Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,887
- 7,673
Yako mambo ya msingi kutafakari! Hivi katika Baraza la mawaziri. Uwakilishi wa zanzibar ni kwa asilimia ngapi?
Ni kama uwakilishi wa Chalinze tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yako mambo ya msingi kutafakari! Hivi katika Baraza la mawaziri. Uwakilishi wa zanzibar ni kwa asilimia ngapi?
Joyce Ndalichako, alikuwa katibu wa baraza la mitihani. Alishutumiwa na Waislamu kuwafelisha.
Nikiwa mwandishi wa habari za uchunguzi nililifuatilia suala hili na kulithibitisha.
Utetezi wake haukuwa na mashiko hata chembe.
Malalamiko ya Waislamu yalisababisha Rais Kikwete kumuondoa barazani.
Lakini leo hii Dk. John Pombe Magufuli amemteua kuwa Waziri wa Elimu. Tena kwanza amemteua kuwa mbunge kisha ndio kampa uwaziri.
Kuna wakati namuelewa Rais Magifuli lakini wakati mwingi napata shida kumuelewa.
Kuwapa uwaziri wenye tuhuma na wengine walioondolewa madarakani kuwarudisha mapata shida kidogo. Sijui dharau kwa Wananchi au haamini kama wanamakosa.
Mpaka sasa Rais ameshateua watu zaidi ya wanne kuwa wabunge na kuwapa uwaziri, sasa sijui wabunge alionao kwenye ccm hawaamini au laa.
Ngoja niendelee kusubiri labda nitamuelewa.
Mwandishi Mwanahalisi.
alitaka kubalance kaskazini kwani mlilalamika sana.ila najua interest ya magufuri ni hao manaibu kwanza wapate uzoefu
hivi kitu gani alifanya huyu mama wizarani?Kwa Mama Ndalichako 100%
Lakini si amesomea mambo hayo hayo - misitu misitu,wanyama wanyama,mimea mimea nk, kwani tatizo liko wapi - kwa binadamu ambao hawana makuu na kujisikia basi Prof.Maghembe ni mmoja wapo,usikivu wake na kuheshimu binadamu wenzake kutamsaidia kufanya kazi kwa karibu na Dk.Maghufuli, hapo naona Rais amepatia sana - ila kwa Prof.Mbalawa naona ingekuwa vizuri kama angerudishwa kufundisha vyuo Vikuu - masuala ya Serikalini niliona wajanja walikuwa wanamzidi kete sana!Eti magembe amepewa maliasili!!! JPM imekuaje tena hapa umeenda chaka kabisa ....au umekosea
vijana walikua wamefaulu,yeye akaja na matokeo ya kwake,liliposanuka akarudisha matokeo halisi na ikabidi aachie ngazi,Uteuzi wa Dr Joyce Ndalichako ni uteuzi bora hasa kutokana na taaluma yake kuendana na wizara aliyopewa.
Lakini Dr.Ndalichako anachangamoto kubwa ya kuaminiwa na Jamii ya waislaam Tanzania kama atatenda haki akiwa wizarani.
Mtakumbuka kuwa akiwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani alituhumiwa na Waislaam kuwa alihusika kuwafelisha vijana wao kwa makusudi na walipofuatilia kujua kwanini wamefeli,Dr.Ndalichako alitoa matokeo mapya haraka matokeo ambayo yaliakisi madai ya waislaam.
Kwa maoni yangu ,Ndalichako atapata changamoto kubwa katika utendaji wake kutokana na Dosari iliyomkabili kipindi hicho.
Ukiachana na hilo Dr Ndalichako ni Mchapa kazi na Mtu ambae anaweza kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya Elimu.
Kila la kheri Dr Joyce Ndalichako,huu ni wakati wa kuonyesha weledi wako na uadilifu wako kwa Rais na watanzania.
Joyce Ndalichako, alikuwa katibu wa baraza la mitihani. Alishutumiwa na Waislamu kuwafelisha.
Nikiwa mwandishi wa habari za uchunguzi nililifuatilia suala hili na kulithibitisha.
Utetezi wake haukuwa na mashiko hata chembe.
Malalamiko ya Waislamu yalisababisha Rais Kikwete kumuondoa barazani.
Lakini leo hii Dk. John Pombe Magufuli amemteua kuwa Waziri wa Elimu. Tena kwanza amemteua kuwa mbunge kisha ndio kampa uwaziri.
Kuna wakati namuelewa Rais Magifuli lakini wakati mwingi napata shida kumuelewa.
Kuwapa uwaziri wenye tuhuma na wengine walioondolewa madarakani kuwarudisha mapata shida kidogo. Sijui dharau kwa Wananchi au haamini kama wanamakosa.
Mpaka sasa Rais ameshateua watu zaidi ya wanne kuwa wabunge na kuwapa uwaziri, sasa sijui wabunge alionao kwenye ccm hawaamini au laa.
Ngoja niendelee kusubiri labda nitamuelewa.
Mwandishi Mwanahalisi.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1. Profesa Jumanne Maghembe - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.
2. Dkt. Philip Mpango - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3. Mhandisi Gerson Lwenge - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
4. Dkt. Joyce Ndalichako - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5. Mheshimiwa Hamad Masauni - Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
6. Prof.Makame Mbarawa - Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015
![]()

Naona ume-mention ID yangu kulikoni?