Rais Magufuli anarudisha uchifu? Kanisani na msikitini tumekuwa tukiambiwa hao ni wapagani

Rais Magufuli anarudisha uchifu? Kanisani na msikitini tumekuwa tukiambiwa hao ni wapagani

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Jana Mh. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa mkoani Morogoro katika uzinduzi wa soko kuu la kisasa la mkoa alipitisha na kulipa jina la soko hilo kuwa Chifu Kingalu Mwanabanzi. Huyu ni chifu wa kabila la Waluguru wa mkoa huo ambao sisi watoto na watu wa kanisa tumeambiwa kuwa walikuwa wapagani.

Kusema ukweli wazungu walipofika Afrika na Tanganyika na kuleta dini za kigeni walisema kila kitu chetu ni cha kishenzi kuanzia mfumo wetu wa siasa, ngoma, chakula hata lugha zetu na vitu vyote kuwa ni vya kishenzi.

Baada ya kusoma historia nimeona mambo ya ajabu sana, kwani wazee wetu walikuwa wanamwona Mungu na Mungu akujificha kama hivi sasa. Na hizi Chifudomu ndiyo zilikuwa sambamba kulinda na kutukuza zile ibada. Kwa mfano wazee wetu waliomba mvua na zilinyesha, viwavijeshi na nzige waliposhambulia mazao yao walimgeukia Mungu na siku hiyo hiyo waliwaona wadudu wamekufa kifo cha mende.

Ndoa ilianza mwanzo hadi mwisho tofauti na sasa kati ya ndoa 10 ni 2 tu ndiyo inasemekana zinavuka kwa mbinde wakati mchungaji anasema wazi kilichounganishwa na Mungu mwanadamu hawezi, hawezi kukitenganisha lakini tunaona wenyewe.

Lakini leo kwanini Mungu aonekani kama zamani kupitia Kanisani na Msikitini na baadala yake tuna soma historia tu kuwa fulani alifanya hivi na vile. Namwona kama Magufuli anataka kuturudisha katika Mungu wa babu zetu, na kama akifanya hivyo hakika yule Mungu wa Babu zetu alikuwa anaonekana tofauti na huyu Mungu wa kisasa.

Angalia Baba wa taifa aliua chifudom na yote aliyo yaanzisha kama viwanda, elimu bure vilikufa huku akiwa anaona kwa macho yake hakika kama Magu analijua hili hasione haya afanye kweli Mungu wetu wa babu na bibi zetu aturudie na kutusaidia hali imekuwa mbaya sana.

Kwa tendo la kuenzi uchifu na kulipa jina soko kuu la Morogoro jina la chifu hii ina maana Mizimu ya kiluguru itafurai na neema itaanza kuonekama na Rais alimuulizia chifu kama yupo na amesema atalala Morogoro kwenye Uchifu ili ajue vitu.
 
Ni jina tu na halina mnasaba na imani. Nakumbuka kule Mzumbe chuo kuna bweni linaitwa Kunambi. Nadhhani ni jina la Kiluguru.
 
Ni vyema maana kuna wale wanaotaka kuona majina ya kithungu sijui wana maoni gani!
 
Hata wazungu, waarabu, wahindi, wachina...... wana mizimu ya kwao. Kuitwa Kingalu au Ali au James ni kitu kingine; na imani ni kitu kingine
 
Kwa hiyo mtoa mada, ungependa tufanye nini?[emoji56]
 
Soko jipya la Dodoma
Jina Ndugai lipo kwenye Bibilia gani?
 
Serikali haina dini!
Acha huo ujinga kijana hata wana wa Israel walipomwacha Mungu wajikuta wapo utumwani yaani ardhi yao waliilipia kodi kwa rais wa taifa lingine, na walipo mrudia Mungu wao walipewa Kaanani yao tena, na msingi wa kumjua mungu umeandikwa sana katika Biblia, pia tena katika agano la kale Mungu anatambulika kuwa ni Mungu wa baba zenu na ardhi yenu kuwa makini Mungu aokotwi kutoka katika dini za kigeni.
 
Kulipa soko la Morogoro jina la chifu wa zamani hakuna maana ya kurudisha uchifu. Ni kumuenzi tu huyo chifu kwa mazuri aliyofanya. Nyerere alipoua uchifu mwaka 1963, pamoja na kwamba yeye alikuwa wa ukoo wa uchifu, bado alienzi machifu kadhaa kwa mazuri waliyoyafanya. Kwa mfano shule ya St. Mary's Tabora ilibadilishwa jina kuwa Milambo, ambaye alikuwa chifu wa hapo. Vilevile uko Iringa shule ya Southern Highlands ikaitwa Mkwawa, ambaye alikuwa chifu huko.

Huko kulikuwa kuwaenzi tu hao machifu kwa mchango wao katika kupigana na mkoloni. Siyo kuashiria uzuri wa uchifu. Zaidi ya hayo haimaanishi cho chote kuhusu imani ya dini. Nyerere alikuwa Mkatoliki thabiti. Asingeweza kubadili jina la St Mary's kuwa Milambo kama kungekuwepo hapo suala la imani. Vivo hivyo kwa JPM.
 
Mbona tukivuta msuba au kunywa gongo (local gin) mnatukamata kama kweli mnaamini katika asili ya mwafrika
 
Nime
Kulipa soko la Morogoro jina la chifu wa zamani hakuna maana ya kurudisha uchifu. Ni kumuenzi tu huyo chifu kwa mazuri aliyofanya. Nyerere alipoua uchifu mwaka 1963, pamoja na kwamba yeye alikuwa wa ukoo wa uchifu, bado alienzi machifu kadhaa kwa mazuri waliyoyafanya. Kwa mfano shule ya St. Mary's Tabora ilibadilishwa jina kuwa Milambo, ambaye alikuwa chifu wa hapo. Vilevile uko Iringa shule ya Southern Highlands ikaitwa Mkwawa, ambaye alikuwa chifu huko. Huko kulikuwa kuwaenzi tu hao machifu kwa mchango wao katika kupigana na mkoloni. Siyo kuashiria uzuri wa uchifu. Zaidi ya hayo haimaanishi cho chote kuhusu imani ya dini. Nyerere alikuwa Mkatoliki thabiti. Asingeweza kubadili jina la St Mary's kuwa Milambo kama kungekuwepo hapo suala la imani. Vivo hivyo kwa JPM.
Nimekuelewa kwa muktadha huo, sasa nakuuliza swali huyo Mkwawa na huyo Milambo ulio wasema hapo juu hawa walipinga kila aina ya kitu walicho leta wazungu kama mfumo wa serikali, siasa, dini ikiwemo Ukristo na Uislam, walitaka mila tamaduni, desturi na imani zetu zetu zidumu. Je. Kubadilisha jina la Mtakatifu Bikira Maria hadi kuwa Milambo ambaye mpinga Bikira maria, je Nyerere alikuwa anatumia akili gani?
 
Back
Top Bottom