Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Rais Magufuli asikitishwa na vurugu za mechi ya Simba na Yanga,Sasa zazuiwa kutumia Uwanja wa Taifa

Acheni kumhusisha Rais kwa kila jambo...kuna harufu ya uongo hapa...thibitisha kama Rais ameagiza isitoke hata senti mpaka gharama zifidiwe....waliofanya fujo ni Simba kwa maana ya baadhi ya wapenzi wa Simba...Ni wahuni wachache wa samba wakiungwa mkono na baadhi ya viongozi wachache wa Simba ambao wana hulka ya hooliganism na siyo uongozi...walichofanya baadhi ya mashabiki hao wa Simba ni kukosa ustaarabu na kitendo chao cha kuvunja viti ni cha kishenzi bila kumung'unya maneno....Huwezi kuharibu viti uwanjani eti kwa kuwa refa 'amewaonea' kwa maamuzi...Hata kama refa amekosea ikumbukwe kuwa yewye pia ni binadamu....kwa walioangalia mpira leo kati ya Arsenal na Burnley watagundua kuwa goli lile alilofunga Koscielny lilikuwa la utata likiaminika kuwa mpira umemgusa mkononi...lakini hatukuona wapenzi wa Burnley wakivunja viti...Wala hatukuona mchezaji wa Burnley akimsukuma refa na kumdondosha chini....Refa pia ni binadamu na anaweza kufanya makosa....miaka michache iliyopita mchezaji wa Simba madaraka Selemani aliu-control mpira kwa mkono na kufunga goli dhidi ya Yanga lakini Yanga hawakuvunja viti....Huko ulaya mabao ya mkono ni mengi kama lile la Ufaransa la Thiery Henry kwenye michuano ya awali ya kombe la dunia...Maradona pia aliwahi kufunga bao la mkono kati ya Argentina na England kwenye kombe la dunia lakini hatukuona viti vikivunjwa....Wanaopaswa kuadhibiwa hapa ni Simba na siyo Yanga....Tuache siasa za mpira hapa Tanzania...Yanga haihusiki na uhuni wa jana...kuvunjwa kwa mageti ni kosa la uongozi wa uwanja kutokana na utaratibu mbovu wa kuingia uwa jani na siyo vinginevyo....

Kwa Mujibu wa Nape kupitia ITV habari na Azam two habari saa mbili usiku wa Leo na kasema kapigiwa simu na Rais kuonesha kukasirishwa kwake na tukio Hilo, uharibifu wa Jana unahusisha pia kuvunjwa Mageti wakati wa Kuingia jee nalo hili linawahusu Simba peke Yao?
 
Watatumia uwanja gani? Wekeni njia mbadala za
kutatua matatizo kama ya kadi, kuwaelimisha mashabiki na wakifanya uharibifu basi mzuie pesa zao lakini sio kusema wote waadhibiwe kuto tumia uwanja wa taifa sabb ya wavuta bangi wachache.....
Ulaya wao hutumia camera kuwabaini mashabiki wakorofi na maamuzi ya refa hayawezi kuharibu viti au chochote uwanjani, mashabiki wa simba ndiyo waling'oa viti kwa hiyo pesa zikatwe kwenye mgao wa simba na mageti kila geti walipishwe kwani geti la yanga lilivunjwa na mashabiki wake.
 
Kwa Mujibu wa Nape kupitia ITV habari na Azam two habari saa mbili usiku wa Leo na kasema kapigiwa simu na Rais kuonesha kukasirishwa kwake na tukio Hilo, uharibifu wa Jana unahusisha pia kuvunjwa Mageti wakati wa Kuingia jee nalo hili linawahusu Simba peke Yao?

Hatubishi kuwa hajapigiwa simu...tunachohoji ni nyie (na siyo comrasde Nape) kusema kuwa Rais amesema kuwa isiondolewe hata senti moja mpaka gharama zifidiwe...Nape hajasema hivyo yaani hajamhusisha Rais kwa maneno hayo....
 
Sasa hapo Yanga inaadhibiwa kwasababu gani? Kitendo cha kuzuia mapato ya Yanga kitawapa kiburi Simba ambao bila shaka wangekuwa tayari kugharamia uharibifu uliofanywa na mashabiki wao. Anyway, Azam wametengenezewa fedha za uwanja.
Ni kweli mkuu washabiki wa simba ndiyo waliharibu viti na simba ndiyo inapaswa kupewa adhabu ikiwemo washabiki wake kuzuiwa kuingia uwanjani lakini kule nje kuna mashabiki wa yanga waliharibu geti huko napo yanga itabeba jukumu la kurekebisha uharibifu huo.
 
Simba walipe gharama za viti pia geti lao lililovunjwa na yanga na wao wakatwe kugharamia geti moja lililovunjwa na mashabiki wake.
 
inafurahisha huku simba wanamsema Mwigulu aache unazi wa Yanga , huku Yanga wanasema Nape aache unazi wa Simba.....

Ningekuwa Magu pesa yote ya Jana wasingepata na kuwafukuzia wakachezee huko mkwakwani na morogoro
Kwanza kuendelea kuwaacha simba na yanga wautumie huo uwanja ni kuwadekeza..
Walipaswa wawe na viwanja vyao..
 
Nape unatakiwa kutoa maamuzi ya haki na sio ushabiki. Unapozuia mapato ya Yanga kwa sababu zipi!!! Unapo generalise kuwazuia Simba na Yanga kwa makosa ya mashabiki wa Simba sio tu unaonyesha ushabiki wako Simba bali chuki yako dhidi ya Yanga. Acha TFF watumie kanuni zao zilizopo. Kama NAPE ataendelea kuwaadhibu Wana Yanga kwa kosa la Wan Simba. Naomba viongozi wa Yanga watangaze kwa wana yanga nchi nzima kuwa NAPE NI ADUI NAMBA MOJA WA YANGA. Yeye NAPE asipotezee matatizo yaliyojitokeza kwa kushindwa kwa mitambo ya elektroniki kufanya kazi siku ya mechi.
Mkuu ulaya wao hutoa adhabu kwa washabiki husika mfano walioharibu viti ni wa simba hivyo wanapaswa kuwakata simba kufidia hasara na yanga pia kule nje mashabiki walivunja geti nayo wakatwe kidogo kwani ukilinganisha uharibifu wa mashabiki wa simba ulikuwa mkubwa zaidi
 
Kwa Mujibu wa Nape kupitia ITV habari na Azam two habari saa mbili usiku wa Leo na kasema kapigiwa simu na Rais kuonesha kukasirishwa kwake na tukio Hilo, uharibifu wa Jana unahusisha pia kuvunjwa Mageti wakati wa Kuingia jee nalo hili linawahusu Simba peke Yao?
kwa upande wa mageti ni pande zote kwani mageti ya yanga na mageti ya simba yalivunjwa
 
barafu. "kuchambisha" huu Msamiati mpya? Hata hivyo ni maamuzi ya Jazba Uwanja siyo wa aliye JUU au Nape, ni Mali yetu itafutwe njia ya adhabu.

Kwa Tanzania ya viwanda Hilo linawezekana.
 
View attachment 410879 ......................................Mh.Nape Nnauye anasema Rais amekasirika sana kwa kitendo hicho na alitaka adhabu iwe kali zaidi lkn wakaamua kama serikali ni kufungia Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka hapo serikali itakaposema vinginevyo.............
hivi ninyi Simba na Yanga huku kunyanyapaliwa ni hadi lini?

badala ya kulialia hapa, tumieni unyanyapaaji huu kama fursa ya kupiga maendeleo kwa kujenga viwanja vyenu wenyewe.

ebo!!!
 
Kama Juma Punda Maharage hajui Simba na Yanga zina wafuasi wengi kuliko CCM na UKAWA kwa pamoja
Tusimlaumu sana, ukitoka mfano Rwanda utayajuaje haya?
 
Sisi wabantu ule uwanja ulitakiwa ujengewe viti vya zege, hatuna ustaarabu hata kidogo!
 
Kwanza kuendelea kuwaacha simba na yanga wautumie huo uwanja ni kuwadekeza..
Walipaswa wawe na viwanja vyao..

ni kweli serikali ndo inawaharibu sawa na mzazi anayelidekeza Toto la kiume la miaka 30 linakaa nyumbani na Dada zake
 
Viti vile havina gharama ya laki 2 Nape kaongeza tu namba labda uwe hujawahi fika Taifa ukakaa na kushuhudia mechi
 
Back
Top Bottom