Zoezi hili ni nyeti sana ukilinganisha na malengo ya serikali ya kuanziahwa kwake. Kinachonisikitisha ni zoezi hili kufanywa na vijana wasio wazalendo ama ni sababu za njaa au la.
Kilichonifanya nilete bandiko hapa, wiki moja iliyopita nilipita njiani nikamkuta kijana anasajili laini za simu. Mimi pia nikaona nisajili laini yangu moja iliyobaki, laini zingine tayari nilikuwa nimeshazisajili, zamu yangu ilipofika yule kijana alianza kunihudumia, alianza akinitaka kutaja namba ya kitambulisho nikafanya hivyo, kisha nikataja namba yangu ya simu baadaye alama za vidole nikaweka, sina uhakika kama mpangilio wa utaratibu ni sahihi, nikaona taratibu hizi ameanza kuzirudia, tena akanipiga picha, hili la kupigwa picha ndiyo lililonishangaza zaidi na kunipa wasiwasi mkubwa.Sababu laini zangu zingine nilizosajili hakukuwa na utaratibu kama huo. Nilimwambia yule kijana kwamba ninawasiwasi na utaratibu anaoutumia kusajili laini za simu na kwamba huenda kitambulisho changu anatumia kusajilia namba ya simu isiyoyakwangu. Yeye akanijibu basi kama ninawasiwasi niende kwa kijana mwingine aliyekuwa jirani yake ambaye pia alikuwa wajisajili laini.
Niliamua kuondoka kuelekea kwenye ofisi za Halotel kwa kuwa nilikuwa mjini niliamini kule wasingeweza kufanya ujanjaunja kama kijana wao alivyotaka kuniingiza mjini, nilipofika nakueleza shida yangu nilianza kusajili laini yangu. Yule msajili Kila akitaka kukamilisha usajili unagoma. Kumbe ile laini yangu ilikuwa imeshasajiliwa tayari na Yule kijana wa kwanza ndipo nikaamini kwamba alikuwa akakamilishia usajili yale mengine aliyotaka kuendelea nayo ilikuwa janjajanja tu. Sijui hizo laini wanazosajili kwa kutumia vitambulisho vya watu wengine wanazipeleka wapi wasiwasi wangu mkubwa yasijeyakawa yaleyale kama ilivyosasa kabla ya ujio wa wa zoezi la usajili wa laini kwa alama za vidole.
Nawasilisha