Acheni kumhusisha Rais kwa kila jambo...kuna harufu ya uongo hapa...thibitisha kama Rais ameagiza isitoke hata senti mpaka gharama zifidiwe....waliofanya fujo ni Simba kwa maana ya baadhi ya wapenzi wa Simba...Ni wahuni wachache wa samba wakiungwa mkono na baadhi ya viongozi wachache wa Simba ambao wana hulka ya hooliganism na siyo uongozi...walichofanya baadhi ya mashabiki hao wa Simba ni kukosa ustaarabu na kitendo chao cha kuvunja viti ni cha kishenzi bila kumung'unya maneno....Huwezi kuharibu viti uwanjani eti kwa kuwa refa 'amewaonea' kwa maamuzi...Hata kama refa amekosea ikumbukwe kuwa yewye pia ni binadamu....kwa walioangalia mpira leo kati ya Arsenal na Burnley watagundua kuwa goli lile alilofunga Koscielny lilikuwa la utata likiaminika kuwa mpira umemgusa mkononi...lakini hatukuona wapenzi wa Burnley wakivunja viti...Wala hatukuona mchezaji wa Burnley akimsukuma refa na kumdondosha chini....Refa pia ni binadamu na anaweza kufanya makosa....miaka michache iliyopita mchezaji wa Simba madaraka Selemani aliu-control mpira kwa mkono na kufunga goli dhidi ya Yanga lakini Yanga hawakuvunja viti....Huko ulaya mabao ya mkono ni mengi kama lile la Ufaransa la Thiery Henry kwenye michuano ya awali ya kombe la dunia...Maradona pia aliwahi kufunga bao la mkono kati ya Argentina na England kwenye kombe la dunia lakini hatukuona viti vikivunjwa....Wanaopaswa kuadhibiwa hapa ni Simba na siyo Yanga....Tuache siasa za mpira hapa Tanzania...Yanga haihusiki na uhuni wa jana...kuvunjwa kwa mageti ni kosa la uongozi wa uwanja kutokana na utaratibu mbovu wa kuingia uwa jani na siyo vinginevyo....
Kwa Mujibu wa Nape kupitia ITV habari na Azam two habari saa mbili usiku wa Leo na kasema kapigiwa simu na Rais kuonesha kukasirishwa kwake na tukio Hilo, uharibifu wa Jana unahusisha pia kuvunjwa Mageti wakati wa Kuingia jee nalo hili linawahusu Simba peke Yao?