Rais Magufuli ameshatimiza ndoto mbili za mwalimu Nyerere, kuhamia Dodoma na Stiegler's Gorge. Bado ndoto moja!

Rais Magufuli ameshatimiza ndoto mbili za mwalimu Nyerere, kuhamia Dodoma na Stiegler's Gorge. Bado ndoto moja!

Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na ndoto zake na miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na Kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pili kumiliki njia kuu za uchumi na tatu kuwa na bwawa kubwa la kuzalisha umeme Stieglers Gorge.
Katika uongozi wake kama Rais, Dr Magufuli ameweza kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.
Pili amefanikisha ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge ambapo mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa.
Tatu, Rais Magufuli ameshaanza kuhakikisha serikali inakuwa na umiliki katika njia kuu za uchumi, amefufua ATCL, TRC inaimarishwa na taasisi nyingine za miundombinu zinaimarishwa na hii ndio ndoto ambayo Nyerere aliifanikisha lakini mabeberu wakaitibua kwa kugawana mashirika yetu karibia yote. Nina imani Rais Magufuli ataikamilisha ndoto hii ya mwalimu Nyerere.

Naomba niishie hapo!
Subiri na uchumi wa kuvaa viraka tulio na ukumbuka viatu tuliviona dukani wakati wa mwinyi
 
Makao Makuu ya nchi kuwa Dar yalisababisha umaskini kwa wananchi?

Yalisababisha madarasa kuwa pungufu??
Yalisababisha maji kutopatikana vijijini??
Yalisababisha ajira kwa vijana kuwa shida??

Tupimwe akili!! Si bure mleta mada una makengeza ya kiufahamu
 
Mbwiga nazungumzia kuhamia Dodoma uwe unaelewa!.....hayo ya umasikini sijui maji mara ajira yafungulie uzi tukutane huko!
 
Yaani kipi cha kumsifia?? Yaani Mwl. Nyerere aote alafu Magufuli aje kufanyia kazi ndoto za mtu..! Moja ni kuonesha yeye hakuwahi kuwa na ndoto wala maono..!

Kinacho chekesha mpaka sasa hajawahi kutuambia anataka kuifanyia nini Tanzania. Kila akiamua anajipya bora angekuwa na jambo moja la kuifanyia nchi aliloona litaa na kudumu milele, kupambana na kila kona kuna atashutuka muda umeisha na hakuna alichofanya.

Jamani jamani !! , hakuna alichofanya.
 
mwalimu ajawahi kuwa na ndoto izo

ndoto zake zilikuwa kumaliza ujinga, maradhi na umaskini na jpm hajafanikiwa hata robo juu ya hayo.

iyo kuhamia dodoma, kuwa na umeme yalikuwa mawazo yake ila si ndoto
Asante...
 
Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na ndoto zake na miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na Kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pili kumiliki njia kuu za uchumi na tatu kuwa na bwawa kubwa la kuzalisha umeme Stieglers Gorge.
Katika uongozi wake kama Rais, Dr Magufuli ameweza kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.
Pili amefanikisha ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge ambapo mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa.
Tatu, Rais Magufuli ameshaanza kuhakikisha serikali inakuwa na umiliki katika njia kuu za uchumi, amefufua ATCL, TRC inaimarishwa na taasisi nyingine za miundombinu zinaimarishwa na hii ndio ndoto ambayo Nyerere aliifanikisha lakini mabeberu wakaitibua kwa kugawana mashirika yetu karibia yote. Nina imani Rais Magufuli ataikamilisha ndoto hii ya mwalimu Nyerere.

Naomba niishie hapo!

Ni kweli tupu ila katika kugawana mashirika hakuna cha beberu wala nini bali ni haohao.
 
Atatimiza ndoto ya nyerere yankukaa madarakani miaka 25
 
Lini kahamia inawezekana mimi niko nyuma ya wakati.
Quinine, the pont is: Nyerere alitaka kuhamia Dodoma kwa vile eti iko katikati ya nchi; hivyo kurahisisha safari ya kwenda mbali kufuata huduma za kiserikali DSM. This concept is outdated! Huko nyuma kwa mfano kutoka BKB kwenda DSM ulikuwa unatumia siku 4. Leo ni siku moja, with private driving unatumia hardly a day! Pia alisema usalama wa nchi unakuwa imara ukiwa mbali na coastal area kwa vile zamani uvamizi ulianzia maadui kutumia bahari kuvamia nchi. Sasa hivi unaweza kushambulia tanzania kutokea Pentagon, huhitaji kuja pwani ya Tanzania! To me hakuna haja ya kuharibu hela kuhamia Dodoma! Siku hizi hakuna kupeleka barua tena kwenda dar kwa posta (kama zipo ni chache), hivyo eti barua itatumia siku 10 kufika ofisi say , ya ardhi dar imepitwa na wakati! With modern telecomunications technology, you do not need to move to DDM to get a timely information delivered! fax, emails etc
 
1.Bomba la mafuta Uganda, kama litajengwa
2. Bwawa la umeme, Rufuji
3. SGR
4. Dodoma
5. Bagamoyo

Kama miradi yote hii itakamilika ndani ya muda iliyopangwa iwe imekamilika, itastaajabisha sana kama uchumi wetu hautakuwa umechangiwa kiasi cha kutosha ili uweze kuendelea kwa kasi nyingine kuliko ulivyo sasa.

Naona na kusikia miradi ikiwekwa saini za ujenzi; lakini sisikii ni wapi hela za ujenzi huu zilipo. Nadhani kuna sehemu ndani ya nchi hii kuna mahela yamechimbiwa chini au yapo kwenye magodoro ya Ikulu ya Magogoni!
 
Back
Top Bottom