashara hata ya ujugu?
 
Okay twende taratibu, kwanini wengine biashara zao zilikuwepo na bado zinaendelea kuwepo, tena zimezidi kupata mafanikio zaidi?
 
Okay twende taratibu, kwanini wengine biashara zao zilikuwepo na bado zinaendelea kuwepo, tena zimezidi kupata mafanikio zaidi?

Umefanya tafiti kujua biashara ngapi zipo na ngapi zimefungwa? Umefanya tafiti kujua makampuni mangapi yako hoi hayajiwezi? Am just curious. The gates for collections are narrowing down! Ndio maana kuna wakati review za kodi zinarudi mara mbili mbili. Unashangaa kulikoni. Yes Covid has destroyed the world economy. But we must protect ours by protecting the businesses around
 
Okay Labda unisaidie wewe sasa, kunipa takwimu hapa ya hizo biashara, maana ndo ilikuwa hoja yako ya kwanza kuivamia hiyo
 
Okay Labda unisaidie wewe sasa, kunipa takwimu hapa ya hizo biashara, maana ndo ilikuwa hoja yako ya kwanza kuivamia hiyo
Sitaweza kukupa maana nina mambo mengine muhimu ya kufanya zaidi ya kupiga siasa toka asubuhi mpaka naenda kulala. Sio kila kitu naunga mkono. Hili suala la biashara na kodi zake, JPM aliwekee jicho la ziada sasa, ili ustawi uwepo. Wasiojua biashara asikubali wawe ndio washauri wake. Wengi wanamdanganya.
 
Hapana huna hizo data za uongo unazozisemea, ndio maana umekimbilia mgongo wa kuwa huna muda wa siasa.
 
Miaka mitano jamaa harudishi tax return refund kwa makampuni, anachoche njaa.
 
Na Alwatan Mabruki

Mara baada ya nchi yetu kupata uhuru iliamua kufuatia mfumo wa siasa ya ujamaa na kujitegemea na ilipofika mwaka 1967 lilitangazwa Azimio la Arusha ambapo njia kuu zote za uchumi zilikuwa zinamilikiwa na kusimamiwa na dola ikiwemo mifumo rasmi ya masoko ya mazao. Mashirika mbali mbali yaliundwa ili kusimamia biashara ya mazao, kwa mfano, GAPEX ilihusika na uuzaji mazao nje ya nchi na biashara ya mazao ya ndani sehemu kubwa ilisimamiwa na kuendeshwa na vyama vya ushirika. Mwanzoni mwa miaka ya 1990 mfumo wa uchumi duniani ulianza kubadilika. Ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ulitekelezwa ili kuendana na dhana mpya ya soko huria. Hali hii kwa namna moja au nyingine iliathiri mfumo mzima wa masoko kwa bidhaa mbalimbali.

Kutokana na mabadiliko mengi katika nyanja za biashara yanayotokea duniani kote ikiwemo Tanzania, Serikali imekuwa ikifanya mapitio ya Sera na Sheria ili kuboresha mazingira ya biashara nchini. Serikali kwa kushirikiana na washirika wa Maendeleo kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (MKUMBITA) imefanya maboresho kadhaa kwa kuangalia changamoto zilizokuwa kikwazo kwa kufanya biashara kwa ushindani na wakati huo huo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutambua kuwa biashara ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda na sekta nyingine za kiuchumi na kijamii. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2015 - 2020), Chama tawala kimeendelea kuisimamia Serikali na kuhakikisha sekta ya biashara inaendelea kuimarika na kutoa fursa za masoko kwa mazao na bidhaa na kuwaunganisha wananchi na masoko yenye upendeleo wa ushuru wa forodha kikanda na kimataifa.

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni kuboreshwa kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Mafanikio mengine yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa na huduma kwenye masoko ya kikanda yanayotoa fursa za upendeleo maalum _(preferential market access)_ ambapo kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018 Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Pesa za Kitanzania milioni 662,492,000, bidhaa zilizouzwa zaidi ni pamoja na madini ya Tanzanite, Chai, Kahawa, Sigara, Dawa na Vifaa Tiba.

Pamoja na Kuimarisha mahusiano ya kibiashara na nchi za nje ikiwemo nchi za Ulaya mfano Uswisi ambapo mauzo ya Tanzania yaliongezeka kutoka Pesa za Kitanzania milioni 334,311,331.2 mwaka 2015 hadi milioni 591,491,000 mwaka 2018 na nchi za Asia kwa mfano India ambapo mauzo yameongezeka kutoka Pesa za Kitanzania milioni 44,631,312 mwaka 2015 hadi milioni 97,566,000 mwaka 2018.

Serikali imeweza kubuni na kuendeleza mikakati ya uhamasishaji wa Watanzania kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani, kuratibu ujenzi wa masoko ya kimkakati katika maeneo ya mipakani ili kuwapa wakulima, wajasiriamali wadogo hususan wanawake na vijana fursa ya kuuza mazao yao nje ya nchi.

Mbali na mafanikio hayo, kumekuwepo na changamoto kadhaa katika biashara, ikiwemo upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji na biashara, uzalishaji wa mazao na bidhaa usiokidhi mahitaji ya ubora unaotoa ushindani katika soko la ndani na nje, Ufahamu mdogo wa matumizi ya TEKNOHAMA, kukosekana kwa Nishati ya umeme ya uhakika na ya kutosheleza kuendesha mifumo, na uelewa mdogo wa wadau kuhusu sheria na kanuni zinazosimamia biashara.

Aidha, serikali inapaswa kutatua changamoto hizo kupitia Wizara pamoja na Taasisi zilizochini yake kwa kuendelea kubuni mikakati na mipango ya kutekeleza majukumu yake ili kuongeza mchango wa Sekta ya biashara na masoko katika pato la taifa. Pia Kuweka mikakati madhubuti ya kuimarisha biashara ya mtandao (e-commerce) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa kweli nitakua mchoyo wa fadhila nisipo ishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari Dkt. Joseph Pombe Magufuli kwa kutambua umuhimu wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara, uchukuzi na mawasiliano kwa lengo la kuwezesha ujenzi wa uchumi imara unaojitegemea. Manufaa elekezi ni pamoja na kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na kuongezeka kwa matumizi ya fursa za kijiografia na mapato ya nchi kwa kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi na wananchi kwa ujumla.
 
Magufuli ameua biashara nchini amewafilisi wafanya biashara hafai kwa lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…