Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Kwanza nimpongeze Raisi Dr John Magufuli kwa kuendeleza moyo wake wa upendo kwa Watanzania wote bila kujali vyama vyao,dini zao,makabila yao na jinsia zao.Niwapongeze viongozi wa vyama vya upinzania kuona na Raisi na kujadiliana mustakabali wa nchi yetu.Najua mengi mtakua mmeongea hasa la kudumisha amani.Wapo wanasiasa wachache wanatumika kuharibu amani ya nchi hii,kuichafua nchi kwenye vyombo vya kimataifa na nchi zingine,hawa watu wana pakuishi,wanapakukimbilia pale amani inapoharibika.Tuwapuuze na tufahamu mbinu zao.
 
Kuuliza si ujinga. Hivi serikali pamoja na mkuu wa nchi wapo Dodoma au Dar es Salaam? Mbona kama shughuli zote za ofisi ya rais huratibiwa Dar es Salaam?
Unauliza majibu. Tumehamia Dodoma usichoelewa nini?. Ukizidi kuuliza utakuwa unaongoza genge la wahalifu. unataka kujua shughuli zinafanyika wapi ili ufanyeje?
 
Zitto karibu huku ushuhudie wanasiasa nguli wanaojua siasa. Wenzako matatizo ya nchi wanakaa chini na kuzungumza, wewe unaenda ugenini kuzungumza halafu unajiona mwamba wa siasa. Rudi darasani ukajifunze uzalendo.
Zitto atabaki kuwa jembe daima na daima, hakuna lolote baya alilofanya kuujuisha Jamii ya kimataifa uozo wa serikali ya Meko bin Jiwe
 
Sasa Audi wa ccm ni chadema tu wale wataunga Nkomo Kz imekuwa rahisi sana kwa cdm
 
Membe hana pa kukimbilia!naona wametahadharishwa wasipokee makapi!!!Ili Membe aende CHADEMA pekee!!!na CHADEMA ITAKUFA MWAKA HUU!!!kazi kweli kweli!!labda itokee ya kongo tz!raisi atoke chama kidogo kabisa!!!
 
Zitto karibu huku ushuhudie wanasiasa nguli wanaojua siasa. Wenzako matatizo ya nchi wanakaa chini na kuzungumza, wewe unaenda ugenini kuzungumza halafu unajiona mwamba wa siasa. Rudi darasani ukajifunze uzalendo.

Wewew ni mwepesi kusahau. Hata Maalim alipodhulumiwa na Mkapa alikwenda nje. Na si mara moja tu, ni mara nyingi.

Hata hii mikutano na viongozi wa vyama vingine, ni matokeo ya safari ya nje ya Zitto. Kimsingi mbinu zote za kidemokrasia zinakubaliwa. Na zote zitatumika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…