Rais Magufuli ametukanwa tena na Jarida la Economist. Tukiendelea kunyamaza, itafika siku Uongo huu utageuka Ukweli!

Rais Magufuli ametukanwa tena na Jarida la Economist. Tukiendelea kunyamaza, itafika siku Uongo huu utageuka Ukweli!

Rais hana muda wa kuwajibu hao The Economist wanaoandika siasa badala ya uchumi.

Magufuli ana kazi moja tu ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais amezindua SGR kwao sio habari!
 
huwa hilo jarida haliandikwi kwaajili ya watanzania. ni kwaajili ya wawekezaji na wahisani/donors. na huwa hawapuuzi hizo ishu. ishaurini serikali ijisafishe kwa matendo. ikishindwa basi kwa maneno. si picha nzuri inajijengea kimataifa.
Waambie hao donors wakate misaada!
 
umesema kanuni namba moja ya mwandishi wa habari ni kusema ukweli. naamini this applies kwa wanahabari wote dunia nzima. sasa je kwa nini wenzako wakiandika kwa msingi wa kanuni hiyohiyo unawaita waongo?
Issue hapa ni acacia, kuzuiwa rasilmali
 
Samahani mkuuu mayala naombaa uniambiee katikaa kutafsiri umetumiaa tafsiri gani???

Manake ninachokiona umetafsiri kama wale wanaotafsiri mikanda ya video i mean series za kibongo kwa sababu ulivyosoma ww na kuelewa ndivyo ulivyo tafsiri while mambo mengine hayakutakiwa kutafsiri hivyo tena ulivyo tafsiri kiswahili ndo umekoseaa kwa sababu umebadilisha maneno ambayo ukisoma kilichoandikwa na ulicho tafsiri ni tofauti! Zaidi umetupa idea ya kiliichoandikwa
 
PASCO, usiingie kuchimbia kichwa chako kwenye mchanga na kutosikiliza criticism , nyingine ambazo ni za ukweli kabisa.

Ukweli unaufanyia kazi, uongo unaacha.

Lakini hata Magufuli ameanza kutambua kuwa mambo mengine hayaendi sawa kwenye kodi.
TRA are literally terrorising business in the country.

Wafanya biashara wakubwa na wadogo wanatozwa kodi hata zaidi ya mitaji yao ya biashara.
Wengi sana wamefunga biashara, PASCO tafuteni tu hizo data.
Juzi Magufuli kaliongelea hilo, hata yeye aneona kuna mahali kateleza.
 
Sijaona tusi apo ila ni sifa za mkuu wetu,
pengine kuna vitu hawajakazia vizuri, kiongozi ukishindwa kuongozwa na busara io ni rogue, kama huamini fuatilia kwa anayoropoka katika hotuba ndipo utaamini ni rogue
 
pascal mayala huna uwezo mdogo sana wa kufikiria kuliko hata ukubwa wa jina lako hapo katika io makala hakuna tusi lolote bali malalamiko ya watanzania wenyewe ndo yanafanya majalida ya nje zijue hali ya tanzania ikoje na matukio pia yanayoendelea tanzania raisi wetu anafanya mambo kama hana washauri yaani anaongoza nchi ya watu milioni 55 kama anaongoza familia yake AIBU sana hii.

Yaani Tanzania inafikia sehemu mwandishi wa habari anakimbilia ughaibuni kuomba hifadhi akiogopa akibaki Tanzania atauliwa yaani ile AMANI na UPENDO tuliokuwa tunahubiriwa imeenda wapi ?

SHAME ON YOU PASCAL MAYALA (kisukuma mayala maana yake njaa)
 
Hivi Mayalla Unawinda uteuzi au. Hivi lipi ambalo sio kweli kwenye article hiyo? Labda utaaramu na mpangilio wa kizungu. Mda ni tatizo ningeweza kuitafsiri kwa lugha yetu pendwa kiswahili ili watu wang'amue wapi tumetusiwa.

ANGALIA NUKUU "It is a lesson on how weak institutions can be hijacked" Bunge,polisi,mahakama na PCCB all are weak institutions. Afrika Kusini rais anaweza kushitakiwa na polis na AG (rejea mashitaka yaliyopelekea zuma kurejesha hela serikalini za kasili yake) Israel waziri mkuu anashitakiwa na AG na polisi.

Hizo ndo strong institutions which can not be hijacked. Kaka huo ndo ukweli.vzr waambiwe wajue. Tanzania ya leo haina MAZUZU
 
Back
Top Bottom