Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Hakuna busara yoyote ya kuufungia. Tumu ikiliyosababisha uharibifu iadhibiwe kwa kufanya matengenezo yanayohusika. Kwa hali ilivyo sasa kuchezesha Yanga na Simba nje ya uwanja huo ni kukaribisha madhara zaidi hayo. Mihemuko michezoni si ajabu, pande zote zikae ziangalie tatizo lilikuwa wapi.
 
Mkuu hapo hamna cha kujikwaa wabongo wengi ni wapuuzi sana haswa linapokuja suala utunzaji mali za uma. Refa kuharibu mchezo halina uhusiano na viti. Refa atahukumiwa na wahusika baada ya mchezo. Nakumbuka siku ya ufunguzi ya ule uwanja watu waliiba koki vyooni. Sasa kama hapo utasema bahati mbaya
Hilo unalolisema ni kweli kabisa, Watanzania hatuna uchungu na mali za umma na kwa kulifahamu hilo inatakiwa kuwe na utaratibu wa kubaini wahusika ili waadhibiwe. Kuwe na tiketi zinazoweza kuhifadhi taarifa za mtu anayeikata na pia kuwe na kamera za kutosha ili kurekodi matukio yanayoendelea pale uwanjani.
 
Maamuz ni sahih ila hela ya simba na yanga ilivyo tamu watarud wenyewe
 
Nimesikitishwa na hilo tamko kupindukia ,Kwani wahuni wachache si wawakilishi wa wanachana na mashabiki wa simba dunia mzima.Tunaipenda simba yetu daima
 
Kama Kahisi Kung'oa Viti Ndiyo Tatizo!! Basi Kwenye Kiwanja Chengine Refa Akituletea Utumbo Kama Wa Jana, Uwanja Tunaupiga Matuta Wote Halafu Tunaoondoka Na Magoli!!
Hatutaki Ujinga Wa Kununua Marefa sisi.


Povu jiiiiiiiingi!

Una kucha za chuma kuweza kufanya hayo maamuzi? au ndio mbwembwe ili muonekane kwenu ni sawa kuhamishiwa Shamba la Bibi?

Wewe unacheka kuhamishiwa shamba la Bibi, Waulize viongozi kwanini walipakataa pale, ikiwa wao ndio walikuwa wa kwanza kuandika barua kuukataa uwanja.

Usiendekeze UMBUMBUMBU!
 
Sawa tu maana sifaidiki na chochote


Ni kweli ila hasara zipo kwa wale walio Andika barua kupelekwa/kuhamishiwa uwanja wa Taifa kutoka Shamba la Bibi.... Na sasa wameamishiwa huku shamba la Bibi kutokana na Mashabiki wao wahuni kufanya upuuzi pale Taifa.
 
Baada ya Uharibifu mkubwa wa Viti vya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliokuwa unafanywa mara kwa mara na Mashabiki wanaoongozwa kwa Mihemko, Hasira na Matumizi yatokanayo na vilevi vikali kama Bange, Mirungi, Viloba n.k yaani Mashabiki wa Simba SC kwa nyakati Tofauti Tofauti umesababisha wizara husika kupitia waziri Nape Nnauye kupiga Marufuku klabu za Simba SC na YANGA SC kutumia uwanja huo kwa mechi za LigiKuu kuanzia hivi leo.



wakati wanajenga wachina taifa kwa billioni 60, Nigeria, wajerumani walikuwa wanajenga uwanja kwa shilingi billion 600 za ki tz! wapelekwe simba na yanga huko tuone kama wata ng'oa vitu! cheap is expensive
 
Katizo ni very tempo.sasa mashine za kielekroniki za tiketi zitaoza...???? MH.WAZIRI angepiga marufuku watazamaji ktk mechi hizo.Na kwani zinakuwa ngapi kwa mwaka..???? Au hata simba na Jkt ruvu hakuna uwanja wa taifa..????
 
wakati wanajenga wachina taifa kwa billioni 60, Nigeria, wajerumani walikuwa wanajenga uwanja kwa shilingi billion 600 za ki tz! wapelekwe simba na yanga huko tuone kama wata ng'oa vitu! cheap is expensive
Wapuuzi sana hawa Mashabiki wa Simba aisee! Sijui waling'oa viti kumkomoa Yanga, TFF au Serikali?
 
Kosa alilofanya mkude ( kumpiga mtama refa) na kupelekea kulimwa red card ndiyo kilichopeleke uvunjikaji wa amani, hivyo TFF inapaswa imfungie kucheza soka maisha, hakuna kuzungusha zungusha maneno apo!
 
Kwanza timu zijenge viwanja vyao, klabu zina karibu karne zimejiimarisha kwenye majungu na ndumba tu
Usijali mkuu! Sisi kama Mabingwa mara 2 mfululizo, Mabingwa watetezi, Mabingwa mara 26 wa kihistoria yaani Dar es Salaam Young Africans SC tumepatiwa ekari 715 huko uzunguni.........

Mambo mazuri yanakuja!
 
Wapuuzi sana hawa Mashabiki wa Simba aisee! Sijui waling'oa viti kumkomoa Yanga, TFF au Serikali?

mihemko ipo mkuu kwenye mpira ni part ya mchezo! tengeneza kilicho bora tuone kama vitang'oka, sio unaleta vitu inferior! pata picha mkuu ume bet mke vs mke halafu refa ana khanisi inakuwaje hasira zake!
 
safi sana TFF wamevuna walichopanda,wakishakosa mapato akili zitawaingia kuendesha soka kwa weledi
 
Back
Top Bottom