Rais Magufuli ameagiza Ifakara kuongezewa Kata na Halmashauri

Rais Magufuli ameagiza Ifakara kuongezewa Kata na Halmashauri

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,741
Reaction score
25,681
jpm-1.jpg

Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza Halmashauri ya mji wa Ifakara kuongezewa kata na halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kubadilishwa jina.

Ametoa maelekezo hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 na kumtaka Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo kusimamia utekelezaji.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Rais Magufuli amesema halmashauri hiyo iongezwe idadi ya kata kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na makao makuu yake yawe Ifakara.

“Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ibadilishwe jina iitwe halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na makao makuu yawe Mgeta kama ilivyoamuliwa na baraza la madiwani, ” inaeleza taarifa hiyo.

Inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi amewasisitiza viongozi wa halmashauri kutowayumbisha wananchi na watumishi kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo.

EIZjtrMXkAEY3j4.jpg
 
Kumbe waliamua madiwani ,kwann kilakitu mnasema president au kutia saini vitu vilivyopitishwa na wezake...semeni president kakubali ,sio kasema kwahyo amesema walimosema wezake
 
Sasa ishu kama hii inatija gani kwenye uchumi wa nchi?!

Ningesikia mkoa wa pwani,na Dar imeunganishwa kuwa mkoa mmoja,geita na mwanza,wilaya ya kyelwa na karagwe,ili tupunguze matumizi ingekuwa poa sana.
Hii nchi,uchumi unahudumia siasa,kila idadi ya watu ikiongezeka,wanagawanya mikoa kutengeneza mikoa,wilaya,zingine,miaka 100ijayo,TZ inaweza kuja kuwa na mikoa 50,kisa watu wameongezeka,hutakuja kusikia USA,wamegawanya jimbo kutengeneza jimbo lingine!!
 
Kumbe waliamua madiwani ,kwann kilakitu mnasema president au kutia saini vitu vilivyopitishwa na wezake...semeni president kakubali ,sio kasema kwahyo amesema walimosema wezake
Kuna upotoshwaji mkubwa sana unaofanywa na idara ya habari ya Ikulu ama kwa makusudi au kwa kujikomba.

Taarifa nyingi ambazo zinapaswa kuwa Rais kaidhinisha idara hii ya Msigwa huarifu kuwa Rais kaagiza, Rais kaamuru au Rais katoa nk.

Lugha hii si shirikishi hata kidogo inakuwa kama ni wazo binafsi la Rais!
 
Tunaboreka sana kiukweli.

Je mji wa Kidatu na Mkamba utakuwa chini ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara au itajuwa chini ya hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero/Mlimba? Ikiwa chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero basi itakuwa janga kubwa sana, kuna umbali mrefu sana hadi kufika makao Makuu ya Wilaya, takribani 180km
 
Kuna haja ya kuwa na sera ya Majimbo.

Sijui kazi ya DC..

Why Mkurugenzi wa wilaya and DAS.
 
Mkuu , Rais akisifiwa unaumia? ! Maajabu sana.
Mwigulu Nchemba alipata ajali ya kugonga punda na gari ikaumia naye akanusurika. Alipotoka hospitali alimshukuru Magufuri badala ya kusmshukuru Mungu.

Poleni Watanzania
 
Kuna upotoshwaji mkubwa sana unaofanywa na idara ya habari ya Ikulu ama kwa makusudi au kwa kujikomba.
Taarifa nyingi ambazo zinapaswa kuwa Rais kaidhinisha idara hii ya Msigwa huarifu kuwa Rais kaagiza, Rais kaamuru au Rais katoa nk.
Lugha hii si shirikishi hata kidogo inakuwa kama ni wazo binafsi la Rais!
Ileje hapo hakuna potoshaji hata km Madiwani walipendekeza, angeweza kukataa
mm naona ni shinikizo la kisiasa, kuna watu hawasikii na mara nyingi ngumi hutembezwa katika vikao vya Madiwani na wengine kuwekwa ndani akiwemo mbunge Liajuakali wa upinzani, sasa walipogwa yameisha patatawalika (divide & ..)
kumbuka Mkoa wa Mbeya kuugawa wengi walikataa Songwe
kumbuka Manyara kutoka Arusha mipaka imekaa km namba 8 watu wa Longido au Kiteto kwenda Babati ni mbali kuliko Arusha Mjini, vilio vya madiwani na wananchi havikufua dafu kipindi hicho wakitafuta mbuga za wanyama
 
Back
Top Bottom