Rais Magufuli leo Dec 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwataka Watanzania kusajili laini zao kwa alama za vidole kama ilivyoelekezwa na TCRA, JPM ametangaza kuongeza siku 20 kwa ambao hawajakamilisha zoezi hilo.
_
Rais Magufuli amefanya usajili huo wa laini yake kwa alama za vidole Chato, Mkoani Geita ambapo ameongeza siku 20 kuanzia Jan 01, 2020 hadi Jan 20, 2020 kwa wote ambao watashindwa kusajili laini zao katika kipindi cha kuishia December 31, 2019 kama ilivyotangazwa na TCRA.
_
Rais Magufuli amesisitiza kuwa baada ya siku 20 alizoongeza kukamilika hakuna kisingizio chochote kitakachokubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa “usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni muhimu kwa usalama wa nchi, unaepusha uhalifu”