Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Rais Magufuli amenukuliwa akisema haya..
Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa wa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi (bahati mbaya ni Mgogo); Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi hata moja ya Zika hapa Tanzania.
Baada ya uzushi wa Zika kupita na kumfukuza kazi aliyesema kuna ugonjwa huo, tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola Watalii hawatokuja, tukasema sisi hatuna Ebola wala Mjukuu au hawara yake Ebola, hatujaona Ebola wala nani amekufa kwa Ebola hapa Tanzania.
1. Rais atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dkt. Mwele Malecela
2. Dkt. Mwele Malecela aula Umoja wa Mataifa. Kuongoza vituo vya magonjwa Afrika
3. Safari itasonga Kwa msaada wa Mungu: Dr. Mwele Malecela
4. NIMR: Asilimia 45 ya watoto wachanga wakutwa na Virusi vya homa ya ZIKA Tanzania