Tatizo la Jiwe no kupenda attention...na hii ndiyo Kiki aliyoipanga kuja nayo baada ya kutumbua kuishiwa nguvu
Dar itabaki kuwa jiji hata akiifanyia figisu....na Chato kitabaki kuwa kijijini. Kamwe hawezi kugawa jiji la Dar vipande vipande.
Unapozungumzia Jiji la Dar es Salaam unazungumzia manispaa za Ilala,Temeke,Kigamboni,Kinondoni na Ubungo. Hizo ni mbwembwe na kutaka attention! Kwa maana nyingine Dar ea salaam itaendelea kuwa na hadhi ya Jiji regardless mgawanyo wa kimamlaka wa kiserikali za mitaa
Kiutawala itasomeka hivyo na kuleta ukakasi manispaa ya ilala kuitwa Jiji la Dar es salaam.
Kiutendaji halmashauri ya Jiji (DCC) iliyovunjwa haikuwa na kazi! Kwa kuwa manispaa zilikuwa zinajitegemea na zilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya bajeti zake za ndani. Rais alitakiwa avunje Mamlaka iliyoitwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (Dar city council). Hili ndio aliopaswa ashauriwe.
Halmashauri ya Jiji ni ngazi ya juu kabisa katika Mamlaka za serikali za mitaa ikifuatiwa na Manispaa,(Municipal Councils), halmashauri za miji (Town Councils) na halmashauri za wilaya (District councils). Mgawanyo huu unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na uwezo kimapato,uwepo wa shughuli za Kiuchumi k.v viwanda,uwepo wa huduma za Kijamii k.v vyuo n.k
Dar es salaam hakuna wilaya inayoitwa D'salaam kama ilivyo Dodoma,Tanga au Mbeya hivyo haileti maana Ilala kuwa halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, ni sawa na kuipa jina Wilaya ya Ilala kuwa na jina jipya wilaya ya Dar es salaam. Hapo ndipo utapata Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam