Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Kubana matumizi ni muhimu.mheshimiwa Rais anabana matumizi.
 
Naona kama maluweluwe tu au ndo uchumi wa kati????mbona mambo mengi yanatakiwa kufanywa zaidi ya hilo
Rais Magufuli amevunja halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi halmashauri ya manispaa ya Ilala kuwa jiji la Dar es salaam.

Source ITV habari
 
Yule kazoea kuwadanganya mataga wenzake kama ww
Usiogope Dr Tulia aliugua mara mbili lakini anadunda kama kawa!

MwanaFA aliugua na sasa yuko bungeni

Piere Liquid aliugua na sasa ni meneja wa Saidia Simba Ishinde

Usiogope bwashee chukua tahadhari
 
Tupo wote.. ukipata maelezo mazuri naomba unitag Mkuu.
Naomba nikueleweshe ili na wengine waelewe..ila maelezo yangu ni kutokana na jinsi nilivyoelewa...kama kuna ambae hajaelewa naamini hapa atanielewa...ila ikiwa nimetoa maelezo yasiyo sahihi, mwenye uelewa zaidi atafafanua ila mpaka hapa naamini nimeelewa na niko sahihi kwa asilimia 100%...Naomba usome kwa makini...


Iko hivi...zamani (kuanzia jana) jiji la Dar lilikuwa linaundwa na halmashauri/kulikuwa na mayors 6 (Temeke, Kinondoni, Ilala, Ubungo, Kigamboni walikuwa na mayors wao then DSM as a whole nayo ilikuwa na Mayor wake ambae ni mayor wa jiji zima..so jumla kulikuwa na mayors 6 ndani ya mkoa mmoja)...Kwahiyo, bajeti ya Mayor wa Halmashauri ya jiji la DSM ilikuwa inachangwa na zile halmashauri zingine 5..kiufupi zile halmashauri 5 zilikuwa na kazi ya kuchangia bajeti zao halafu tena zitoe kiasi kidogo ili kuchangia bajeti ya Halmashauri ya jiji zima..Hapo ilikuwa ni gharama mara mbili...

sasa, ili kupunguza gharama Rais ameamua kuiua halmashauri ya Jiji la dsm na badala yake halmashauri ya Ilala ndo itaplay role kama halmashauri ya Jiji...Maana yake, sasa zitabaki halmashauri 5 tofauti na 6 za mwanzo...Halmashauri za sasa zitakuwa ni TMK, KINONDONI, KIGAMBONI, UBUNGO na ILALA ambayo sasa itasimama kama halmashauri ya jiji zima...Maana yake hakutakuwa na ile hali ya mapato ya halmashauri moja kuchangia bajeti ya jiji...pesa inayokusanywa tmk itatumika tmk, the same as kino, ubungo na kigamboni halafu pesa au mapato yatakayokusanywa Ilala yatatumika kwa jiji zima maana Ilala sasa ndio halmashauri ya jiji...Hapo gharama mara mbili zitakuwa hazipo kama mwanzo.

KIUFUPI..mkoa wa DSM utabaki kuwepo na JIJI LA DSM litaendelea kuwepo ila tu kiutendaji, Ilala itakuwa inafanya majukumu ya mkoa mzima ndio maana imepandishwa hadhi kuwa Halmashauri ya Jiji...BINAFSI NIMEMUELEWA RAIS.


Ngoja nikupe mfano mwingine....

Assume, shule uliyosoma ilikuwa na form 1 hadi 4...sasa kila darasa lilikuwa linatoa kiongozi wake ambapo jumla viongozi watakuwa 4 (mmoja kila darasa) halafu pia anakuwepo na kiongozi wa shule nzima (huyu anachaguliwa mmojawapo miongoni mwa hao viongozi wa madarasa)..Jumla tunapata viongozi 5....sasa, ili kuiendesha shule mapato ya form one yalikuwa yanatumika kumlipa kiongozi wa form 1 na kiasi kingine kuchangia kumlipa kiongozi wa shule nzima maana kila darasa lazima lichangie kumlipa yule kiongozi...Matokeo yake sasa, kila darasa lilikuwa linaingia cost mara mbili...moja gharama za kumlipa kiongozi wake wa darasa na pili kuchangia gharama za kumlipa kiongozi wa shule na wakati huo huo, kiongozi wa shule anapatikana kwa kuchaguliwa mmojawapo kutoka kwa wale viongozi wa madarasa...Kikawaida huu ni mzigo mkubwa wa uendeshaji..

sasa ili kupunguza gharama, shule inaamua kuwa viongozi wa form 1, 2 na 3 watasimamia madarasa yao halafu kiongozi wa form 4 ndo anapewa hadhi ya kuwa kiongozi wa shule nzima..kwahiyo mapato ya form 4 yatatumika kuendeshea shule nzima (Hakuna tena michango kutoka madarasa mengine) halafu mapato ya yale madarasa mengine yatatumika kwenye madarasa yao tu..Hakuna kuchangia tena kwenda kwa uongozi wa shule nzima....Ila bado shule itaendelea kuitwa jina lile lile..Hadhi mpya ya Form 4 haina effect kwenye jina wala hadhi ya mkoa kwa ujumla..


Maana yake...JIJI LA DSM litaendelea kuwa hivyo..MKOA wa Dsm utaendelea kuwepo..Wilaya za Ilala, tmk,kino, ubungo na kigamboni zitaendelea kuwepo....ila katika utendaji na usimamizi wa bajeti na miradi ya mkoa mzima...Ilala au maamuzi ya Ilala ndio yatasimamia jiji zima...So, ilala ni monitor wa Jiji (dsm) ila bado jiji litajulikana kuwa JIJI LA DSM...


Mpaka hapa naamini walau utakuwa umeelewa japo kwa kiasi kidogo...!
 
Kwa kadri ya macho yangu uamuzi wa Magufuli wa kuvunja halmashauri halali ya jiji UMEPINGWA KWA ZAIDI YA 95% , ajitafakari sana kama bado ana ushawishi wowote
 
Tatizo suala hili nadhani bado halijatolewa ufafanuzi wa kina tuvute subira ndg yetu jaffo nadhani mda sio mrefu atalitolea maelezo ya kina tuwe na subira na #tusipende kuropoka ovyo
Ukiacha uongozi tu , Jaffo ana uwezo gani wa kutuzidi sisi wakati ukweli wote uko wazi kabisa ?
 
Kupunguza wingi wa halmashauri. Badala ya halmashauri sita (jiji na manispaa tano) sasa zinakwenda kubaki tano tu.
Hiyo kitu mwananchi wa kawaida inatusaidia nini kama Ilala yenyewe ndo chafu kuliko
 
Mimi sijaelewa mantiki ya maamuzi haya...

Je, ina maana Dar es Salaam inabaki kuitwa mkoa tu wakati huohuo kiutawala ikiitwa Ilala City au?

Hii itakuwa na maana na manufaa gani hasa?

Nimejaribu kupitia majiji makubwa duniani na namna yanavyojitawala/kujiendesha. Sijaona huu mfumo wa ki - Magufuli...

The biggest and most populous City in the world now ni TOKYO, Japan lenye jumla ya wakazi (watu) wanaoishi ndani ya mji mmoja 37,000,000...!

DSM hadi 2020 ilikuwa inakadiriwa kuwa na wakaazi 6,400,000 lakini kuna shida nyingi kuliko kawaida...

Kuna ubaya gani tukaenda kujifunza kwa wenzetu namna wanavyosimamia majiji yao na kuwa ktk mpangilio na miundombinu ya usafiri na maji safi na taka mizuri kabisa...

Solution ya matatizo ya jiji la DSM siyo kubadili majina bali in kukaa chini na kuja na mkakati Wa kitaalamu zaidi ukilenga kuboresha Master plan ya jiji lote...
 
Elimu yetu ni dhahiri shahiri ina shida sana. Watu wana vyeti ila bongo zao ni tupu.

Haya ndio madhara ya kucheza na Elimu. Kitu kimezungumzwa kwa Kiswahili fasaha watu mnashindwa kuelewa nini!?

Hii ni hatari kwa Taifa.

Wewe ndiye mwenye shida upstairs. Usitusingizie sisi wengine kuwa hatuna elimu ya kutosha kuelewa...

Tunaelewa vizuri sana. Lakini kinachohojiwa na wengi hapa ni "mantiki" ya maamuzi haya ni nini...

Aidha, kama wewe unaelewa, basi jaribu kutueleza kutakuwa na tofauti na manufaa/faida gani kwa wananchi kwa kubadili jina la jiji lote la DSM kuwa Ilala City tofauti na lilivyokuwa linaitwa Dar City...
 
Huyu mzee naye amebakiza kiki tu mjini, hana swaga yaani kwishney
 
Kama una ubongo mkubwa ,nadhani utakuwa umeelewa nia ya jp kuifuta hal.ya jiji la dar. Badala yake ni jiji la ilala.
 
Huko masaki zaidi ya wanadiplomasia na vigogo kwenda kulala kuna uzalishaji gani? Unaweza ukakuta pato la stendi ya gomzi ni Kubwa kuliko kinachoingizwa Kata nzima ya masaki sijui ni kata kijiji au tarafa.
 
Hivi ni kwamba watu hawaelewi kweli au wanapenda malumbano tu?

Unaposema kwa mfano jiji la tanga inamaanisha hata muheza ni sehemu ya jiji la tanga ila makao makuu ya jiji la tanga yanakua ktk manispaa ya tanga.

Kwa hiyo jiji la dar es salaam litaendelea kuwepo ndani yake ikiwepo manispaa ya temeke, ilala, kinondoni, kigamboni na ubungo lakini makao makuu ya jiji la dar es salaam yatakuwepo ktk ofisi za halmashauri ya ilala.

Kama na mm nitakua nimeelewa tofauti nipo radhi kuelimishwa au kufahamishwa juu ya hilo.
 
Back
Top Bottom