Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Waziri Nape Nnauye amezifungia timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na serikali.

Hii ni kufuatia baadhi ya mashabiki kuvunja viti jana.

CtwZvCLWYAAPRRS.jpg


---------
Kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mh.Nape Nnauye leo akiwa ndani ya uwanja wa Taifa kuangalia uharibifu uliofanyika ktk mechi ya Simba na Yanga,Nnauye anasema jana alipigiwa simu na Mh.Rais JPM na akawa amekasirika sana kwa kitendo kilichofanywa na mashabiki wa pande zote mbili,upande wa nje karibu mageti nane ya upande wa Simba na Yanga yamevunjwa na ndani upande wa Simba kuna viti karibu 1782 zimeharibiwa.

Ghalama ya kila kiti ni shilingi laki mbili,hivyo kwa jumla ya ghalama ya viti tu bila mageti ni karibu milioni 300.Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.Pia serikali imeamua kuzuia mapato yote ya Simba na Yanga mpaka hapo watakapothibitisha kulipa uharibifu wote uliofanywa na mashabiki wao.

Mh.Nnauye anasema wataenda mbele zaidi kwa kuweka kamera uwanjani ili waweze kunasa sura za mashabiki watakaokuwa wanafanya vitendo vya uharibifu.

Chanzo kikubwa cha vurugu katika mechi ya jana ilikuwa ni mambo mawili;kwanza ni mfumo wa kadi kufeli,kadi nyingi "ukichambisha" zilikuwa zinasema kadi fake na hapo mtu katoka kununua kwenye kituo halali na kwa watu halali,na kadi nyingine zinasema huna salio la kutosha.Na hata ukienda kwa polisi basi unaambulia kirungu au kofi kwa kudhaniwa ni "usanii"

.Hali hii ndio ilisababisha watu waanze kuvamia mageti kwa kuona hakuna namna.Kadi umekata na uwanjani usiingie.Serikali imtazame upya mzabuni aliyepewa kazi ya kuuweka mfumo wa kielectroniki ambaye majaribio yake ilikuwa ni mechi kubwa ya Simba na Yanga.Mfumo ulionyesha kushindwa kabusa kabisa.Mpaka saa kumi jioni,upande niliokuwepo watu karibu 500 kadi zao zilikuwa zinagoma.

Sababu ya pili ni Refa Saanya.Huyu maamuzi aliyoyafanya anastahili adhabu.Hili si la kuongelea sana maana lipo mikononi mwa bodi ya ligi,TFF na Chama cha Waamuzi.
 
Baada ya Uharibifu mkubwa wa Viti vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliokuwa unafanywa mara kwa mara na Mashabiki wanaoongozwa kwa Mihemko, Hasira na Matumizi yatokanayo na vilevi vikali kama Bange, Mirungi, Viloba n.k yaani Mashabiki wa Simba SC kwa nyakati Tofauti Tofauti umesababisha wizara husika kupitia waziri Nape Nnauye kupiga Marufuku klabu za Simba SC na YANGA SC kutumia uwanja huo kwa mechi za LigiKuu kuanzia hivi leo.
 
Duuh hapo itabidi waende uhuru ambako pitch yake ni mbovu sana ile.
Na vilabu vyetu vipate akili vijenge viwanja zao sasa naamini ule ungekuwa uwanja wa simba ingekuwa ni ngum washabiki kung'oa viti hata kama wana hasira kias gani
 
Tutaona!! Usipotumika na simba au chura Unadhani nani atatumia
 
Maamuzi ya kimiemko na mwendokasi . Kitengo kitawarudisha.
 
Sijui kama hiyo marufuku itadumu wakati wote. Cha msingi tuangalie wapi tulipojikwaa tusiangalie tulipoangukia. Hivi unafikiri kwa marefa kama wale soka letu litapiga hatua???!
Mkuu hapo hamna cha kujikwaa wabongo wengi ni wapuuzi sana haswa linapokuja suala utunzaji mali za uma. Refa kuharibu mchezo halina uhusiano na viti. Refa atahukumiwa na wahusika baada ya mchezo. Nakumbuka siku ya ufunguzi ya ule uwanja watu waliiba koki vyooni. Sasa kama hapo utasema bahati mbaya
 
Ni vema kabisa.. Hata huo wa uhuru wasipewe wakacheze moro au viwanja vingine sio lazima dar.. Mbona kagera sugar walihamia kirumba kama uwanja wao wa nyumbani...!
Wakiufanya uwanja wa jamhuri moro kuwa uwanja wao wa nyumbani itaongeza msisimko wa mpira morogoro.
 
Back
Top Bottom