Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Mkuu uongozi wa Tanzania una matatizo mazito mno ! sijawahi kuona !
Maana tunaanza na HOJA ya kwanza ni kwa nini kusiwe na sifa maalum ya Mamlaka ya Serikali ya mitaa kuwa Mji mdogo, Mji,Manispaa au Jiji.

Lakini pia kuwe na sheria ya kuanzisha na kufuta mamlaka za miji.

Siyo mtu anaamka na kutangaza kuanzia leo eneo fulani linakuwa Mkoa ama Wilaya fulani inahamishiwa au kuondolewa toka Mkoa fulani.
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadhi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua daraja la juu la Ubungo leo Jumatano Februari 24, 2021.

Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.”

"Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa.

Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati.

Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli. Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

“Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala,” amesisitiza.
Source : GILLY BONNY ONLINE TV
 
Mliokuja Dar na Malori ya Ng'ombe pamoja na Treni za Mizigo wala huwa hamjifichi. Washamba wakubwa nyie. Ilala ndiyo Dar es Salaam na Tanzania hutaki tafuta Sumu ya Panya ikoroge, uinywe ili Ufe kabisa.

Wala hujakosea maana nilidandia gunia za mkaa na saa hii nakaa kwa Lulenge nyuma ya airport tu hapo ila si bado nipo Dar, Utafanyaje sasa mkuu
 
Naomba msaada wa kueleweshwa hapa wakuu, hii ina maana gani na itakuwa na tofauti gani na ilivyokuwa mwanzo, pia faida zake hasa kwa sisi tunaoishi kwenye hilo Jiji linaloitwa Ilala kwa Sasa?
Msaada pls hapa nimestuck.
Inamaana kwamba mkoa wetu wa Ilala sasa umekuwa jiji. Hakuna halmashauri ya jiji la DSM kama hapo mwanzo. Tunapoelekea jina Dar es Salaam linaenda kutoweka.
 
Yamekua
IMG-20210224-WA0060.jpg
 
Dsm ilikuwa inaundwa na manispaa nne kinondoni,ilala,,ubungo na kigamboni
halmashauri ya jiji la dsm ilikuwa inasimamia halmashauri za manispaa zote nne lkn haina eneo lake rasmi la kiutawala,halmashauri ilikuwa na uwezo kuuchukua mradi wowote katika manispaa yyte na kuendeleza na kugawana manispaa inayopatikana mradi kwa utaratibu maalum
hvyo alichokifanya ni sahihi tu
Tano...umesahau Temeke
 
Labda sasa Kariakoo ndani ya jiji jipya itakuwa kama Dubai biashara masaa 24 , mwanga wa kutosha usiku wote lazima biashara zilizokufa Kariakoo ambazo wafanyabiashara kutoka Zimbabwe, Congo, Malawi , Zambia , Comoro n.k warudi na wasiwaze kwenda China wala Dubai kufuata mzigo.

Na machinga wote watasombwa kubwagwa Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni.

Jiji la Dar es Salaam "mpya" litaambaa na barabara ya Nyerere kuchukua ukanda wa Tazara Stesheni DSM, viwanda vote Ukanda wa "Pugu Road " hadi Airport ya Uwanja wa Kimataifa wa JNIA. Jiji hili jipya litaamba Kurasini mivinjeni mpaka bandari zote kavu na bandari yenyewe. Maeneo ya Mjini Kati Posta, Gerezani, Mnazi Mmoja , Upanga, Magomeni hadi Ukanda wa Morogoro road Ubungo Maji mpaka Stendi Mpya Mbezi Louis.

Bila kusahau maeneo ya Oysterbay , Masaki hadi Mawasiliano 2000 stendi yatakuwa ndani ya Jiji jipya la Dar es Salaam lenye miundo-mbinu ya flyover, madaraja , BRT mwendokasi, superfast internet, bila uchafu wa meza za wamachinga, bidhaa kupangwa barabarani sehemu za wenda-kwa-miguu.

Hii itasaidia Jiji jipya la Dar es Salaam kukusanya kodi kwa kusaidiana na TRA kwa ufanisi huku miundo-mbinu ikibaki wazi na safi kwa wenye shughuli zenye TIN Number TRA na Dar es Salaam jiji jipya kuwa ULAYA ndani ya Africa.

Hawa wamachinga "wametuchelewesha" sana Dar es Salaam yenye miundombinu na magorofa makubwa kuchangia kodi, kwani biashara zimekufa na wameharibu muonekano wa jiji kisa wamechangia Tshs. 20,000 kitambulusho cha mfanyabiashara mdogo wakati wanaharibu mazingira ya biashara kubwa, biashara za kimataifa na hata watu wanakimbiza ofisi zao toka mjini kati kuzipeleka maeneo ya Victoria, Makumbusho ili kuondokana na hawa "wakuja" machinga wasioelewa maana ya jiji.

Watendaji nao wa serikali madiwani, mameya, waDC , Mkuu wa Mkoa bila kusahau viongozi wa CCM ngazi zote Dar es Salaam nao wamekuwa waoga na kukosa ubunifu kulifanya jiji kuwa Dubai au Singapore ya Afrika huku serikali imewekeza matrilioni ya fedha kuinua hadhi ya mji wa Dar es Salaam uwe wa kisasa kufuatana na uwekezaji mkubwa wa Maendeleo ya Vitu uliowekwa jijini Dsm.
 
Hapa nimemuelewa rais alichofanya nikupunguza Gharama za uendeshaji wa iliyokuwa halmashauri ya jiji wakati wanaounda hilo jiji wapo hapahapa ilala ,kinondoni na temeke.

Amefanya vyema ilala inaweza ku handle shughuli zote za iliyokua halmashauri ya jiji. Wale wazamani mtakumbuka iliyokua tume ya keenja mambo hayakutofautiana sana na hili.
 
Hizi sarakasi ngoja tuone mwisho wake , Chanika ni Jiji , Mwenge, mikocheni , Masaki , oysterbay ni Manispaa !

Hii move ina malengo fulani ya hovyo sana lakini mahesabu yake wameyakosea mno !
Funguka dogo
 
Ndugu zangu Wachagga hapo Kimara walikuwa wanaaga kila January kuwa wanarudi jijini Dar sasa watakuwa wanaenda Wilaha ya Ubungo wakati ndugu zao pale Moshi wafakuwa jijini soon
🤣🤣🤣🤣 ngoja wakuvamie
 
Hapa tunashindwa kuelewa, kwa mfano Mwanza mjini (kati) kuna wilaya mbili ambazo ni Nyamagana na Ilemela.

Ilemela imepewa hadhi ya kuwa manispaa ya Ilemela, lakini hakuna Manispaa ya Nyamagana badala yake Nyamagana imebeba hadhi ya Jiji la Mwanza.

Katika matukio yote ukisikia wanaongea jiji la Mwanza maana yake wanaongelea wilaya ya Nyamagana na sio mkoa wote.
Clarify...
 
Hapa nimemuelewa rais alichofanya nikupunguza Gharama za uendeshaji wa iliyokuwa halmashauri ya jiji wakati wanaounda hilo jiji wapo hapahapa ilala ,kinondoni na temeke.

Amefanya vyema ilala inaweza ku handle shughuli zote za iliyokua halmashauri ya jiji. Wale wazamani mtakumbuka iliyokua tume ya keenja mambo hayakutofautiana sana na hili.
Kama umeelewa wewe ni vizuri nadhani utawaelimisha na BAVICHA hapo Ufipa
 
Back
Top Bottom