I
Ingependeza sana maana mtu akikaa muda mrefu kwenye madaraka na anajua atafia pale hawezi kuwa na vitamaa tamaa vya kujilimbikizia mali 😳🙄
Hii Demokrasia ya miaka mitano Uchaguzi kisha baada ya miaka kumi anakuja Rais mwingine mimi huwa sioni nini hasa faida yake !
Kwa sababu hata matunzo yao na mafao yao na familia zao ni mzigo mzito kwa Wananchi wa kwenye Nchi zetu zinazoitwa Nchi masikini !
Kama anapatikana Kiongozi anayeongoza vizuri kwa kutumia sheria vizuri na kuifuata Katiba bora itakayo kuwa imepatikana bila upendeleo wowote hakuna sababu ya kuweka ukomo wa URAIS wa miaka 10 !
Kama anaongoza vizuri na anaziangalia vizuri mali za Nchi aachwe aendelee tu mpaka mwisho wa maisha yake huku akiwa anatayarishwa mwingine wa mfano wake 😳 !
Uongozi ni kipawa haupatikani kwa mtu anayepigiwa kura tu 😳
Wengine wanaweza wakapigiwa kura nyingi au kura kidogo lakini hawana vipawa na wakawa viongozi 😳!
Au nasema uongo ndugu zanguniii 😳😳🙄🙄 !