Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

Aidha Bwana SUGU amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuhakikishia hilo na kujenga imani kwa wawekezaji wengine.

Mhhhhhhh MACHALE KUNDESA!!!

SUGU TAYARI IMEIASHA HIYO SOON Atajoin na kina GAUCHO MINJINO,SILINDE,LIJUALIBUTU.
 
Watanzania wengi wamefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli ya kusimamisha nia ovu waliyokuwa nayo watendaji wa serikali ya kutaka kubomoa hoteli maarufu ya aliyekuwa mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Sugu.

Kwa bahati nzuri huyo Sugu ameeleza kuwa hoteli yake hiyo ilikuwa na vibali vyote vya mamlaka zinazohusika za kukamilisha ujenzi huo.

Swali linakuja hao watendaji waliotaka kuibomoa hotel I hiyo, walipata wapi kiburi hicho cha kutaka kuibomoa hoteli hiyo, wakati wakijua fika kuwa mwekezaji huyo ana vibali vyote vya mamlaka husika?

Kama hao watendaji hawajapata kiburi hicho kwenye mamlaka za juu za nchi, basi tunategemea hao watendaji waliokuwa na nia hiyo ovu watumbuliwe mara moja.

Kinyume cha hapo tutakuwa tunajenga nchi ambayo baadhi ya watendaji wanaweza kujiamulia mambo yao kwa lengo la visasi tu kwa ajili yakuwakomoa baadhi ya wananchi.

Kama kweli Rais Magufuli ameitoa hiyo kauli bila unafiki wowote, basi tunamtegemea awatumbue haraka hao watendaji wa serikali waliotaka kuibomoa hiyo hoteli, kinyume cha taratibu kwa lengo tu la kutaka kumkomoa Bwana Sugu.

Kwa kuwa sisi wananchi tunamjua Rais wetu kuwa ni mtu asiyetaka masihara hata kidogo na ni mwepesi sana wa kuwatumbua watendaji wake hata kwa "vijikosa" vidogo, basi tunatarajia kwa hawa watendaji wake ambao walitaka kubomoa hiyo Hoteli ya mamiloni ya shilingi za mwwkezaji mzawa wa kitanzania, ambaye amefiata taratibu zote za uwekezaji, basi tunatarajia atawatimbua mara moja ili kuondoa fikra za wananchi wengi kuwa huyo Sugu alitaka kukomolewa kwa kuwa ni kiongozi wa Chadema, hasa tukitilia maanani usemi maarufu wa Rais wetu Magufuli kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA
 
Hao watendaji walifanya hivyo kama njia ya kujipendekeza kumfurahisha bosi wao kwasababu wanaijua tabia yake, kwani walivyovunja Billicanas au kuharibu mashamba ya Mbowe kule Hai walifuata sheria gani?

Club Billicanas ilivunjwa licha ya zuio la mahakama lililokuwepo, kutokufuata sheria ndio imekuwa tabia kuu ya utawala uliopo, halafu chakushangaza, wanatokea watu na kusifia hatua hiyo ya Magufuli kuzuia hoteli isivunjwe, lakini hawajiulizi kwanini hoteli ivunjwe wakati ujenzi wake ulifuata sheria na taratibu zote?

Kwa mtindo huu tutaendelea kuchezewa akili sana na kuishia kushangilia kama mazuzu, pia wengi wataendelea kuumizwa kwa matendo ya kidhalimu watayofanyiwa kwa maamuzi ya wachache wasio na huruma na watanzania wenzao, na wasiofuata sheria za nchi.
 
Hao watendaji walifanya hivyo kama njia ya kujipendekeza kumfurahisha bosi wao kwasababu wanaijua tabia yake, kwani walivyovunja Billicanas au kuharibu mashamba ya Mbowe kule Hai walifuata sheria gani?
Wanga tu Wale. Walikuwa wanamchafua JPM...sasa anawaruka kimanga.

Wengine waiorukwa kimanga ni Wale wauaji wa Alphonse Mawazo. Wakati ni mahakama ya ukweli hata watesi waliomshambulia Lissu nao pia watalipwa hapa hapa Duniani. Acha tuwe na subra.
 
Hao watendaji walifanya hivyo kama njia ya kujipendekeza kumfurahisha bosi wao kwasababu wanaijua tabia yake, kwani walivyovunja Billicanas au kuharibu mashamba ya Mbowe kule Hai walifuata sheria gani?
Hao watendaji walifanya hivyo kama njia ya kujipendekeza kumfurahisha bosi wao kwasababu wanaijua tabia yake, kwani walivyovunja Billicanas au kuharibu mashamba ya Mbowe kule Hai walifuata sheria gani?
Ndiyo maana ninasema kama Rais Magufuli anataka kujitoa katika suala hilo inabidi awafukuze kazi Mara moja watendaji wake hao ambao wanafanya kazi kwa ajili ya kuwakomoa wananchi........

Kinyume cha hapo tutajua kuwa ubomoaji huo, ulikuwa na " all blessings" zake
 
Hatua ya Rais kumtetea mwekezaji Mzawa bw Sugu bila kujali itikadi ni ya kupongezwa na kwa hilo ameumaliza mwaka vizuri kwa kuwawezesha wawekezaji wazawa kujiamini. Huu ni Mwanzo mzuri kwa sekta binafsi kujenga uhusiano mzuri na serikali na hii tafsiri yake kila mtendaji atapaswa abadiri fikra. Sasa kumekucha kila mtu ajipange kuwekeza ili mradi afuate sheria za nchi. Na ndiyo maana kwa sasa TIC iko ofisi ya Rais chini yake.Bravo Rais Mpendwa!
 
Sugu siyo mkorofi kwa serikali na kodi analipa!
 
Mhe rais baadhi ya qaku wa mikoa ni wakurupukaji. Ni majip .. wana under perform. Tale them out.kulikuwa hakuna haja ya chalamila kutengenexa ugomvi na kuraka kubomoa hotel half rais alipotoa tamko kaja upande wa rais.
Aache unafki.. hila hazinengi taifa
 
Watendaji waliobomoa jengo la Tanesco ubungo wamechukuliwa hatua gani ?
 
Ili asionekane mnafiki, anapaswa aende hatua moja mbele, kwa kuwatumbua wale wote waliohusika na kupanga njama hizo ovu za kutaka kumbomolea mwekezaji huyo mzawa, kwa visa tu na kutaka kumkomoa
 
Create a fictitious problem and then solve it. Team P & W will do the rest
 
Wanga tu Wale. Walikuwa wanamchafua JPM...sasa anawaruka kimanga.

Wengine waiorukwa kimanga ni Wale wauaji wa Alphonse Mawazo. Wakati ni mahakama ya ukweli hata watesi waliomshambulia Lissu nao pia watalipwa hapa hapa Duniani. Acha tuwe na subra.
Wale waliotekekeleza mpango huo muovu, kwa maagizo toka juu, ndiyo wajifunze kuwa "Za kuambiwa changanya na za kwako"

Na ule msemo mwingine unaosema mwisho wa ubaya aibu!
 
Sugu siyo mkorofi kwa serikali na kodi analipa!
Ukorofi maana yake nini? tatizo lenu mnataka kusifiwa nchi nzima, asitokee mtu mwenye mawazo tofauti kwenu anageuka adui, na kwasababu bahati mbaya mna mamlaka, basi mnayatumia mamlaka yenu vibaya kumuadhibu bila kufuata sheria, hii ni mbaya sana.
 
Chadema watasema hii imeundwa mtandaoni,sugu hawezi kushukuru
 
Siyo unampa sifa Rais Magufuli, bila kutafakari hiki kiburi cha kufanya madudu yote hayo anakipata wapi huyo RC Chalamila?

Kama kiburi hicho hakijatoka kwake Mheshimiwa Rais, basi tutegemee awatumbue hao akina Chalamila haraka sana!
 
Watendaji waliobomoa jengo la Tanesco ubungo wamechukuliwa hatua gani ?
Hii issue inanifanya niwaze mbali kidogo, inawezeka mpango wa kuibomoa hiyo hoteli ulikuwa wa siri, bahati nzuri kwetu siri ilipofichuka wakaona mpango wao umeshaharibika, ndio wakaja na hili tamko la Rais kuzuia uvunjwaji, hapa swali linakuja hao waliotaka kuvunja ni walevi au vichaa? kwanini wafikirie kuvunja sehemu ambayo haina tatizo kisheria?!

Nadharia hii inachangiwa zaidi na yale yaliyomtokea Mbowe chini ya utawala huu, mali zake nyingi zimeharibiwa bila sababu zozote za msingi.
 
Sugu nae anatengenezewa mazingira ya ...??
 
Anzisha tatizo halafu litatue uonekane una huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…