Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri, ila rais wa Tanzania siyo mjumbe wa baraza hilo bali ni Mwenyekiti wa baraza. Hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ya nwaka 1977.
Lakini interesting, ni kwamba rais wa Zanzibar, ni mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT, impliedly, rais wa Zanzibar katika JMT ni waziri wa Zanzibar.
Sijui waandishi wa Katiba ya JMT, 1977 walikuwa na lengo na au maana gani.
Lakini ajabu nyingine, Katiba ya Zanzibar ya 1984 toleo 2010, inasema Zanzibar ni nchi na ina rais, ila Katiba ya JMT, rais huyohuyo anatambuliwa Kama Waziri, impliedly, Waziri wa Zanzibar.
Ninafikiri tuna haja ya kusawazisha haya Mambo. Ni mengi.
Waziri Mkuu wa JMT hatambuliki Kikatiba huko visiwani, lakini pia, Katiba ya JMT inamtambua Waziri Kiongozi wa Zanzibar, wakati Katiba ya Zanzibar haimtambui maana hicho cheo kilifutwa 2010.
Katiba ya Zanzibar inawatambua Makamo wa Kwanza na wa Pili wa Zanzibar wakati Katiba ya JMT haimtambui hilo Jambo.
Sasa sijui, kiitifaki Makamu wa rais wa JMT akiwa pamoja na hawa Makamo watatambulikaje.
Lakini pia rais wa Zanzibar anakuwa anaapa mbele ya Majaji Wakuu wawili, ameapa mbele ya Jaji Mkuu Zanzibar kuwa rais wa Zanzibar, na anaapa kwa Jaji Mkuu wa JMT kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri. Labda ni sawa; lakini, mbona Makamu wa rais hali kiapo mara mbili ilihali naye ni mjumbe wa cabinet?
Katiba hizi zinahitaji mapitio ili zilinganishwe mana Sasa ni muda mrefu Katiba ya JMT haijarekebishwa since 2008 ambapo ilirekwbishwa.
Kabla ya 2008 ilirekwbishwa 2005, 2002, 1998, nk.