Rais Magufuli anapenda kuona watanzania wakiumia?

Rais Magufuli anapenda kuona watanzania wakiumia?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,718
Reaction score
58,893
Wakulima wa nchi hii wanauza Mahindi, Mchele, Karanga, Machungwa kwa wingi katika miji ya Mombasa na Nairobi yaani wanategemea soko kwa 60%.

Wafanyabiashara wa ng'ombe wa Tanzania ndi wanalisha nairobi na kenya nyama na wanategemea kipato kutoka Kenya.

Tunauza mbao kwa wingi nchini Kenya, Kenya imewekeza karibia 2trion na nchini na inatoa ajira kiasi kwa Watanzania Mfano KCB, na mabenki kibao ni uwekezaji wao.

Kwanza mimi siwashangai Magufuli na Uhuru nawashangaa Watanzania wapumbavu wanaoshangilia mgogoro huu wakati wanajuwa kabisa mwisho wa siku watakao teseka ni wakulima wafugaji na wawekezaji wa Tanzania.

Kuna mambo mengine ya kujitakia na wala hayana msingi wowote kwa watu wetu leo watanzania wamesahau ya Kukamatwa kwa manji na Mbaazi?

Mgogoro wa Dangote na kupunguza wafanyakazi? Mgogoro wa Korosho mpaka leo wengine hawajalipwa?

Halafu tunategemea eti serikali wataumia Kwa kufungwa mpaka wa Kenya?

Kuna watu wamezoea kuona wanzao wakiteseka kama Rais Magufuli Tuendelee kusubiri mlejesho.
 
Aliyeamua kufunga mpaka mwanzo na kusababisha usumbufu mkubwa ni Dr Magufuli kwa akili yako?
Naamini wewe siyo mtanzania. Watanzania tunafahamu jinsi ambavyo tumeongozwa kupita kwenye janga la corona bila usumbufu. Huko kwa majirani tumeona wenzetu vurugu mitaani, na moshi mkubwa ukitanda hewani. Sisi hapa kazi tu.
 
Lockdown huwa haizuii mizigo bali ni watu
Inaonekana umeota usiku kucha, ila si agenda ilikuwa kufunga mipaka na mkasema uhai ni muhimu zaidi kuliko uchumi, What happened?

Sent using Jamii Forums mobile app
Una ubongo mdogo sana ndugu yangu. Hata nchi walizo lockdown ndege za mizigo ziliendelea kutua kama kawaida kwa ajili ya bidhaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wapumbavu wanaoshangilia mgogoro huu wakati wanajuwa kabisa mwisho wa siku watakao teseka ni wakulima wafugaji na wawekezaji wa Tanzania
We waache ajira zipukutike na njaa ikishaingia ufahamu ndio unarejea ili watu waende kwenye box la kura na ghadhabu

Naongea kwa uchungu sana
 
60% ya matunda yanaliwa Mombasa? labda ya kimasihara!


soko la ndani linatisheleza.

McHale kwa sasa 1000, kwa kilo.

tunahitaji watalii tuongeze forex
 
Aliyeamua kufunga mpaka mwanzo na kusababisha usumbufu mkubwa ni Dr Magufuli kwa akili yako?
Naamini wewe siyo mtanzania. Watanzania tunafahamu jinsi ambavyo tumeongozwa kupita kwenye janga la corona bila usumbufu. Huko kwa majirani tumeona wenzetu vurugu mitaani, na moshi mkubwa ukitanda hewani. Sisi hapa kazi tu.
Speak for yourself ,wewe siyo msemaji wa watanzania. Akili za ajabu kweli- unbelievable.
 
Sisi wakenya wa Tanzania tulifurahi sana watanzania kufungiwa mpaka, lakini sasa tunashangaa kwanini watanzania wametuiga.

Halafu tulifunga mpaka sijajua watanzania wanaingiaje Kenya mpaka wanapimwa na kukutwa wameleta ugonjwa.

Watanzania wa pvyp sana na watakufa njaa mwaka huu maana sisi wakenya ni wa kimataifa na nchi zote za Africa masharili tumeungana tykawatenga watanzania
 
Kumbe wewe ni mkenya? Sasa mmelikoroga endeleeni kulinywa! Madreva wetu wanavyonyanyaswa na wakenya mipakani hamuoni eeh??!! Na bado!
 
We waache ajira zipukutike na njaa ikishaingia ufahamu ndio unarejea ili watu waende kwenye box la kura na ghadhabu

Naongea kwa uchungu sana
Tunataka tujue nani bingwa kati ya watz na nyinyi wakenya!
 
Kwenye suala la biashara kati ya Kenya na Tanzania, kuna siasa na hujuma Serikali ya Kenya inatufanyia. Haiwezekani Watanzania wenzetu ambao ni Madereva wa Malori wanyanyaswe kwa kisingizio cha Corona, huku Madereva wa Malori hayo hayo kutoka Kenya, wakioneshwa ukarimu!

Kupitia mchezo huu wa "wewe mwaga ugali halafu mimi nimwage mboga" utawaamsha viongozi wetu kama ilivyotokea mpaka wa Tanzania na Zambia kule Tunduma, na mpaka wa Tanzania na Rwanda kule Rusumo, kukaa chini na hivyo kuzimaliza tofauti zao.

Hivyo mtoa mada usiwe na hofu! Hili suala ni la muda tu na hivyo litamalizwa kidiplomasia kati ya pande mbili. Halitakuwa ni tatizo la kudumu.
 
Back
Top Bottom