Rais Magufuli amtuma RC wa Mbeya kusitisha uvunjaji wa Hotel Desderia inayomilikiwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kisingizio cha mazingira

That is right.

Hao waliotaka kuvunja hoteli hiyo, wanapaswa wafukuzwe kazi Mara moja
 

Kufananisha Club Bilicanas na hotel ya Sugu sio sahihi. Mbowe pale club Billicanas alikuwa mpangaji wa nyumba ya serikali[ National Housing] na alikuwa na deni kubwa la kodi ambayo alikuwa anadaiwa!! NHC walisema kama walivyokuwa wanavunja sehemu nyingine, walitaka kiwanja chao ili wajenge Nyumba nyingine kama kitega uchumi!!!

Sugu hii ilikuwa hotel yake!!!
 
Baadhi ya majengo ya hotel ya Desderia yamejengwa ndani ya mita 60 kutoka mtoni. Sheria za mazingira zinakataza ujenzi ndan ya mita hizo. Wataalam wetu watoa vibali ni wala rushwa wazoefu na watu wa kutumwa na waheshimiwa. Walitoa vibali kimakosa.

Msijeshangaa akija rais mwingine ikabomolewa na Sugu kulipwa fidia. Rais ametumia busara. Sugu alichemka kujenga pale wakat akijua ni mwanasiasa wa upinzan hivyo uwekezaji wake unaweza kutumika kumuumiza. Tukumbuke fujo alizofanyiwa mbowe na DC wa hai.
 
Tujiulize je kuna wengine waliovunjiwa kama Mbowe, pamoja na kuwa walikuwa wapangaji wa NHC?

Kama jibu lilikuwa kavunjiwa Mbowe peke yake, inadhibitisha kuwa nchi hii ina "double standards" ya hali ya juu linapokuja suala la utekelezaji wa sheria za nchi hii, wakati huo huo Rais wetu haishi kusema kuwa Maendeleo hayana Chama!
 
kule tu kwenye shamba lake moshi wengine baadae mikoa mingine waliruhusiwa kulima "karibu na vyanzo vya maji"ila yeye aliharibiwa shamba kwa mbwembwe...KAMA SHERIA KWELI SUGU KAVUNJA AVUNJIWE HOTELI,KAMA WATU WALIKUWA WANATAKA KUMUONEA SABABU YA KISIASA KAMA ALIVYOSEMA MKUU WA MKOA SUALA DOGO LINAINGILIWA NA RASI WA NCHI NI AIBU,WAHUSIKA WATAJWE MAJINA WAFUKUZWE,NDIYO MAANA WAWEKEZAJI WANAOGOPA HATA WATU WANAOGOPA KUWEKA HELA BENKI KUMBE MAAMUZI YA WATU WANAJIFANYIA WATAKAVYO SIVYO?
 
Sifa za MaCCM mara nyingi ni kero! Mtu anatengeneza tatizo yeye mwenyewe na kulitatua yeye mwenyewe! Halafu MaCCM munaingia nusu uchi mitaania kucheza Ngoma ya Kigodoro?
 
Kwa hiyo hao watoa vibari mliwaruhusu kupokea rushwa kwa Sungu? Kwa nini hamjawafungulia Kesi ya kula rushwa na kuhujumu wa mazingira? Lakini hapa naona mnahangaika na majengo ambayo yaliruhusiwa kujengwa kwa mjibu wa taratibu za malaka zinazooruhusu ujenzi kuwa halali hapa nchini Tanzania? Kama ujenzi wa hoteli ya Sungu haukua halali tungempongeza Rais, kama tungesikia kuwa ametoa malipo ya fidia kwa Sungu ili ajenge hoteli yake mahali halali kwa mazingira na ujenzi. Ajabu hapa ni vichwa vya habari vya mapambio ya magazeti ya kesho, kumsifia doctor aliyempa mgonjwa Panadol kutuliza maumivu ya jipu kwamba amehurumia wakati alijua tiba halisi ya jipu Ni kupasua tu.
 
Wakat mwingine mtu unakata tamaa ya kuchangia mijadala hapa jukwaan sababu akili fupi za hapa jukwaani zinaona mambo kwa ushabiki wa vyama au unazi wa kidini na ukanda/ukabila
 
Nyie makamanda uchwara hebu tulieni.
Sina ukamanda wowote ,Ila hii tabia ya mwenyekiti wetu kuanzisha tatizo then kulitatua limeshajulikana haina haja ya kuyarudia matukio haya.tudesign namna ingine.si unaona hata ya DED wa Geita wanatuponda!hili si juzi tu tunarudia show hizohizo.
 
Kwanza hata hivyo kulikuwa na ulazima gani wa kurekodiana wanasema ooh Mhe. Kanituma nije ooh kasema Hotel yako isibomolewe.

Kibwengo anaforce sana kuonekana mwema mbele ya jamii wakati kila mtu ashamjua yeye ndio anajua yaliko makaburi ya kina Ben Saanane ,Azory Gwanda, Kanguye.

Haya maigizo yafike mwisho tu
 

Wasifiaji wote wamejaza Kamasi bongo zao
 
Hiyo ni "Agenda setting" kuuhadaa ulimwengu ili ionekane rais ana nia njema. Ilipangwa hivyo Kwa makusudi kabisa !!
 
Siasa ni game,ukute mzee ndio aliruhusu jamaa wafanye hivyo huku akijua kuwa baadaye atawazuia ili kujitengenezea umaarufu wa kupendwa na wananchi.Siasa inadeal Sana na kucheza na akili za Watu.
 
Ah!!wapi sio kweli, angekuwa mbunge kwa tiketi ya CCM hapo sawa.
 
Wakati Rais Magufuli akiwa ziarani Mbeya mwaka jana Sugu alipanda kwenye gari ya mh Rais na kupewa kipaza sauti kisha akawatangazia wana Mbeya kwamba anamuunga mkono Rais Magufuli kwa 100%

Sitashangaa kumuona Sugu CCM!

Kaenda Slaa ccm lakini bado ccm inategemea kura za kwenye mabeg na maagizo haramu ya Magufuli, ndio itakuwa Sugu? Hata Mbowe akienda ccm, bado ccm haitapata mvuto, itabidi iendelee kutegemea nguvu za dola kupata uungwaji mkono.
 
Alikuwa anadaiwa shillingi ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…