Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

We naye ni mmoja wa wajinga
 
Hapa nipo kwenye panton feri wamefungulia Singeli sauti ya juu balaa, sijui wanashangilia ilala kuwa jiji
Kwa Sasa ni saa 0434 alfajiri
 
Hili suala hata MATAGQ wenyewe hawaelewi chochote
Anyway huku Ubungo kijijini maisha yamekuwa magumu nataka niamie jijini Ilala
 
Umesahau kusema hili, hata wamachinga wote wapo Ilala
 
Umeiweka vizuri mkuu, ninakushukuru lililofanywa lina faida nyingi kwa uchache:-
1. Dar es salaam Jiji lililokuwepo ilikuwa kama kupe tu kunyonya Halmashauri zingine;
2. Ilikuwa inaongeza gharama za uendeshaji bila sababu Mf. Magari, watumishi, n.k
3. Kuweka mgongono wa kimajukumu
Kutaja japo kwa uchache.
 
Ndugu zangu Wachagga hapo Kimara walikuwa wanaaga kila January kuwa wanarudi jijini Dar sasa watakuwa wanaenda Wilaya ya Ubungo wakati ndugu zao pale Moshi watakuwa jijini soon
Moshi kamwe haiwezi kua Jiji hata kama ina vigezo, Jiwe hawezi kubali hilo labda akutoka madarakani
 
Buguruni, Vingunguti, Kivule, Gongolamboto, Chanika, Pugu ndio jiji halafu Masaki, Oysterbay, Msasani, Mbezi beach, Kinondoni, Sinza eti ni Manispaa tu, Maajabu!
 
Tusubiri tu kwa uvumilivu,ipo siku ataibeba dar nzima kama ilivyo na kwenda kuitua chato
 
WATU WALIPOKUWA WANAONGELEA DEMOKRASIA WATU HAWAKUELEWA WENGINE , DEMOKRASIA IKIBAKWA KWA WAPINZANI BAADAYE HUHAMIA NDANI YA CHAMA TAWALA .....UAMUZI WA KUFANYA ANAVYOTAKA KWENYE SERIKALI ZA MITAA NDIO ULIOKUWA UNAFANYA ALAZIMISHE MADIWANI WOTE WAWE WA KWAKE ...NI WAZI KUNGEKUWA KUNA MADIWANI WA VYAMA VINGI BARAZANI HANGETHUBUTU KUFANYA HIVYO KWAKUWA MALALAMIKO YANGEKUWA MENGI, KAMA TU WAKATI ULE KUWEKA MEYA WAKE ALIKUWA ANASHINDWA ,KWA KUHOFIA VURUGU ....LEO SASA CCM WAMEONA HUYU MTU ALIVYOKUWA NA DHARAU.....UNAVUNJA HALMASHAURI HATA BILA KUSHAURIANA NA MEYA WAHUSIKA .....DHARAU SANA .,ANAJUA HAWANA LA KUMFANYA NA HAWANA PA KWENDA KULALAMIKA AU KUNGEKUA NA WAPINZANI BARAZANI WANGEUNGANA NAO ,HAWAPO.
NA HUU NI MWANZO TU WA UVUNJAJI WA DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA CHAKE MWENYEWE .....HATA MKAPA ALIPOVUNJA HALMASHAURI HAKUKURUPUKA ALIFANYA UTAFITI NA ALIWASHIRIKISHA UN-HABITAT ....
WATU WANASEMA HATA MAMEYA HAWAHESHIMIKI TENA ANAWAONA KAMA MADIWANI TU .. MNAONA HATA ALIVYOMTUKANA MEYA WA MOROGORO HADHARANI .....UNAJUA MTU AKIKUPA KITU BURE LAZIMA AKUSIMANGE ....KAMA PIA WABUNGE WANAVYOSIMANGWA BILA MAGUFULI HAWANGEFIKA BUNGENI HIVYO WAFUNGE MIDOMO
 
Bakhresa anaishi wapi?
Diamond anaishi wapi?
Maraisi wastaafu wanaishi wapi?
Mwamunyange anaishi wapi?
Nyumba za mawaziri ziko wapi?
Mo anaishi wapi?
Acha ushabiki ilala ni ofisi tu Ila madoni wote makazi kinondoni
 
Rais kafanya jambo jema.

Ukisema kwamba Dar hakuna Wilaya inaitwa Dar es Salaam, hata Kilimanjaro, Ruvuma, Rukwa, Mwanza, Mara, Pwani Manyara, Kagera, pia hakuna Wilaya zenye majina ya hiyo mikoa.

Rais kafanya jambo jema kuokoa mapato yaliyokuwa yanaenda Halmashauri ya Jiji isiyokuwa na eneo la kiutawala na isiyo na miradi
 
Hoja siyo ku criticise. Hoja ni kwamba jamaa humu wametoa maelezo yanayoeleweka hadi tusioelewa tumeelewa.

Mimi mmojawapo sikuwa naelewa lakini niliposoma thread hii nimeelewa.

Tabu ni baadhi yenu kama wewe mmeng'ang'ania kilichomo kichwani na ambacho ni wrong.

Kwanza waliotuelewesha hadi hapa inaelekea wamesomea mambo haya na wamefanya kazi nzuri na haikuwa lazima kutuelewesha.

Wametupa elimu ya bure wewe unataka warudierudie. Ni wajibu wako usiyeelewa kurudiarudia usichokielewa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…