Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Wananchi wengi wa nchi hii wanatamani nchi yetu iwe na Katiba mpya ambayo itaendana na nyakati hizi, tofauti na Katiba tuliyo nayo hivi sasa ambayo ilitungwa mwaka 1977, ambayo wananchi wengi wanaiona kuwa haikidhi matakwa ya sasa ya kisiasa na kijamii
Wakati wananchi wengi wanatamani nchi yetu iwe na Katiba mpya, iliyoboreshwa na itayompunguzia madaraka makubwa mno aliyopewa Rais, hali ni tofauti kwa Rais wa nchi, ambaye anatamani nchi yetu iwe na Katiba mpya, ambayo itazidi kuminya zaidi haki za binadamu na itazidi kumuongezea madaraka
Uthibitisho wa hilo ni kauli aliyoitoa hivi karibuni Rais Magufuli kuwa anashangaa yeye apewe mamlaka kikatiba ya kuteua, lakini anyimwe uwezo wa kutengua!
Maneno hayo aliyoyatamka hadharani hivi karibuni wakati akiwahutubia wananchi
Huo ni ujumbe mzito sana, kuwa Rais huyu, haafikiani na baadhi ya ibara za Katiba hii iliyopo hivi sasa za yeye kupewa mamlaka ya kuteua bila kupewa uwezo wa kuwatumbua wateule wake!
Ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, zipo ibara ambazo zinampa mamlaka ya kuteua kwenye baadhi ya nafasi nyeti za watumishi katika nchi yetu, lakini hazimpi madaraka ya kutengua, kutokana na unyeti wa nafasi hizo
Miongoni ya nafasi hizo alizopewa mamlaka ya kuteua, bila kupewa uwezo wa kutengua ni pamoja na CAG na majaji wa mahakama kuu
Yeye anatamani katika kila nafasi aliyopewa mamlaka ya kuteua, vivyo hivyo apewe uwezo wa kutengua!
Hivi kwa "hobby" yake ya kuteua na kutengua, kama angepewa mamlaka hayo si nafasi zote wangekuwa wanafanya kazi ya "Praise and worship for Magufuli" kwa woga wa kutumbuliwa??
Kwa mwenendo wa kisiasa tunauona unavyoendelea ndani ya nchi yetu kwa hivi sasa, upo uwezekano wa kuwapata wabunge wengi wa CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, zaidi ya theluthi mbili, ambayo itawawezesha wabunge hao kupitisha muswada wa kuibadilisha Katiba ya nchi yetu
Kama tulivyoona, hali imebadilika hivi sasa, badala ya mkulima asiyejulikana kupeleka kesi mahakamani ya maombi ya kutaka ukomo wa vipindi vya kukaa madarakani kwa Rais uondolewe, hivi sasa yameanza kujitokeza majina maarufu, yaliyojiunga na mkulima huyo na kutamani Rais wetu aongezewe muda wa kutawala
Sote wananchi tumemsikia aliyekuwa Waziri mkuu wa zamani wa nchi hii, Mizengo Pinda, akieleza maoni yake mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kilichoketi huko Mwanza, kuwa anatamani Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala nchi hii, angalau kwa kipindi cha miaka 15!
Wakati wananchi tulio wengi nchini tunatamani Katiba hii tuliyo nayo iondolewe kwa kuwa ni Katiba ambayo imempa madaraka makubwa mno Rais wa nchi, kumbe Rais wetu "anatamani" tuwe na Katiba mpya ambayo itakuwa mbovu zaidi ya hii tuliyo nayo hivi sasa, itakayompa madaraka makubwa zaidi sawa na Mungu
Watanzania wote inatubidi tupinge kwa nguvu zetu zote mipango hiyo "inayoandaliwa" kwa siri na watawala wa awamu hiii ya kutaka kurekebisha Katiba ya nchi hii tunayoiona kuwa mbovu, ili watuletee Katiba nyingine mbovu zaidi, itakayompa madaraka makubwa zaidi Rais na itakayoondoa ukomo wa Rais kutawala