Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

huyu Ndalichako mbona anajadiliwa sana? Mwenye wasifu wake atuwekee hapa tafadhali
 
mnafurahia kwa sababu yule mama ni mdini balaa, mnajua atakachowafanyia wanafunz wa kiislam
 
Waislam watafeli sana... hadi div 7 zitawekwa.. haaaaaa
 
Arudishe elimu mahali pake. Huu ufaulu wa kuunga unga ambao hata mzazi hujui kama mtoto amepata ngapi aufutilie mbali.
 
Yaani Magembe...?? Hapa Magufuli kachemka hadi basi...!!! Haki ya Mungu...!!

Prof. Magembe.. ni wa kumpa UWAZIRI...? this is a big joke
 
Ila wadau naona mnamsifia mama Joisi,lakini kuna mambo lazima tuyaangalie kwa mapana
KWANZA:Joisi anakuja wizarani tayar ameshaingia kwenye siasa,nafasi anayoshika ni ya kisiasa na si ya kiutendaji teeeena,so utendaji wake utakua ni wa kisiasa siasa,ni afadhali angekua Katibu Mkuu wa Wizara.
PILI:Joisi anaingia wizarani tayar kuna sera mbovu kabisa ya elimu ya mwaka 2014,so anakuja kuitekeleza sera mboooovu kabisa ambayo ukweli haina tija kwa mustakabali wa elimu Tanzania,je ataleta maajabu chini ya sera hii?tukukumbuke hii sera imepitishwa mwaka jana tu na hata wadau weengi wa elim bado hawajaijua,hiko ni kisiki kingine.
TATU:Joisi anakuja wizarani tayari viwango vya ufaulu kwa sekondari vimeshapangwa,je atavibadili tena?je mabosi wake watakubali? Ambao ni (CCM na MAMLAKA ZA JUU YAKE).
Nne:Mtihani wa kwanza kwa Joisi ni suala la ada elekezi kwa shule binafsi,sote tunajua hizi shule binafsi nyiiingi ni za hawa tunaowaita vigogo hukohuko kwenye system,je Joisi atafanikiwa hilo?
TAno:Ili Joisi afanikiwe yule profesa pale wizarani aondolewe kwanza (Katibu mkuu wizara ya elimu) maana haendani na spidi ya serikali hii,na ni chanzo cha changamoto kadhaa,lakini poa wizara ya elimu jamani ingepaswa kuwa na manaibu wawili,hilo halikwepeki kabisa,maana kuna.mambo ya shule za awali (nasari na praimari),kuna elim sekondari,kuna vyuo vya ufundi na ualim na kuna vyuo vikuu,pagumu hapo!!!
MWisho,namtakia kila la kheri mama Joisi,lakini namkumbusha now ameshakua mwanasiasa kamili,NEKTA ilikua taasisi ndogo nowana wizara,asije kuharibu hata ya NECTA tukayasahau
 

Mdau umeona mbali sana,sikua nimesoma comment yako kabla sijacomment ila ulichoandika ndicho nilichotolea angalizo hapo juu,
Nakupa KONGOLE
👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
 
Yaani Magembe...?? Hapa Magufuli kachemka hadi basi...!!! Haki ya Mungu...!!

Prof. Magembe.. ni wa kumpa UWAZIRI...? this is a big joke

Yaani kachemka kweli. Hakika CCM ni ile ile. Huyu alikua kwenye ile list ya 'Mizigo' enzi za JK.
 
Atakuwa ametubu dhambi zake, maana ngazi aliachia mwenyewe. Ni heri ametubu kiukweli lakini kama ametubu kiuongo-uongo ataumbuka tu kama alivyoumbuka Lowassa.

Ningeona ajabu sana kama ungekomenti bila kumgusa mbowe,lowassa,ama chadema in general....
 
Wana Wa Islaeli Walianzia Utumwani Kabla Ya Nchi Ya Ahadi, Watanzania Sasa Tutarajie Neema Ila Wezi Na Wazembe Watarajie Mkosi
 
Kwanza Ongera, 1.Madaraja Ya Ufaulu Kwa Wanafunzi 2. Madaraja Ya Mshaara Kwa Waalimu Wengi Wametumikia Daraja Moja Kwa Mda Mrefu 3. Mtaala Wa Elimu Ifanye Elimu Ikidhi Mahitaji Ya Viwanda, Kilimo Na Ufugaji 4. Weka Mfumo Unaojali Vipaji Vya Watoto Mfano Mtoto Anaweza Kuanza Chuo Cha Awali Akaenda Mpaka Chuo Kikuu Kwa Fani Yake Bila Kupitia Sekondari. Mungu Akubariki Utimize Majukumu Yako
 
Nimeisoma post yako ambayo umeijadili kwa kirefu zaidi ambayo ni kweli tupu na ndo hayo hayo ambayo, humu humu jamvini, hatimae tutaona hafai wakati Ndalichako ni mtendaji mzuri sana. Na endapo Mchome ataendelea kubaki kwenye nafasi yake ya ukatibu mkuu, hiyo itakuwa ni tatizo sana kwa Ndalichako. Yaani still namtamani huyu mama angekuwa katibu mkuu!
 
Tumuombee huyu mama ili aweze kutumbua majipu kwenye Elimu,ili yetu ilikua inapoteza mwelekeo,.sasa naona italudi kwenye njia
 
Binafsi sina taarifa rasmi kuhusu hili, kama ni kweli, wamuache huyu mama hapohapo muda wote, elimu ya nchi hii itakuwa ya kupigiwa mfano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…