Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

Apande tu huko watanzania hatumhitaji magonjwa ya mlipuko waziri wa afya ndie mwenye dhamana yeye akajiibukia tu na Zika yake hewa .Kuwa mtaalamu sio kuwa mwongo
Aende kuwaongopea wazungu
Kama angekuwa mwongo mwongo na msanii.. hiyo nafasi hata wazungu wangemtupa.
Asingepita hata interview.
Hakuna kazi ambazo ni ngumu kupata kama mashirika makubwa ya nje. Interview ni heavy na ni tricky sana.
Ukiona mbongo kapenya.. basi ni smart na ana deserve.
Haswa kwa hiko cheo.
And for the record tu alikuwa DG wa NIMR.
 
Je huo ushahid kuwa anatumika uliwahi patikana?
Maana naona sikuiz mtaalam yoyote asipoendena na sera za mhe.. anaitwa anatumika.
Kama kweli angekuwa anatumika.. hata hiyo nafasi ya sasa angeisikia kwenye bomba.
 
Mr. President kasema kweli. In reality hakuwa na mamlaka ya kutangaza ugonjwa husika [emoji17]
Sawa kabisa hakuwa na hayo mamlaka, si alishachukua hatua ya kumtumbua? Nini kinachomuuma sasa? Kwa vile alipata kazi?
Miaka zaidi ya mitatu bado tu yuko rohoni mwake? Huo ni udhaifu mkubwa sana, vinginevyo lipo jambo ambalo..........?
 
Acha uzwazwa,Rais alikuwa yupo kwenye muktadha wa kuelezea magonjwa ya mlipuko sasa hapo lazima aanze kwa kujenga hoja kuanzia kwenye ugonjwa wa zika.
Sasa na yeye lazima amtaje mtu,utafikiria alikuwa mke mwenzio zamani nilijua wanawake wana shida kumbe siku hizi wanawake wanaafadhali aisee karibu tutaiongiza dunia kama tutaendelea kuzaa wavulana na sio wanaume.
 
Walikuwapo huko UN akina tibaijuka lakini bado walikuja kula vijicenti vya mboga.
Chezea pesa wewe, huko aliko makato ya kodi si mchezo.
Usimfananishe dr.mwele na vitu vya ajab ajab kabisa.
Mwele is not politician.. however tibaijuka was
 
Sawa basi...si alishamfukuza kazi...akaendelea na maisha yake ya nini anarudia rudia kwani kazi kaanza kumfukuza huyo?
Hizi habari ni siasa tu.

Magufuki kashindwa kupima watu Covid-19 na kuweka mkakati wa kukinga raia, anataka kuaminisha watu kwamba hakuna Covid-19, kuna mabeberu wana nia mbaya na nchi wanatangaza kwamba kuna Covid-19, na walishawahi kujaribu kufanya hivyo kwenye Zika tukawashtukia.

Ni siasa za mfamaji hizi.

Ila kwa akiki za Watanzania wengi, atawachota vizuri tu.

Utasikia "Magufuki kiboko yao mabeberu".

Na ujinga mwingi kama huo.

Wakati hapo hapi tunawabembeleza waje kutalii, tunawabembeleza watuhisani kwenye bajeti.
 
Usimfananishe dr.mwele na vitu vya ajab ajab kabisa.
Mwele is not politician.. however tibaijuka was

Kwani yeye ana nini zaidi ya tibaijuka, ukiwa na fani kisha ukaitumia vibaya haina maana hiyo elimu yako.
 
huu utawala unadharau sana umma. wanajua umma umejaa vilaza ambao hawajui kama wao ndo wenye nchi. hiki anachozungumza kina tofauti gani na yule polisi aliyemuua Fylod
 
For the record mwele ana bosi wake. Na pia is not if kwamba anafanya kazi mwenyewe. Kuna team kubwa inayofanya kazi.
So kumlaum kisa corona.. wkt fika china walificha mpaka hali ilipowazidia.. leo hii lawama zote kwa who..china ah.. hawaonekani.
Na america ilikuwa haina nia ya kujitoa... trump alionywa na vyombo vya usalama CIA kuwa kunajanga linakuja akapuuzia.. akatanguliza siasa..
Akaja kuonywa na who japo walichelewa.. nao akapuuza... akaitwa kirusi cha kichina..
Yamekuja kumfika ..anatafuta wa kumuangushia lawama. Ameona amuangushie who.. leo america wanajuta kumchagua mshkaji. Kila anapogusa anaboronga.
 
WHO nini bna emu mtafuteni Tibaijuka na Rose mingiro ndo watawambia Hizi communities zilivo, taxes ni kubwa sana huko
Kwa hiyo kama taxes ni kubwa ndio hawalipwi au?
Mama asha rose migiro alikuwa deputy secretary of UN from 2007 to 2012.
While WHO ni shirika nje ya UN. Stil linapata funds from UNSDG.
Haijalish taxes ni kubwa . Is how they get there...
 
Si ndio hiyo ishara ya Mabeberu kutumia wajinga, wapenda Rushwa, wenye Nia ya kuuza nchi, baada ya kushindwa jaribio lao na Dau la pesa Kwa huyo mjinga wakaona ni Bora wamwajiri Wao?
Una evidence kuhusu allegation zako? Kama unazo ziweke hapa. Else ni story za kusadikika
 
Na kuna mwingine anatumiwa na Mabeberu yupo ulaya kutaka kuharibu amani ya Nchi yetu
Nchi hii haina amani kilaza wewe kuna uwoga...watu wanavunja katiba kila siku nchi ya wajanja unapinduliwa
 
Kwani yeye ana nini zaidi ya tibaijuka, ukiwa na fani kisha ukaitumia vibaya haina maana hiyo elimu yako.
Mwele na tibaijuka ni field tofauti. Mmoja ni scientist mwingine economics.
Unasema elimu yake imetumika vibaya? Once again. Mna ushahidi? Kama mnao muuweke hapa.
Na kwanini msimfungulie kesi ya uhujumu uchumi kabisa?
Kwann mnamuacha anatoka nchini hiv hiv?
 
Kwenye janga la corona tu kuhusu vipimo alikurupuka bila kutumia akiri,
Sasa huyo uanafikili yuko sawa?
Ana mapenzi na mabeberu.
 
Walimfukuza yule mama kwa kumuonea tu na Mungu amemlipa zaidi.

Moyo wa rais wetu umejaa chuki na visasi visivyo na maana.
Alimuonea kivipi? Tuthibitishie ukweli wa taarifa yake kuhusu ugonjwa wa zika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…