Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Umelallnika bila kua na hoja kama mtu anae jitamhua ama alie soma
Ungekua unajitambua baada ya vihoja vyako ungetoa na suluhisho
 
Great work, mnafanya kazi nzuri so far.

Lakini, wewe kama mwana JF ambaye upo for almost 11yrs kama active member (na unakumbuka why we exist): Unakubaliana nami kuwa kauli ya Rais leo ina makosa?

Natambua, kwa nafasi uliyo nayo inaweza kuwa ngumu kukiri, ndani ya nafsi unanielewa vema tu.

Tuseme kweli mlifanikiwa kuziondoa hizo masks mtaani, leo alikuwa anaongelea nini? Kuwa we are compromised hadi leo?!
 
Yani pandemic lina zaidi ya mwaka, limefika mpaka Ikulu yake, yeye bado anasema tu mpaka leo?

Tena kuhusu kitu simple kama barakoa?

Huu uzembe gani huu?
Nimeshangaa, he admitted hadi ndugu zake wamepigwa, watendaji wake wa karibu wamepigwa. Halafu yeye kama Rais anapokiri haya anataka tuchukulie “POA” tu?
 
Korona isingeingia sebuleni angeendelea kutangaza dawa ya Bupiji. Rais utafikiri Miganga WA kienyeji toka Sumbawanga.
Unajua unaweza kumfananisha rais na mganga wa kienyeji kutoka Sumbawanga, halafu ukawa umemtukana huyo mganga wa kienyeji kutoka Sumbawanga kwa kumfananisha na rais huyu.

Mganga wa kienyeji akakwambia hata mimi na magumashi yangu yote sijafikia magumashi ya Magufuli tafadhali usinifananishe naye unanionea bure.
 
Simply sijaona kosa la Magufuli, bali ninachokiona ni chuki binafsi tu. 2020 alikuwa Rais yeye but hii ni vita, na vita ina mbinu nyingi na ndio maana hata vifaa vya kupimia corona walivishtukia baada ya kuona matokeo yanayotoka yana mashaka. Kumbuka wakati wanashtukia vifaa, of which kipindi hicho bado vifaa vya upimaji vilikuwa vichache kupatikana hata huko wanakotengeneza, tayari kulikuwa na kontena nyingi tu za barakoa zimeingia na zikapimwa kama zimefikia viwango vya kawaida bila kujua hizo ni carier za virus. Ishu ya mapapai ndiyo iliyofungua macho na kujua kumbe hata barakoa zina changamoto kama ambavyo baadhi ya vifaa vya upimaji. Nadhani unajua nini kiliwapata watu wa maabara kuu ya serikali ambapo ndani yake kulikuwa na watu wa usalama wa taifa ambao kiutaratibu sisi wananchi haturuhusiwi kisheria kujua wamechukuliwa hatua gani.
 
Nimeshangaa, he admitted hadi ndugu zake wamepigwa, watendaji wake wa karibu wamepigwa. Halafu yeye kama Rais anapokiri haya anataka tuchukulie “POA” tu?
Anaweza kumaliza kwa kukwambia "ni mapenzi ya Mungu tu" akafunga mjadala.

Ukianza kuingiza siasa kwenye dini kipi kitakukataza kusema hivyo?
 
Kwahio badala ya kuhakikisha mbovu haziingii unaona ni sawa kutoa taharuki kwamba zinazotoka nje zina matatizo ?, Mteja layman asiye na kipimo kwenye macho atajuaje ipi ndio na ipi sio (au ndio kuwaambia wasivae barakoa yoyote ambayo sio made in Tanzania)

Na je wale walioleta ambazo ni nzuri (TBS wamezipitisha ) nao unasemaje ?, Pia unataka tuamini kwamba viwanda vyetu sasa vipo bora kiasi kwamba quality ni top notch ? Kumbuka ni hivi hivi viwanda watu wakinunua khanga au shati linapauka likipigwa upepo tu let alone ukifua...

Na hawa wazungu ni wajinga kiasi gani waweze kuweka sumu kwenye barakoa tu na sio vitu vingine ambavyo kila siku vinaingia ? Na kama waligundua hilo na evidence wanayo kwamba kampuni fulani ilileta misaada ya barakoa zenye matatizo ni hatua zipi zimechukuliwa ili kuwawajibisha ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…