Rais Magufuli ameshatimiza ndoto mbili za mwalimu Nyerere, kuhamia Dodoma na Stiegler's Gorge. Bado ndoto moja!

Rais Magufuli ameshatimiza ndoto mbili za mwalimu Nyerere, kuhamia Dodoma na Stiegler's Gorge. Bado ndoto moja!

kwa haya tumuombe kwa Mungu afanikishe na zaidi, Kila jambo na maksudi yake hapa duniani, arejeshe uimara wa mabenki pia

Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na ndoto zake na miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na Kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pili kumiliki njia kuu za uchumi na tatu kuwa na bwawa kubwa la kuzalisha umeme Stieglers Gorge.
Katika uongozi wake kama Rais, Dr Magufuli ameweza kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.
Pili amefanikisha ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge ambapo mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa.
Tatu, Rais Magufuli ameshaanza kuhakikisha serikali inakuwa na umiliki katika njia kuu za uchumi, amefufua ATCL, TRC inaimarishwa na taasisi nyingine za miundombinu zinaimarishwa na hii ndio ndoto ambayo Nyerere aliifanikisha lakini mabeberu wakaitibua kwa kugawana mashirika yetu karibia yote. Nina imani Rais Magufuli ataikamilisha ndoto hii ya mwalimu Nyerere.

Naomba niishie hapo!
K
 
Nimeona mradi wa Stiglers trilioni 6 kudadadeki. Halafu mradi unaisha na hakuna matokeo! Yan nahisi akaunti za watu benki itabidi zitaifishwe safari hii.
 
Yaani kipi cha kumsifia?? Yaani Mwl. Nyerere aote alafu Magufuli aje kufanyia kazi ndoto za mtu..! Moja ni kuonesha yeye hakuwahi kuwa na ndoto wala maono..!

Kinacho chekesha mpaka sasa hajawahi kutuambia anataka kuifanyia nini Tanzania. Kila akiamua anajipya bora angekuwa na jambo moja la kuifanyia nchi aliloona litaa na kudumu milele, kupambana na kila kona kuna atashutuka muda umeisha na hakuna alichofanya.
Umevaa miwani ya mbao?SGR,ununuzi wa ndege,upanuzi wa bandari na airports karibu kila makao makuu ya mkoa,flyovers tazara na ubungo ambapo mradi unaendelea nakadhalika.
 
Mwambie afukue makabrasha yote ya mwalimu, mengine apandishe kitandani halafu akiamka asubuhi nchi haina hela, anawaza kodi ya kichwa na kunyang'anya watu korosho
 
mwalimu ajawahi kuwa na ndoto izo

ndoto zake zilikuwa kumaliza ujinga, maradhi na umaskini na jpm hajafanikiwa hata robo juu ya hayo.

iyo kuhamia dodoma, kuwa na umeme yalikuwa mawazo yake ila si ndoto
Kama JPM hajafanikiwa kwenye ndoto za Mwalimu ni Rais yupi aliyefanikiwa?
 
Nimeona mradi wa Stiglers trilioni 6 kudadadeki. Halafu mradi unaisha na hakuna matokeo! Yan nahisi akaunti za watu benki itabidi zitaifishwe safari hii.
Kwa sasa wanapandisha bei ya umeme kila kukicha ili wapate pesa za kukenga bwawa jipya karibu na jiji kubwa kama DSM then watakuja baadae kutuambia wanapunguza bei kumbe waliongeza bei kwa makusudi wakati wameachana na umeme rahisi wa Upepo na makaa ya mawe.

Pia hawajatuambia kuwa uzito wa hilo bwawa litatengeneza mgandamizo mkubwa kiasi gani kwenye miamba ardhini jambo litakaloweza kusababisha tetemeko LA Mara kwa Mara kwenye jiji LA Dsm.?
 
Wewe uko mtaa gani?......... Ufipa st?
Ndo shida ya wengi kila jambo kuhusisha na Siasa,kwataarifa yako nipo hukohuko ulipo na ni jambo ambalo halihitaji utafiti,na kama ww ni bongo lala unatakiwa usiwe ndiyo mzee tumia akili yako original
 
Kama JPM hajafanikiwa kwenye ndoto za Mwalimu ni Rais yupi aliyefanikiwa?
haya mambo ya kama yanatoka wapi jpm hajafanikiwa na hata (hawezi ) fanikiwa

kifupi hakuna aliye fanikiwa
 
Mwalimu Nyerere alikuwa mwanaharakati wa kugombania uhuru, na wengi wa wanaharakati wa kugombea uhuru walikuwa si watawala bora, kwani fikra zao zilikuwa kutafuta uhuru lakini walikuwa hawajui nini wafanye baada ya uhuru, na ndoto za mwalimu nyingi aliziota baada ya kulala katika usingizi wa ukomonisti, ndiyo maana alishindwa kuzitekeleza, sasa nchi imebadilisha muelekeo. Baada ya utawala wa viongozi 4, leo hii mnataka kuturudisha nyuma katika siasa za ujamaa na kujitegemea? Ina maana viongozi wote waliopita baada ya mwalimu walikuwa hawajui ndoto za baba wa taifa?
 
Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na ndoto zake na miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na Kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pili kumiliki njia kuu za uchumi na tatu kuwa na bwawa kubwa la kuzalisha umeme Stieglers Gorge.
Katika uongozi wake kama Rais, Dr Magufuli ameweza kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.
Pili amefanikisha ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge ambapo mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa.
Tatu, Rais Magufuli ameshaanza kuhakikisha serikali inakuwa na umiliki katika njia kuu za uchumi, amefufua ATCL, TRC inaimarishwa na taasisi nyingine za miundombinu zinaimarishwa na hii ndio ndoto ambayo Nyerere aliifanikisha lakini mabeberu wakaitibua kwa kugawana mashirika yetu karibia yote. Nina imani Rais Magufuli ataikamilisha ndoto hii ya mwalimu Nyerere.

Naomba niishie hapo!

Badilisha Avatar yako maana hata hufanani na Yohana Mbatazaji. Uu muongo kama nini? Amefanikisha lini? Ndio kwanza anaanza mchakato.
 
Ujinga,maradhi na umaskini ongeza na rushwa. Kuhamia Dodoma hakuna faida kwa Watanzania.
 
Hiyo iliyobaki ilikuwa nzuri kwa wakati ule, kwa sasa mifumo ya kiuchumi duniani inakataa
Sidhani kama inakataa....We need to refine it to meet the modern challenges.
Let's be thinkers and not followers of everything from the west
 
Back
Top Bottom